REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

KAULI YA COMMON KUHUSU MAHUSIANO YA DRAKE NA SERENA WILLIAMS

2:06:00 AM Add Comment

IKUMBUKWE: Common aliwahi kuwa na Mahusiano na Mcheza Tennis Serena Williams ambaye Hivi sasa, ni “Mdandio” Mpya wa Drake.

Pia Mnamo Mwaka 2011, Common aliwahi kuingia katika Timbwili na Drake, huku kisa akiwa ni huyo huyo Serena Williams.

Sasa, Baada ya taarifa kuzagaa na hatimaye kuthibitika kabisa kuwa,  Serena na rapper Drake ni wapenzi na Wapo katika mahaba mazito, kauli ya Common ya kuwapa Baraka katika mahusiano yao, hatimaye Imetoka.

Common ambaye ni Mkongwe na Mbabe wa Hip Hop, amedai kuwa, Serena ni Rafiki yake, ingawa kipindi cha Nyuma wamewahi kuwa na mahusiano kipindi cha nyuma.


Lakini Kwa hivi sasa, kama Yuko “happy” na mahusiano Mapya, basi anamtakia kila la Kheri na hana tattizo Juu ya hilo






KIM KARDASHIAN NA KANYE WEST KULIPWA USD 440,000 KUTOKA KWA CO-FOUNDER WA YOU TUBE

1:12:00 AM Add Comment

HATIMAYE  Kesi imezaa Matunda ikiwa ni baada Ya Kanye West na Mkewe Kim kardashian West kufungua mashtaka hayo, kufuatia kuvujishwa kwa Video Clip yao wakati wa Kuvalishana Pete ya Uchumba.

MIAKA miwili iliyokata, Kim na Kanye, walifungua Mashtaka dhidi ya Co- Founder wa Youtube, Chad Hurley, ambaye inasemekana ndiye aliyevujisha Kipande hicho cha Video Kilichorekodiwa, bila Idhini ya Wanandoa hao.

Taarifa zinazidi kumiminika kuwa, Hurley alikuwa katika Eneo la Tukio, katika uwanja wa AT & PARK Huko San Francisco, na alifanya Shughuli ya Kurecord kwa Siri Kubwa, na kisha kukipost katika Youtube, kunako Kipengere chake kipya-MIXBIT.

Ingawa aliweza kubeba Umaarufu Mkubwa Ndani ya Dakika 15 Tu, Hurley anatakiwa kusalimisha Mkwanja huo, USD 440,000 sawa na 972,840,000 Za Kitanzania


Malipo hayo yanatakiwa kufanyika Ndani ya Siku Chache zijazo.

TAARIFA KUHUSU PICHA ZINAZOSAMBAA MITANDAONI ZIKIMTUHUMU TYGA KUSHIRIKI MAPENZI NA MWANAUME MWENZAKE.

2:50:00 AM Add Comment

KUPITIA Mtandao wa Twitter, Kuna picha ambayo imekuwa ikisambazwa na watu mbali mbali wakidai kuwa zinamuonesha Tyga akishiriki Tendo la Ndoa na Mwanaume Mwenzake.

Ingawa Ulimwengu wa Burudani na Mashabiki wa Tyga walipata Mshtuko na kuanza kujiuliza nini Kinachoendelea, Tyga alionekana kama ni mtu ambaye hakuwa na Mshtuko sana, badala yake alipost kuwa “Shetani Mwingine ameanza kazi”

Lakini baada ya muda kadhaa, ushahidi Mwingine ulitoka ukithibitisha kabisa kuwa, Kijana aliyeonekana katika picha hiyo, sio Tyga, na wala hana uhusiano na tyga, bali ni watu ambao wanaelekea kufanana.


Aidha, Fan Huyo wa Tyga, alipost Picha halisi ya Kijana ambaye alionekana katika Picha hiyo, na kuwafanya wengine wapumue na kuamini kuwa Ni Kweli sio Tyga

PICHA: JAGUAR NA SIZE 8 WANAPOMCHEZESHA STYLE YA "MATEKE" MAKAMU WA RAIS-WILLIAM RUTTO

1:38:00 AM Add Comment

MAKAMU WA RAIS NCHINI KENYA- WILLIAM RUTTO akicheza Style ya "Mateke" katika Jukwaa na Msanii jaguar pamoja na Size 8.

Jaguar alizindua Foundation(Taasisi ) yake inayoitwa JAGUAR YOUTH EMPOWERMENT FOUNDATION maalum kwa ajili ya Vijana.


TIZAMA PICHA NYINGINE





VIDEO: NIMEKULETEA MNYOO AMBAYE ANAWEZA KUKUPA PESA NDEFU SANA-KENYA

12:53:00 AM Add Comment

CITIZEN TV.
UNAWEZA Ukadhani labda Mnyoo huyu anaweza kuleta Pesa kupitia Njia Fulani hasa za Kishirikina, lakini Ni Tofauti Kabisa.

Nchini Kenya, Mnyoo hatari anayetambulika kwa Jina la GUINEA WORM, anasakwa Vibaya sana na Wataalamu wa Afya Nchini humo kwa ajili ya Kumuangamiza hara iwezekanavyo.

Kwa Mujibu wa CITIZEN TV, Wizara ya Afya nchini Kenya imekuwa katika harakati za kumsaka na kumwangamiza Mnyoo huyo, lakini kumekuwa na udanganyifu wa Hali ya Juu.

Dr. Sammy Mahugu-Afisa Uhamasishi (MOH) amefafanua kuwa, hivi sasa wameanzisha kampeni ya “Pata Pesa na Guinea Worm” ambayo itadumu kwa Miezi Mitatu.

Endapo utafanikisha kumpata Mtu ambaye ana Mnyoo huyo, basi utaweza kujishindia Ksh 100,000 kwa Wewe Mkazi wa Kenya.

Dr. Mahugu ameongeza kuwa, Mnyoo huyo ni Mrefu sana, na huwa anaingia katika Sehemu mbali mbali za Mwili kama vile Mguuni, Kichwani, Tumboni na hata Mkononi.

Kwa Urefu alionao Mnyoo huyo, na ili kumtoa Mzima mzima bila kubaki Mwilini, inaweza kugharimu Muda wa Wiki Nzima, huku maumivu yakiwa makali sana.


TIZAMA VIDEO HIYO HAPA:


(VIDEO)-MKE WA MTU NI SUMU:UUME WAKE UMEBAKI KUSIMAMA BAADA YA KULA URODA NA MKE WA MTU

12:03:00 AM Add Comment

Hii Imetokea Nchini Kenya

JOHN KAZUNGU ana historia ambayo hatoweza kuisahau katika maisha yake, ikiwa ni baada ya kujikuta akikutwa na Hisia za tendo la Ngono Bila kupungua, kwa Siku 14.

Sababu ambayo ilimfanya hata Uume wake usimame muda Wote, ni baada ya Kufanya mapenzi na Mke wa Mtu.


TIZAMA HALI HALISI ILIVYO HAPA:

KUNA KITU KINGINE KUTOKA KWA DIAMOND PLATNUMZ HIVI KARIBUNI?

2:57:00 AM Add Comment


Na baba Juti.
KUPITIA Instagram account Yake, Diamond ameonekana kufurahishwa sana na hatua ambayo Mkwaju wake wa Nana aliomshirikisha Mr Flavour, umefikia hasa kimataifa.

Video ya Mkwaju huo, ambayo iliongozwa na Director GODFATHER, hivi sasa imeshika Nafasi ya Kwanza katia Chat ya Muziki wa Afrika kunako Kituo Kikubwa Kimataifa, MTV base-Afrika.

Ili Kuonesha Furaha yake, “Baba Tiffa” alizama kunako Instagram na na kuandika Kuwa alitaka kuwataarifu mashabiki wake kuwa, Mkwaju huo umeshika namba Moja, hivyo anawashukuru kwa support yao. Pia wawe tayari kwa ajili Mzigo Mwingine.

TUNAMNUKUU.


Morning... jus wanted to tell you that, your favourite Song #Nanais Number one on the @mtvbaseafrica Official African Chart... thanks alot for your Support🙏 Get ready for Another HIT in TOWN!!!

SERENA APEWA ANAGALIZO KUHUSU DRAKE

2:46:00 AM Add Comment

Na Baba Juti
SIKU ya jana , Ulimwengu wa Mitandao ya Kijamii ulirindima na habari za Rapper Drake kunaswa na Serena Willliams katika hali ya Kimahaba kunako Mgahawa Mmoja Nchini marekani.

Lakini Licha ya Ukaribu huo Kupewa Baraka na baadhi ya wadau na mashabiki wa wawili hawa, bado kuna Onyo ambalo Selena Williams alionekana kupewa, huku akikisitizwa kuwa makini na rapper Huyo.

Kwa mujibu wa taarifa za kiuchunguzi, inadhihirika kabisa kuwa, Rapper drake kwa asilimia kubwa,amekuwa akipenda sana kukunjuka na akina dada wacheza Utupu kunako Night Clus (Strippers), Wapenda Ngono, na hata wanamitindo.

Moja kati ya Rafiki wa Serena, alidaiwa kumshauri Serena kuwa, inabidi asijisahau namna ambavyo Dreezy anafanya mambo yake.


Na Mpaka hivi sasa, Inasemekana kuwa, Mkali huyu wa BEST I EVER HAD, bado anapenda kujihusisha na akina dada wa aina Hiyo, jambo ambalo Serena anatakiwa kuwa nalo makini sana

TYGA: NAJISKIA POA KUFANYA MAPENZI NA BINTI MWENYE UMRI MDOGO

2:38:00 AM Add Comment

KUTOKA BLACK TOUCHEZ
KYLIE JENNER, Girlfriend Wake na Tyga, ana Umri wa Miaka 18 akiwa na Umri wa Miaka 25.

Kitu hicho kimekuwa kikiwafanya Mashabiki wake wengi wajikite zaidi hasa katika Kumkosoa, kwa Kuwa na mahusiano na Binti Mwenye Umri Mdogo, Ukizingatia walianza mahusiano Kylie akiwa na Umri wa Miaka 17.

Sasa, ili kudhihirisha Kuwa, amechoka kauli hizo ambazo kiujumla huwa zinamkwaza, ukizingatia anahitaji kuwa happy, Tyga ameamua kuwajibu kupitia Mkwaju ambao kiujumla unaonekana kabisa kumzungumzia Kylie Jenner ambaye anasakamwa katika Suala zima la Umri.

Katika Mkwaju Huo uliopewa jina la STIMULATED, Tyga anafafanua kuwa hata kama watu wanazungumza sana, ila yeye yuko Sawa na anaenjoy na hata Kuridhika kufanya tendo la Ndoa/ Mapenzi na Binti Mwenye umri Mdogo.

Moja kati ya Mistyari amabyo inasikia kunako Mkwaju huo ambao umejaa 
maneno makali, ni kama Ifuatavyo:

 “They say she is young/ I shoulda waited. She a big girl, dog, when she stimulated/She a big girl dog, I’m puttin’ in. Yeah I’m penetrating,”


Lakini Pia, Melody ya Mkwaju Huo, imechukuliwa kunako wimbo wa CHILDREN wa ROBERT MILES.

ISIKILIZE HAPA (Explicity Content)



KUTANA NA CELEBS 5, KATI YA 10, AMBAO RAPPER DRAKE AMEKUNJUKA NAO…

2:57:00 AM Add Comment

KUTOKA BLACK TOUCHEZ,
WENGI tulikuwa tukidhani kuwa Rapper Kutoka YMCMB, Drake, alikunjuka na Robbin Fentty Rihanna Peke yake, lakini kumbe kuna Wengine ambao wanamajina yao katika Burudani Industry ulimwenguni kote.

Wafukuza mapepo Leo Tunashusha Full List ya Waliofyatuka na Dreezy katika Kitu kinachofahamika kwa Jina la Mahaba.


1. SELENA WILLIAMS-2015.
Dreezy alianza kuonekana  karibu na Serena Williams ambaye ni Mcheza Tenis asiyeshikika, aktika Baadhi ya Mechi ambazo amekuwa akishiriki. Tofauti na Hilo, Hivi karibuni, wawili ahoa walionekana kuwa pamoja katika Moja ya Migahawa , na ilikuwa ni mazingira ya Usiku.

Mnamo Mwaka 2011, Dreezy alijikuta akiingia katika Bifu kali na rapper Common baada ya kusadikika kuwa anakunjuka na Serena, ikiwa kipindi hicho Common na Serena walikuwa ndo kwanza wamepigana Chini.

Common alifikia hatua ya kuthibitisha kuwa ni kweli amepigana Chini na Serena, na alifahamu kabisa kuwa Drake na Serena Walikuwa na mahusiano, kitu ambacho hakuwa na Shida Nacho. Lakini kilichomfanya aanzishe noma na Dreezy, ni baada ya kuhisi kuwa, Nyimbo Nyingi zilizokuwa zikitungwa na rapper Huyo kutoka Toronto Canada, zilikuwa zikimhusu Yeye (Common)


2. RIHANNA : 2009-2010
UHUSIANO wao ulianza kufahamika kuanzia Mwaka 2009 mpaka 2010 ambapo wawili hawa hawakuweza kupiga hatua Nyingine.

Kipindi Hicho Riri alikuwa amepigana Chini na Breezy, lakini Mwisho wa siku akajikuta akiangukia Mikononi mwa Rapper Huyo aliyevunja na Mkwaju wa STARTED FROM THE BOTTOM.

Lakini baada ya Kupigana Chini, Dreezy alifyatuka kuwa, Kitendo ambacho Rihanna alimfanyia, ni malipo ya kile ambacho Drake mwenyewe aliwafanyia wanawake wengine ambao aliwahi kuwa nao katika mahusiano.


3.TYLA BANKS.
INGAWA Hakuweza kudandiana naye Kimahaba, Darke alithibitisha kuwa, aliwahi kumfukuzia Bibi Huyu ambaye ni hatari katika Suala Zima la mitindo.

Akikiri hilo, Dreezy alidai kuwa ni kweli aliwahi kuenjoy naye vizuri katika Date Night yao, ambapo walienda eneo pendwa sana Nchini marekani, DISNEY.


4. CAT WASHINGTON : 2009
CAT WASHINGTON alifahamika sana kupiti Kipindi cha TV kinachofahamika kwa jina la BAD GIRLS CLUB.
Dreezy alikutana na Bibie huyu kupitia Video ya BEST I  EVER HAD, na ilikuwa ni Mwaka 2009.

Washington anadai kuwa, aliweza kuenjoy sana na Drake, na kila mmoja alikuwa amekufa ameoza kwa mwenzake, hivyo lilikuwa ni Penzi tamu sana.


5. KEISHA CHANTE.
KEISHA amewahi kuwa Mtangazaji wa Kipindi cha 106 & PARK cha BET,. Na aliweza kutengeneza Jina kubwa sana kupita Maelezo.

Kwa mujibu wa maelezo yake, Keisha na Drake waliwahi kuwa na mahusiano wakiwa na Umri wa Miaka 14, kitu ambacho anadai walikifurahia sana.


Keisha anasema kuwa, walikutana baada ya Yeye kuhamia Toronto-Canada kwa ajili ya Shughuli za Muziki, na kipindi hicho Drake alikuwa yuko katika Tasnia ya Burudani.

PICHA NNE: LOWASSA AKIWA KATIKA SOKO LA TANDALE

2:42:00 AM Add Comment

Mgombea Uraisi wa Chadema anayewakilisha UKAWA Mh Edward Lowassa leo ameendelea na ziara yake ya kutembelea wananchi katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam! Leo asubuhi alitembelea eneo la Tandale.




ZITTO KABWE: “WASANII WA TANZANIA, KAMPENI ZIKIISHA, NA THAMANI YENU IMEISHA”

2:38:00 AM Add Comment

KUTOKA BLACK TOUCHEZ
MGOMBEA Ubunge kwa Jimbo la Kigoma Mjini Kwa Tiketi ya ACT-MAENDELEO, Zitto kabwe, ameamua kuwatolea Uvivu wasanii mbali mbali Nchini Tanzania, ambao kiujumla hivi sasa wameelekeza Macho yao katika Siasa.

Katika Kufafanua zaidi, Zitto ameonekana kukwazwa zaidi na namna ambavyo wasanii ambao hivi leo wanawaimbia Viongozi wa Siasa ambao Kiujumla hawakuwahi hata kuzungumzia Suala lolote linalohusu Mslahi yao.

Zitto kayasema hayo Kupitia Instagram account yake, ikiwa ni baada ya Kupost Picha ya Mohamed Mwikongi-Frank, ambaye anagombea Ubunge Pia kwa Ticketi ya ACT.

Tunamnukuu
“Wasanii wa Tanzania, wakati tunatetea kazi zenu kurasmishwa ili mfaidi jasho lenu, hawa mnaowaimbia Leo hawaikuinua mdomo wao kuwatetea. Kampeni zikiisha na thamani yenu imeisha. Tulipopaza sauti kupinga unyonyaji wa makampuni ya simu kwenye RBT hawa wanaoahidi kuwatetea Leo hata habari walikuwa hawana. Naomba mtafakari sana hatma ya tasnia yenu.”


MNAZUNGUMZIAJE KAULI YA ZITTO.

TAARIFA KUHUSU UJAUZITO WA MARIAH CAREY

1:45:00 AM Add Comment

MITANDAO mbali mbali ya Kijamii Nchini marekani, ilianza kutoa taarifa kuwa Mariah Carey (45) hivi sasa ni mjamzito.

Lakini kama haitoshi, jamaa ambaye alitajwa kuhusika na Ujauzito huo, ni Billionea JAMES PACKER, tajiri ambaye anamiliki CASINO mbali Mbali Nchini Marekani.

Lakini Baada ya taarifa Hizo Kuzagaa na hata kupambwa haswa, hatimaye Mtandao wa Gossip Cop ulifyatua jibu kuwa, Carey na Mpenzi wake huyo , hawatarajii kupata Mtoto yeyote, na taarifa ambazo zinazidi kusambaa, hazina ukweli wowote.


Mariah carey ambaye Hivi sasa ana watoto wawili wenye Umri wa Miaka 4, alianzisha mahusiano yake na James Packer, ikiwa ni baada ya kuachana na Mumewe wa Ndoa, NICK CANNON.

DRAKE NA SERENA WILLIAMS…HALIFICHIKI PEMBE LA NG’OMBE

1:05:00 AM Add Comment

HATIMAYE yametimia ikiwa ni dhahiri kabisa kuwa Zile Fununu za Drake na Serena kuanzisha Uhusiano wa Kimapenzi, zimekuwa KWELI.

Kwa Mujibu wa Mtandao wa TMZ, Serena na Dreezy walionekana wakipeana “Mabusu-Mahaba”  Katika Mgahawa wa CINCINNATI, Weekend Hii (AUGUST 23).

Wawili hao kwa mara nyingine walionekana wakipiga  “Dinner” Kibongo Bongo tumezoea kusema Chakula Cha Jioni katika Mgahawa wa SOTTO, ikiwa ni baada ya Serena  kutwaa Taji la WTA.

MUSIC: J FLANI FEAT. JUNNY KADO-UZURI WAKO

2:00:00 AM Add Comment

BAADA ya Kufanya Poa na Mkwaju Wa FREEDOM ambao alimshirikisha HONEYA na NATTY E (Mwanza Tanzania), Hatimaye rapper J Flani Kutoka Nchini Canada, amerejea kwa mara Nyingine Tena

Mzigo ambao amekuja nao safari Hii, ni “Mchezeko” Mkali mahali popote Ulipo, na Unakwenda kwa Jina la UZURI WAKO.

Katika Noma Hilo, J Flani amemshirikisha JUNNY KADO. Isikilize na Kudownload.

FAHAMU MTU AMBAYE, ETI ANAFANANA MDOMO NA MTOTO WA DIAMOND PLATNUMZ.

7:04:00 AM Add Comment

BAADHI ya sehemu za Mwili za Mtoto wa Diamond Platnumz na Zari, zinanza kuoneshwa kwa kificho, na huku watu wakizidi kusubiri kwa hamu kumuona.

Lakini wadaku na hata wale wataalam wa Kufananisha Vitu, wameshaanza kuzungumza kuhusu nani anafanana na Mtoto huyo katika baadhi ya Viungo, kati ya Zari na Diamond.


Katika Picha Moja wapo Ya Latiffah, ambayo ilionesha Mkono, na Mdomo kwa Mbali, basi imewafanya Followers watambue kuwa, unafanana na Mdomo wa nani kati ya watu hao wawili.

Followers zaidi ya Mmoja, walicomment na kuamini kuwa, Mdomo wa Mtoto huyo, unafanana na Mdomo wa mama Yake, yaani  ZARI THE BOS LADY

Followers hao walicomment Hivi:

maggiepetersangkaThe baby totally Zari. U got strong bood
mamamudy11kabisaaa

sheria_mwana_va_sembilinyiJamani mtoto bado mchanga rangi ake bado haijajulikana ila mdomo km wa zari(afadhali)

noszraVyote vya zari...ila mbegu ya dimond

miss_lourine@judieyni10094 lips za mama si baba. Bette


KWA Upande wako, unasemaje kuhusu Hili?

WIZI WACHANGIA KUANGUKA UCHUMI WA TAIFA

6:39:00 AM Add Comment

Imeelezwa kuwa moja ya mambo yanayochangia kuanguka kwa uchumi wa Taifa ni tabia ya wizi wa fedha za umma unaofanywa na watumishi wa Serikali kupitia njia ya manunuzi.

Hali hiyo imebainishwa juzi na Askofu wa Kanisa la Africa Inland Church Tanzania (AICT) Dayosisi ya Shinyanga, Askofu John Nkola katika ibada ya sherehe za kumpongeza Mchungaji Amos Ndaki kwa kutimiza miaka 21 ya utumishi wake ndani ya kanisa hilo.

Askofu Nkola amesema kuporomoka kwa uchumi wa Taifa mara nyingi kunachangiwa na watumishi wasio waaminifu ndani ya Serikali ambao huiba fedha za Serikali kwa kutumia njia ya kudanganya kwenye manunuzi mbalimbali ya umma, hivyo kuisababishia hasara Serikali.

Akifafanua amesema vitendo hivyo vimekuwa vikifanywa na watumishi wasiokuwa na hofu ya Mwenyezi Mungu ndani ya mioyo yao, hivyo kwao dhambi ya kuiba huona ni jambo la kawaida bila kuelewa wizi wanaoufanya una athari kubwa kwa walipakodi na wananchi kwa ujumla.

MNYAA APIGWA CHINI ZANZIBAR

6:33:00 AM Add Comment

Chama cha Wananchi (CUF) kimetangaza wagombea wa nafasi ya ubunge na uwakilishi kwa majimbo 54 ya uchaguzi kwa nafasi na uwakilishi na majimbo 50 kwa nafasi ya ubunge huku kikimtema kigogo wake, Muhammed Habibu Mnyaa (pichani), baada ya jimbo lake la Mkanyageni kufutwa na Tume ya Uchaguzi (Zec).

 Mkurugenzi wa uchaguzi wa chama hicho, Omar Ali Shehe, alisema baada ya Zec kufanya mabadiliko ya mgawanyo wa majimbo na kuongeza majimbo manne mapya, chama hicho kililazimika kufanya mabadiliko ya wagombea wa majimbo.

 Alisema baadhi ya wagombea waliogombea majimbo ya zamani na sasa yamebadilishwa majina wamewapa majimbo hayo yaliobadilishwa majina na kuwaongeza wagombea wanne kwa majimbo mapya kwa nafasi za uwakilishi.

 Mnyaa alikataliwa na wananchi katika kura za maoni, lakini baadaye Baraza Kuu la Uongozi likapitisha jina lake kugombea nafasi hiyo, hatua iliyoibua malalamiko kutoka kwa wanachama wa CUF kwa madai ya kuwa hakuwa chaguo lao.

 Baraza Kuu la CUF lilirejesha jina la Mnyaa kabla ya Zec kutoa ripoti ya mapitio na mgawanyo wa majimbo na baada ya kumaliza kazi hiyo tume ililifuta jimbo la Mkanyageni alilokuwa akiliongoza.

 Shehe alisema jana kuwa utaratibu uliotumika katika kuwapata wagombea wa majimbo mapya wamefuata katiba ya chama ambayo inaruhusu kufanya mabadiliko katika hali ya dharura.

 Aidha, CUF imemrejesha Naibu Naziri wa Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati, Haji Makame Mwadini ambaye alibwagwa katika kura za maoni kutetea nafasi yake  ya uwakilishi kwa jimbo la Nungwi na jina lake halikurejeshwa na Baraza Kuu la chama hicho, lakini sasa amepewa kugombea jimbo la Kijini.

 Waliobadilishwa majimbo baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) kutaja majina mapya kwa baadhi ya majimbo ni Mji Mkongwe, Ismail Jussa Ladhu (sasa Malindi) wakati ni Ali Saleh aliyekuwa anagombea ubunge Mji Mkongwe (sasa Malindi).

Wengine ni mwakilishi wa jimbo la Mtoni, Nassor Ahmed Mazrui amepelekwa  jimbo la Mtopepo, Mansour Yussuf Himid uwakilishi jimbo la Chukwani badala ya Kiembe Samaki na Abdillahi Jihadi Hassan uwakilishi jimbo la Mwanakwerekwe badala ya Magogoni


SIKU MOJA YA KUZALIWA, SIKU MOJA YA UMAARUFU, SIKU MOJA YA KUINGIZA DEAL LA MILIONI 50. NI MTOTO WA DIAMOND PLATNUMZ, LATIFFAH

6:54:00 AM Add Comment

blacktouchez.com
LATIFFA, Ndiye Mtoto wa Chibu Dangote-Diamond Platnumz na Zari, ambaye amepata Umaarufu ghafla, huku akiingiza Mkwanja baada ya kuzaliwa Tu.

PRINCESS TIFFA, amepata Deal kali, kama ambavyo Diamond Platnumz ameandika:


“Napenda kumtangulizia Allah shukrani zangu nyingi kwa Barka na Mapenzi mengi anayozidi kuyapata Binti yangu@princess_tiffah toka kwenu wapendwa wangu... Napenda kuwajulisha kuwa@princess_tiffah amebahatika kupata 50Million Endorsement toka#BABYSHOP ya @Msasani_city_mall &@pugu_mall Mkataba ama makubaliano hayo ni ya kuwa Balozi wa #BABYSHOPiliyopo @Msasani_city_mall &@pugu_mall
kwa Muda wa mwaka mmoja....Ubora wa bidhaa zilizopo katika #BABYSHOP ya Mall hizo ndio sabau kubwa ya mimi na mama ake @zarithebosslady kukubali Binti yetu kuwa Hilo ndio duka Pekee litalomvalisha na kumpatia Nyenzo zote za watoto... Ningependa ifahamike kuwa Chochote utachomuonanacho@Princess_tiffah kimetoka duka lililo kwenye Mall hizo...Napenda kutoa shukrani za dhati kabisa katika uongozi Mzima wa @Msasani_city_mall &@pugu_mall kwa kuwa Mfano Bora
#ProudDad”

BABA LEVO AMEPASUA..SASA KUGOMBEA UDIWANI HUKO KIGOMA KUPITIA ACT.

6:32:00 AM Add Comment

blacktouchez.com
MSANII mwenye Vituko Kuliko Balaa, BABA LEVO, hatimaye amefanikiwa kupasua katika Nafasi ya Ugombea wa Nafasi ya Udiwani kupitia Chama kipya cha ACT.

Akifyatuka kwa Furaha , baba Levo alithibitisha hilo kupitia Instagram account Yake, na hivi sasa anasubiri kuchuana na Vyama Pinzani ili kuhakikisha anachukua nafasi ya Udiwani katika kata Husika.

Aliandika Hivi.

ASANTE SANA MUNGU WANGU KWANI HAIKUWA RAISI LAKINI UMENIWEZESHA MUNGU WANGU... NESHINDA KWENYE KURA ZA MAONI NA MIMI NDIYE NITAKAYE PEPERUSHA BENDERA YA ACT WAZALENDO KATA YA MWANGA KASKAZINI KATIKA NGAZI YA UDIWANI..
.. ASANTE by BABA LEVO

HAPPY BIRTHDAY NIKKI WA PILI. HIZI NDIZO SABABU ZILIZOMFANYA AMUITE RAIS KIKWETE NI SHUJAA

6:30:00 AM Add Comment

Blacktouchez.com
SIKU Ya Jana, wasanii na wadau Mbali mbali Nchini Tanzania, walipata nafasi ya kujumuika na Rais anayemaliza Muda wake Nchini Tanzania, JAKAYA MRISHO KIKWETE, Ikulu.

NIKI WA PILI ni Moja kati ya wasanii ambao walihudhuria, huku akitoa Speech Nzuri na yenye Nguvu.

Lakini Sababu ambazo zimemfanya Niki, ameziorodhesha katika account yake kama Ifuatavyo

Tunamnukuu

Hizi ni sababu kwa nini leo najumuika na wasanii kukuaga
1.2005...uliwapandisha wasanii katika jukwaa la kampeni yako ingawa chama kili pinga sana..kusema hawa ni watu wa hovyo

2.ulilipia utafiti mkubwa wa world intellectual property rights organisation....kufanyika tanzania kujuwa mchango wa sanaa kiuchumi

3.utafiti huu ndio ulitowa ushahidi wa sanaa,miliki bunifu kutambulika katika katiba inayopendekezwa

4.kuhidhinisha mitambo ya ku monitor nyimbo zinapopigwa tv na redio..ili wasanii walipwe....na mchakato uko ukingoni

5.kushinikiza malipo ya rbt kutoka 7% mpaka sasa kufika 30%

6.mfumo wa kulinda movie wa stika za TRA..ingawa bado unachangamoto nyingi.na sasa umeamrisha TRA..kuwajibika
7.kushiriki mambo ya kijamii ya Cassini
Wewe ni shujaa wa tasnia hii

PICHA: PEMBE LA NG’OMBE…HALIFICHIKI. SIZE 8 AKIWA NA MIMBA KUBWA TU…

2:40:00 AM Add Comment

BLACK TOUCHEZ
KUNA kipindi ilikuwa kama Siri hasa pale Muimbaji wa Nyimbo za Injili Nchini Kenya, SIZE 8, alipokuwa akiulizwa kama tayari ameshapata Ujauzito wa Mumewe DJ MOE.

Lakini Kupitia account yake ya Instagram huyo, hakuna kilichofichika katika Picha zake za Birthday Yake.

Akiwa amevalia Gauni aina ya DELA, Kitumbo kilionekana Kuchomoza Mbele ya Mkali huyo wa “Mateke”, na kudhihirisha kabisa kuwa tayari Ndoa Imetia Vema…


TUNATARAJIA MAZURI kutoka kwa Size 8 na DJ MOE

MNADA BANNER