REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

DULLY SYKES HATAKI U-TEAM KATIKA INSTAGRAM

2:54:00 AM Add Comment

Mtandao wa Instagram ni mtandao wa kijamii ambao umetokea kuwa na mashabiki wengi sana Tanzania hivyo wengi wanaamkia huko asubuhi mchana na mpaka usiku na kumekua na team zinatengenezwa kwa wale wenye mapenzi na watu flani.

Dully Sykes ametangaza rasmi hataki kutengenezewa team ya aina yoyote, anakubali mashabiki wenye upendo nae ila hataki mtu atengeneze team manake zinamtengenezea uadui na watu wengine pale team inapotumika vibaya.

TUNAMNUKUU
"Sitaki kuwa huko sababu nitatengeneza maadui, hawa wanaonisuppot kila siku nitabaki nao tu ila kama wataongezeka waongezeka kwa nguvu za Mungu na sio ushabiki wa kitimu."
"Timu za Instagram zimeharibu hali ya hewa sasa hivi, zamani sisi kulikua kuna makundi yanashindana kwenye bongofleva lakini sio kushindana kwa ugomvi, ni kazi inapigwa alafu baadae tunatembeleana, na kulikua kuna Camp ikiwemo Misifas Camp ya kwangu, pamoja na kushindana kote lakini tulikua tunakaa tunakula na kunywa pamoja”

Dully Sykes ni miongoni mwa mastaa wa Tanzania ambao kwenye page zao za Instagram hawamfollow mtu yeyote, mwingine kwenye hiyo list ni Ali Kiba ambapo wote wanasababu zao kwanini imekua hivyo.

MNADA BANNER