REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

ITENGO CHA CHIMBUA CHIMBUA: RIPOTI YA AWALI KUHUSU KIPIGO ALICHOPOKEA MR. NICE

1:06:00 AM Add Comment

KAMA utakuwa unakumbuka Vizuri kabisa, jana TTM tulikupa Kidokezo Kwamba kuna Info zisizo rasmi zimetufikia Kuwa Jombaa aliyetikisa na Style ya TAKEU Nchini Tanzania, LUCAS MKENDA “Mr. Nice”, alipokea Kifinyo Cha Hali ya Juu kutoka Kwa Jamaaa hivi.

Sasa baada ya Kukigiza Kitengo cha CHIMBUA CHIMBUA Kutoka Dawati la Nyuma ya Pazia, Finally, Ripoti ya Awali imetoka.

Baada ya Kuzama kunako Mtandao wa BAABKUBWA.COM ili kufahamu kipi ambacho kimejiri, inasemekana Kuwa Eti, Mr. Nice alikutana na Mbwadidi hilo katika maeneo ya SINZA AFRIKA SANA jijini DSM,

CHIMBUA CHIMBUA ilizidi kutonya Kuwa, Chanzo halisi cha Tukio hilo, Ni baada ya Mr. Nice Kumshobokea Demu Mmoja hii wa Jamaa aliyekuwa Meza ya Jirani, akiwa Na washikaji Wengine.

Aidha ripoti inaeleza Kuwa, Mr. Nice Huenda alikuwa ashalewa Vya kutosha, na Ndipo alipoanza Kutumia USTAA Wake kutaka Kumpokonya Huyo Mamito, jambo ambalo Mhusika, yaani PAPITO wa MAMITO huyo aliona Si Sawa, ni Bora nikafanya la Kufanyika.

Taarifa bado zinamiminika kuwa, PAPITO Huyo hakuwa Pekea yake, bali alianza kushirikiana na wenzake, Kumfinya Haswaa Mr. Nice mpaka kufikia hatua ya kukimbizwa Hospitali baada ya Kugndulika jamaa keshapoteza fahamu


Lakini Info za Uhakika kutka kunako hospital ya Mwanayamala iliyoko Daslaam, inthibitisha Kuwa Ni Kweli Mr. Nice amepokelewa hospitalini hapo na kufikishwa ICU akiwa hajitambui na aliumizwa Sana

D’BANJ HATAKI UJINGA..AMELIFUNGULIA MASTAKA MTANDAO WA UK DAILY MAIL KWA KUMVUNJIA HESHIMA.

12:21:00 AM Add Comment

“Ukinikosea Heshima Nitaitafuta Kwa Nguvu” hiki Ndicho alichokithibitisha Star wa Nigeria, D’BANJ-“THE COCO MASTER” himself.

Akizungumza kunako Moja kati ya Interview Nchini Nigeria, D’banj maesema kuwa ameamua kufikia hatua baada ya DAILY MAIL kumchafua na hata Kumharibia Sifa yake, kwa Kuandika kuwa Yeye Ni Mtu wa Totoz, yaani anapiga na kuacha.

Katika ufafanuzi wake, D’banj ameongeza kuwa hivi sasa anajadiliana na Wanasheria wake ili kuweka kila kitu sawa, na hatimaye kuweza kufuata taratibu za Kisheria na kukamilisha Mchakato mzima wa kufungua Mashitaka hayo.

Aidha Mkali huyo wa OLIVER TWIST ameongeza kuwa habari Ile haikuwa na ukweli wowote kuhusu maisha yake na hata tabia yake, kwani yeye hana Mwenendo huo, kwa kuwa anawaheshimu wanawake.

Tofauti na Hilo, D’Banj aliongeza kuwa, katika uandishi huo hasa katika hiyo Stori yake, DAILY MAIL hawakufanya hata mahojiano naye kuhusu Tabia waliyompakazia. Hivyo walimzungumzia Kokomaster Vibaya, ingawa anahisi walitaka kumzungumzia KENYA MOORE kwa kile kilichodaiwa kubiringika naye, lakini hawakumtafuta D’banj Mwenyewe ili Kuweka Usawa.


Kuhusiana na Suala la mapenzi Kwake hasa mahusiano aliyonayo hivi sasa, D’banj amedai kuwa hivi sasa ana Mpenzi anayempenda kwa Dhati, na atamuoa Siku ambayo atakuwa tayari.

SIZE 8 AVURUNDA SAFARI HII…

12:14:00 AM Add Comment

MATEKE ni Moja kati ya Mikwaju ambayo imempa Jina kali haswaa katika Muziki wa Injili baada ya Kuokoka. Tunamzungumzia SIZE 8.

Baada ya Kuachia Video yake ya YUKO NA WEWE, SIZE 8 amejikuta akiingia Kunako Mchakato mgumu ikiwa ni baada ya Video hiyo kuonekana kukosa Ubora tofauti na Video zake zaAwali kama Vile MATEKE na MOTO

Baada Ya Kunyaka Info Hizo, Kitengo Cha Chimbua Chimbua kilizama kunako Mtandao wa YOUTUBE na kukuta Video hiyo ambayo iliwekwa rasmi mnamo MARCH 14, 2014, ikiwa tayari ishatizamawa na watu zaidi ya 31,000.

Tofauti na hilo, Kitengo hiki kimeshusha Ripoti yake kuwa, mpaka hivi sasa, wadau Mbali mbali wa Vyombo vya habari wakiwemo watangazaji, wamedai kuwa safari hii Size 8 amekuwa Tofauti sana hasa katika utoaji wa video nzuri.

Aidha Baadhi walidai kuwa, Kawaida ya SIZE 8 huwa ni kuachia Audio Nzuri na Video kali balaa, ila safari hii, ameingia kusikostahili kwa kuwa haikuwa na Mvuto wa Kuhamasisha watu kuitazama zaidi.
Mpaka hivi sasa Size 8 hajazungumzia Ishu hiyo, lakini kiujumla wengi Wameonekana Kuikandia Haswaaa
TIZAMA VIDEO HIYO HAPA


MNADA BANNER