REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

OH MY GOD !!! : INASEMEKANA MARIAH CAREY NA DRAKE KUNA JAMBO?

2:40:00 AM Add Comment
Na Baba Juti  


#WatuWaMungu Kuna Taarifa ambazo zimekuwa zikishtua kidogo kwa Upande wa Burudani na Enda[po kama zina ukweli wowte basi, Mariah Carey atakuwa ametisha aisee.

Baada ya kukana kutokujihusisha ama kurudiana na aliyekuwa Boyfriend Wake, Bryan Tanaka, hatimaye kuna fununu ambazo zinaendelea kudai kuwa, Mariah Carey na Drake kuna Jambo la Usiri sana ambalo linaendelea Baina yao

Kwa Mujibu wa Chanzo kimoja ambacho kinaaminika kuwa katika Management ya Hitimaker huyo wa Bye Bye, Mariah amekuwa akiwasiliana kwa Siri sana na Drake, na hata mawasiliano yao sio ya Kawaida hata Kidogo

Naomba Tunukuu tafadhari:
“Mariah Carey amekuwa akiwasiliana na Drake kwa Siri kubwa sana, kaisi kwamba kama ingekuwa ni Ishu za Kikazi, lazima management yake ingefahamu kama kuna jambo. Na Kitendo cha Mariah kumtext Drake kimemshtua sana rapper huyo ambaye hivi sasa ana miaka 30.”

Ukiachilia Mbali suala la Mawasiliano, Pia chanzo hicho kimedai kuwa, Mariah Carey amekuwa akienda Mara kwa Mara kwa siri kubwa sana katika Mgahawa ambao Drake hupendelea kujipatia Chakula, na hata J- Lo aliwahi kupelekwa pale pamoja na Serena Wiliams

Tunamnukuu
“Wote wawili wameshawahi kukutana na kupata Vinywaji wiki mbili zilizopita. Na hata Marafiki ambao walikuwa karibu nao siku hiyo wanadai kuwa walikuwa wakionesha kila aina ya Dalili za Mahaba na kufanyiana vitu ambavyo sio vya kawaida”

Hata hivyo watu wengine walidai kuwa, Mariah Carey amefanya Hivyo kwa sababu maalum, ambayo ni kumuumiza Jennifer Lopez Kihisia, maana wawili hao huwa haziivi hata Kidogo.

USIOGOPE !!! KUWA WEWE KAMA WEWE, HIYO NDIYO NGUVU YAKO

2:38:00 AM Add Comment

Na Baba Juti   
#WatuWaMungu Kama kuna kitu ambacho unadhani unakikimbia il hali ni asili yako, basi unakosea sana na inabidi ujitahidi kukiweka wazi ili kila mtu ajue na hata akuzoee kama ambavyo ulivyo


Hii imewekwa wazi na moja kati ya Warembo ambao walijipatia Umaarufu na Ujiko wa Vitu kadhaa kutoka Nchini Marekani, kupitia Instagram, kwa kuwa na Ngozi laini sanjari na “Shepu” Nzuri, lakini kumbe Ndani yake kuna Jambo

MORGIE, binti mwenye Followers Wengi Instagram, aliamua kuweka wazi kile ambacho watu wengi hasa wanawake wengi wamekuwa wakikikosa na hata kuamua kukificha ili hali kinawatesa Sana…VINYWELEO na NDEVU

Morgie anadai kuwa, Hapo awali amekuwa akinyoa sana Vinyweleo vyake katika Miguu yake, Mapaja, Mikononi, Tumboni na hata Kifuani ili kuificha Kasoro yake, kitu ambacho wengi hawakukijua na kutamani japo kutaka kujua Ulaini wa Ngozi yake unatoa Wapi

Lakini Baada ya MORGIE sasa kutupa Nyembe za Kunyolea na kuamua kujiachia kama alivyo kawaida, wengi walimshangaa na hata kumchukia huku wakimtukana matusi makali
Hatua Hiyo ilimfanya Mrembo huyo kuhama Eneo alilokuwa akiishi na kuhamia LA ambako mpaka hivi sasa amekuwa akiishi maisha Mazuri tu

Pia anaongeza kuwa, amekuwa akivaa Nguo Fupi, ambazo zinaonesha semu kadha wa kadha za Maungo yake yenye Vinyweleo Vingi, na hata akipita sehemu, hakuna ambaye anamzungumzia Vibaya wala kumtolea Hukumu, yaani wanamchukulia kawaida sana

ROZAY: BADO HAJAMUACHA BIRDMAN

2:34:00 AM Add Comment



Na Baba Juti    
#WatuWaMungu hakuna kitakachokwenda sawa kwa hivi sasa baina ya Rick Ross na Birdman hasa ikiwa ni baada ya kuzidi kufanya kila afanyalo ili kuudhihirishia Umma kuwa amemchoka kwa kwel
i

Kama utakuwa unakumbuka Vizuri zaidi, Rozay kipindi cha nyuma kidogo wakati akituambia kuwa anaachia Albu yake 9 “RATHER YOU THAN ME”, alisema kwamba ataachia Track ambayo inaitwa IDOLS BECOME RIVALS

Katika kufafanua zaidi, aliweka wazi kuwa ile itakuwa ni BARUA ya Wazi kwa Mtu ambaye anastahili kupata Ujumbe huo, na kweli amefanya Hivyo
Katika Track yake Hiyo ya IDOLS BECOME RIVALS, Rozay amezungumzia vitu Vingi kuhusu Birdman na kuweka wazi kuwa ni moja kati ya watu ambao hawastahili kupewa Heshima

Tofauti na Hilo, RICK ROSS ameongeza kuwa, Cash Money ilikuwa ni Moja kati ya Record Label ambayo ilikuwa kama Njia Nzuri kwa wasanii kadha wa kadha, lakini baadaye imebadilika na kuwa njia ya kuwanyonya watu wengi

Katika Track hiyo, Rick Ross amewataja watu kama akina DJ Khaled na Lil Wayne kama miongoni mwa waathirika wakubwa sana, lakini tizama hivi sasa, kila mtu ana maisha tofauti

MNADA BANNER