REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

I LOVE MY DAUGHTER: CHEKI PICHA ZA OCTOPIZZO AKIMPIKIA MWANAYE CHAKULA< SIKU YA BIRTHDAY YAKE

2:42:00 AM Add Comment


BAADA YA KUITWA SHOGA NA 50 CENTS, RICK ROSS ANA HILI LA KUSEMA…

2:26:00 AM Add Comment

Siku ya Jana TTM tulikupa Mtonyo kuwa Rappa 50 Cents ametoa Diss kwa watu tatu ambao ni MMG BAWSE RICK ROSS, THE BAD BOY BAWSE- P.DIDDY pamoja na Mdau wa Mziki Nchini marekani, STEVE STOUTE, huku akiwaita kuwa ni mashoga…

Lakini baada ya Kuona Tukio hilo, TTM hatukuweza kulaza damu mpaka tufahamu jibu la Watatu kati ya hoa ambao walionekana kuvunjiwa Heshima katika account ya 50 CENTS ya Instagram, lakini baadaye ikafutwa.

Lakini kama Vile tulifahamu, Finaly RickRross ndo amekuwa Mtu wa kwanza kuzungumzia Suala hilo ambalo ambalo wengi walikuwa wanasubiri majibu yake.

Katika Jibu rahisi na la kueleweka ambalo Rick Ross alilitoa, ni kwamba hana Mpango na kujibu chochote wala kujibizana na 50 CENTS, kwa sababu hamtilii maanani, wala hasumbuliwi na chochote atakachokizungumza.


Sasa kutokana na Jibu Hilo la Rozay, TTM tunajiuliza, inawezekana anampuuza 50 Cents?

UNAJUA HILI KUHUSU DAVIDO NA SUALA LA ELIMU..

2:25:00 AM Add Comment

TUMEKUWA Tukisikia wasanii mbalimbali wakizungumzia masuala yao mbali mbali ikiwemo kuboresha na kuibua Vipaji vya wasanii wengine ambao pengine wanachipukia.

Thanx God hata kwa Upande wa Tanzania, Diamnod Platnumz  laifanya kitu ambacho ni kizuri, kuwasomesha watoto kadhaa ambao waliibuka washindi katika Shindano lake la NGORORO DANCE kwa watoto wadogo, Siku ya CHRISTMAS ya mwaka jana.


Sasa Basi, back to Nigeria, DAVIDO ameonekana kuzingatia pia saula la Elimu especially kwa Vijana wenye umri mdogo.

Katika moja ya Mishe zake zilizompeleka Nchini Uingereza Maarufu kama UK, DAVIDO ambaye hivi sasa anakimbiza na kwaju la AYE, amezungumza na watoto wadogo ambao wako Mashuleni, huku akiwasihi kuzingatia Suala Zima la Elimu kwa sababu ndio njia Mbadala na muhimu katika maisha yao.



Davido aliyasema hayo wakati akitembelea shule moja huko Tottenham, ambako pia alipata nafasi pia ya kutambulisha shindano kwa watoto hao ambalo linaitwa CAN YOU DANCE SKELEWU, na Mshindi ataondoka na kitita cha POUND 2000.

CHRIS BROWN HANA UBAYA NA RIHANNA PAMOJA NA DRAKE

2:22:00 AM Add Comment

CHRIS BROWN hana ubaya na wala hana mpango wa Kulianzisha Timbwili baina yake na DRAKE kutokana kuwa karibu na RIHANNA

Kwa Mujibu wa Mtandao wa TMZ, TTM tumebaini kuwa, Breezy hata haumizi kichwa kwa ajili ya Ukaribu wa Rihanna na Drake, licha ya kutokuelewana Vizuri (Brown na Drake), kwa sababu hivi sasa akili yake ipo katika kusaka Mkwanja, pamoja na kuandaa ujio wake katika Music Industry


Kama utakuwa unakumbuka Vizuri, Ishu ya Drake kuwa karibu na Rihanna ilionekana muda mrefu kidogo, lakini ukaribu wa Nchini Ufaransa katika Jiji la Paris, uliwafanya wawili hao kutengeneza HEADLINES Kubwa Ulimwenguni Kote

WAHUU: NAMELESS NDIYE BABA MZAZI HALALI WA MTOTO WETU NYAKIO.

2:18:00 AM Add Comment

KIUKWELI Hata Mie Nilishtuka kuona info hii kutoka Nchini Kenya, but Honestly ninajivunia Kile ambacho WAHUU amekizungumza katika Moja ya Interview Nchini Humo.

Wahuu ambaye alishika sana akili za Mutu Nyingi kupitia kwaju la SWEETLOVE, alifunguka na kujibu swali ambalo aliulizwa kuhusu Mzazi halali wa Mtoto wao Mpya wa kike, NYAKIO.

Katika maelezo yake, WAHUU amesema kuwa, NAMELESS Ndiye baba wa Mtoto na atabaki kuwa baba wa Mtoto wao huyo.

Pia Wahuu aliongeza kuwa, ni kweli kuna muda ilitokea mikwaruzano katika Ndoa, kama ambavyo hali inavyoweza kutokea kwa wanandoa wengine, lakini yale ni matatizo madogo tu ya kutokuelewana, na hata siku moja hawakuwahi kufikiria suala zima la Taraka au Kuachana.



Pia Wahuu aliongeza kuwa, kuna baadhi ya Vitu ambavyo wao kama wanandoa walikuwa wakijikuta hawakubaliani navyo na kutofautiana, lakini hawakuwahi kumaliza Wiki au Mwezi pasipo kuongeleshana ama kusalimiana, kama ilivyo kwa Wengine ambao hudiriki hata kumaliza Mwezi hawasalimiani, licha ya kwamba wanaishi Pamoja

MNADA BANNER