REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

PICHA: MTOTO WA 2 FACE IDIBIA, ZION ATIMIZA MIAKA MITANO

9:11:00 AM Add Comment



Anaitwa ZION,Mtoto wa Tatu wa 2 Face Idibia

PICHA : LIKE MOTHER, LIKE DAUGHTER

8:50:00 AM Add Comment
SMILING: Mkongwe katika Tasnia ya Filamu Nchini Nigeria, katika "Nollywood" PATIENCE OZOKWO maarufui kama "mama Mnandi" akiwa ni Mwingi wa Tabasamu katika Ndoa ya Binti yake

HATIMAYE: CHAMELEONE AWAKUBALI HAWA...

8:15:00 AM Add Comment

Baada ya kufunika vilivyo kwa kutoa burudani ya nguvu katika tamasha kubwa ambalo limefika huko nchini Uganda hivi karibuni msanii Jose Chameleone amesema kuwa amewaomba mashabiki na wadau kuwapa sapoti wasanii wa Goodlyfe, Moses Radio na Weasel TV.

Chameleone ambaye ni ndugu na Weasel TV alitumia nafasi hiyo ya kuwaomba mashabiki katika tamasha hilo kutokana na kwamba wasanii hao wamekuwa ni wenye mafanikio makubwa na kwamba katika wiki mbili zijazo wanatarajia kufanya uzinduzi wa albamu yao waliyoibatiza jina ‘Obudde’.

Aidha Jose Chameleone alionyesha kuwa yeye ni gwiji na mwenye kipaji katika tamasha lake la ‘Badilisha’ haswa alipoweza kuimba zaidi ya nyimbo 40 ambapo pia aliziimba nyimbo za wasanii mbalimbali Afrika Mashariki kama wimbo wa Kigeugeu wa Jaguar, Mukama wa Judith Babirye, Bread and Butter kutoka kwao Moses Radio na Weasel TV, Kasepiki wa Bebe Cool na Wendi wa Bobi Wine.

WASHAMBA:KWA WALE WOTE AMBAO HATUKUIONA, HUYU SI JUSTIN BIEBER NA SERENA GOMEZ?. INAMAANISHA WAMERUDIANA?

7:58:00 AM Add Comment

UKATILI : HAMMER Q, UNYAMA HUU ULIOUFANYA KWA MKEO, NI UJINGA NA UBWEGE ULIO NAO. NAHISI WEWE NI MTOTO NA UNA AKILI ZA KITOTO

6:55:00 AM Add Comment
 Suruari ya Hammer Q ikiwa imetapakaa Damu

HAMMER Q.
Binafsi pia ni Mtanzania, na Ninaye mama Mzazi mwenye jinsia kama hiyo ya Mkeo Mpendwa Salha. Pengine hata Mama yako Mzazi ni Jinsia hiyo hiyo ya Salha. Au Unabisha?

Haki ya Mungu, amini usiamini, unabahati kubnwa sana, maana Tanzania hatujachukulia Kivile suala la "DOMESTIC VIOLENCE", lakini kama ingekuwa hivyo, binafsi ningemuona MPUMBAVU sana yule ambaye angekuja kukutolea dhamana kwa Ujinga na Unyama huu ulioufanya kwa Mkeo Salha.

Kama ulikuwa hauna akili juu ya hili,adhabu uliyoitoa kwa Mkeo ni zaidi ya Ukatili ambao hata mama yako angefanyiwa,ungemuona katili aliyemfanyia hivyo. Kama ni masualaya Makosa ndani ya Ndoa zenu au Mahusiano yenu, kuna njia mbadala za kuyatatua, l;akini sio Ufala huu ulioufanya.

wewe sio Muislam kabisaaaaa...ila inabidi ujione kama Kafir, hasa kwa Tukio hili uliolifanya.

Nakuona Bwege sana,na tena Mpumbavu usiye na Akili kufanya hivi. Kama utakuwa umechukia,Bora iwe hivyo ili ujue kuwa unaidajhririsha Jinsia ya Mama Zetu wazazi.

PHOTO : HASTA LA VISTA BABY ALONG SIDE NATTY E BRANDY !!! THE ROK CITTERZ

2:23:00 AM Add Comment
& Natty E Brandy tukiwa kwa Big Pouz ndani ya Cook Out Chember la Mtu Mzima "Big Dady " Oxy.
(Picha na Na George "G.B. Pazzle" )

EXCLUSIVE: HATUTAKI ZAWADI ZA MTOTO

2:04:00 AM Add Comment
WAKATI KIBONGOBONGO tukililia zawadi pindi tunapopata watoto katika Famili zetu, Hahahaaa, Kim na Kanye wamesema "HAWATAKI ZAWADI ZA MTOTO " toka kwa Rafiki au Shabiki yeyote yule

Kwa Mujibu wa Mtandao wa Udaku wa TMZ, imekaririwa kwamba Mwanadada Kim Kardashian amesema kuwa, badala yake, zawadi ambazo walitakiwa kupewa toka kwa Mafanz wao, jamaa na hata Ndugu, basi zipelekwe katika hospitali ya LURIE CHILDREN'S HOSPITAL iliyoko ChicagoMrekani,ambako Mtu Mzima KANYE WEST alikulia



BREAKING NEWZ: MSIGWA ANAUWASHA MOTO SASA HIVI BUNGENI

1:54:00 AM Add Comment

Na Frank M.Joachim
MBUNGE wa Iringa Mjini kwa Ticketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA, Mchungaji Peter Msigwa, hivi sasa yuko anauwasha moto akiwakilisha maoni ya Kambi ya Upinzani Bungeni katika Bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii, kwa mwaka 2013/ 2014.

Katibu wa CCM, Abdallah Kinana na Mkewe wametajwa kuhusika na Udanganyifu katika Baadhi ya Hisa katika Idara ya Maliasili na Utalii, huku Makada Wengi wa CCM wakitajwa haswa katika ugawaji wa Vitalu kwa Kampuni mbali mbali.

BLACK TOUCHEZ ITAZIDI KUKUJUZA KWA KILA KITU

BIASHARA : SONGEA ITAKUMBWA NA HILI

1:32:00 AM Add Comment


Na Julius Konala
HALMASHAURI ya Wilaya ya Songea, mkoani Ruvuma ipo hatarini kukumbwa na baa la njaa kutokana na baadhi ya wakulima kuanza kuvuna mahindi mabichi yakiwa shambani na kuyauza.

Aidha tulipita maeneo mbalimbali ya masoko ya uuzaji wa mazao ya mahindi likiwamo soko kubwa la Sodeco lililopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani humo na kushuhudia hali hiyo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana, baadhi ya wafanyabiashara walisema hali hiyo inatokana na serikali ya mkoa kushindwa kutoa vibali vya kununulia mahindi ya mwaka jana katika ghala la hifadhi ya chakula la taifa.

Kwa upande wake mmoja wa wafanyabiashara ambaye pia ni Mkurugenzi wa kampuni ya kukoboa na kusaga nafaka ya Mtanzamo, Julius Mlawa, alisema lengo la serikali ya Mkoa wa Ruvuma kutaka kutoa vibali vya kununua mahindi kwenye ghala la chakula la taifa kwa kipindi kile lilikuwa zuri, lakini kwa sasa mpango huo hautafanikiwa kutokana na serikali kutaka bei ya sh 450 kwa kilo moja wakati sasa wakulima wanauza sh 300 kwa kilo.

Alisema kwa ujumla wafanyabiashara mara zote wamekuwa wakisukumwa na soko lililopo, kwani wakulima walishaanza kuuza mahindi mapya tofauti na kipindi cha nyuma ambacho Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Said Mwambungu, alipoahidi kutoa vibali vya kununua mahindi kutoka hifadhi ya chakula ya taifa ambapo mahindi mapya yalikuwa bado hayajaanza kuvunwa.

Mkuu wa Wilaya ya Songea, Joseph Mkirikiti, amepiga marufuku kwa wafanyabiashara wanaojihusisha na ununuzi wa mahindi mabichi kutoka kwa wakulima na kusema kufanya hivyo ni kuwanyonya wakulima na kukaribisha janga la njaa na kuongeza kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa mfanyabiashara yeyote atakayebainika kufanya hivyo.

MAJANGA: MOROGORO MAFURIKO TENA

1:17:00 AM Add Comment


NAVicky Kombe, Morogoro
NYUMBA 25 na mashamba ya mazao ya chakula yanayokadiriwa kufikia ekari 2908 katika kata ya Bwakira chini wilaya ya Morogoro, yamesombwa na maji baada ya mvua kubwa kunyesha na kusababisha mafuriko.

Tukio hilo lililtokea Aprili 6 mwaka huo na kuvihusisha vijiji vinne vya Bonye, Mbwade, Bwakira chini na Dakawa na hivyo kuwaacha wakazi wake katika wakati mgumu.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa, Diwani wa kata hiyo, Pessa Mohamed, alisema kuwa mafuriko hayo mbali ya kuharibu makazi na mashamba ya mazao ya chakula, pia yameziacha familia 1598 zikiwa hazina mahala pa kuishi.

Kwa mujibu wa diwani huyo, mazao yaliyoharibiwa na ekari kwenye mabano kuwa ni mahindi (1158), mpunga (1143), ufuta (274), nyanya (3), ufuta (27), alizeti (3) miwa (2) na nyanya (1).

Hata hivyo, alisema kuwa juhudi zinafanywa kuhakikisha wakulima wanapata mbegu kwa kushirikiana na kitengo cha maafa katika wilaya hiyo.

Alisema kutokana na mafuriko hayo, kata hiyo sasa inaweza kukumbwa na njaa na hivyo ameiomba serikali na wadau mbalimbali kujitokeza kusaidia mbegu za mahindi za muda mfupi kwa ajili ya kunusuru njaa katika kata hiyo.

“Tunaomba wadau mbalimbali watusaidie mbegu za mahindi ya muda mfupi kwanza kuliko kuleta chakula, hicho kitafuata baadaye,’’ alisema.

MNADA BANNER