REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

MCHUMBA WA BOSS ANADAIWA PESA HII...NAYE NI TONI BRAXTON

2:38:00 AM Add Comment
 
Na Baba Juti   
HIVI, Kwa Wewe Binti ambaye ni Mrembo, unatokea kupendwa na Mwanaume ambaye ana mihela kibwena, halafu anakuchumbia na kuonesha hadharani kuwa kwako amekufa ameoza, utafurahia au hautofurahia kuwa naye?

Kama kama hautofurahia mahusiano hayo, basi inabidi ujifunze maana linaweza tokea la kutokea kama ambavyo limetokea kwa Toni Braxton ambaye ni Mchumba wa Birdman ambaye ni boss wa CASH MONEY RECORDS LABEL

Kama utakuwa hujafahamu, Mamlaka ya Kodi Nchini Marekani, imetangaza Rasmi kuwa inamdai Toni Braxton Mkwanja wa Kodi ambao alikwepa kuulipa, ambao ni USD 780,808.29 sawa na Tsh 178,024,290.12 kuanzia mwaka 2015 mpaka hivi sasa

Kwa Mujibu wa Taarifa kamili kutoka katika Kitengo husika, Toni anadaiwa Kodi hiyo kutoka maeneo mawili na yo ni 
State of Californa
2015: $113,500.93
2016: $116,870.07
Federal
2015: $310,223.28
2016: $240,214.01
Sasa, hatujafahamu atalipa vipi mkwanja huo, wacha tusubiri

MNADA BANNER