REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

UTAMU WA KUCHIMBA DAWA !!!! : DESIGNEER "ANASWA" AKIKOJOA MBELE YA GARAGE BINAFSI YA MTU

1:55:00 AM Add Comment

Na Rich Sam   
#WatuWaMungu kila mmoja aseme Paaanda !! Paanda!! Paaanda !!! Paanda !!! Paaaandaaaaaa !!!, bonge la mzigo ambalo liliusumbua sana ulimwengu, wala tusiongee sana tukamaliza utamu

Wengi tumemmis Desiigner, uwongo?, maana zile kelele zake, fujo zake, mbwembwe zake, amsha zake, vituko vyake, ongea yake, huwa ni unique yaani hakuna msanii mwingine ambaye anafnaya akama anavyofanya Desiigner !!


Ila sasa, kuna hii ambayo binafsi tumeipenda na tukaona ni bora tukaiongeze katika moja kati ya vituko vyake, ingawa hatujui dhamira yake

Bwana Desiigner alibambwa na wakuda wa mambo akikojoa ama kutoa haja ndogo katika Private Garage ya Mtu aisee, kweupee bila hata kuogopa

Ingawa haikufahamika kama bwana Desiigner alikuwa amebanwa sana mpaka ikamlazimu kusimamisha gari lake aina ya Lamborghin na kujibanza sehemu achimbe dawa, ama ilikuwa ni makusudi, ila wengi wamestaajabishwa sana na tukio hilo

BACK AGAIN ?: TUTARAJIE TAARIFA "TAMU" KUTOKA KWA JANET JACKSON NA JERMAINE DUPRI

1:11:00 AM Add Comment

Na Rich Sam   
#WatuWaMungu inawezekana kabisa kukawa na jambo kubwa ambalo tunatakiwa kulitarajia kutoka kwa ma-ex wawili ambao walikuwa na mahaba ya dhati kipindi chao cha "mahusiano"

Kwa mujibu wa Taarifa kutoka kwa chanzo muhimu kabisa cha familia ya Janet Jackson, inasemekana ni kweli na hakika Janet na Jermain Dupri wameamua kurejesha kile ambacho kilikuwepo kipindi cha nyuma.

Kama utakuwa unafuatilia vema maisha ya wawili hawa, haikuwa mapenzi tu ndani ya maisha yao, bali pia kulikuwa na kazi ambapo Jermain Dupri alikuwa akimsimamia Janet jackson katika kazi zake na hata kumfikisha Sehemu mbili

Chanzo hicho kimeongeza kuwa, Urafiki wa wawili haop kwa hivi sasa, umekuwa ni wa karibu kuliko kawaida, hivyo muda wowote linaweza kutokea la kutokea na taarifa zikaja njema zaidi

" Jermain ni mtu muhimu sana kwa Janet, maana tangu amekuwa katika wakati mgumu, yuko naye karibu, na hicho ndicho ambacho Janet huwa anakipenda zaidi kutoka kwa Jermain. tusubiri tu, maana urafiki wao ni zaidi ya urafiki wa kawaida kabisa"

MNADA BANNER