REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

KIFO CHA GOLDIE:PREZZO ALITAKIWA AKUTANE LEO NA GOLDIE

2:19:00 AM Add Comment

Prezzo akiwa na Mpenzi wake Marehem Goldie Halvey, wakati wako pamoja BBA

HAKIKA NI MSHTUKO KWA KILA MDAU WA WAWILI HAWA.
Kwa mujibu wa taarifa kamili ni kwamba, Jackson "Prezzo" Makini alitakiwa akutane na Marehemu Goldie Halvey kwa ajili ya kumalizia siku ya Valentine Day pamoja.

Hayo yalisemwa na Mkali huyo Jumanne iliyopita, katika kipindi cha Churchill Nchini humo (Kenya), ambapo alithibitisha kuwa alikuwa na ratiba ya kwenda kuonana na Mpenzi wake huyo
Aidhaa kwa taarifa rasmi ni kwamba, Prezzo jana aliondoka Kenya kuelekea Nigeria
MAREHEMU Goldie Harvey

Goldie alifariki muda Mchache baada ya kuwasili kutoka Nchini Marekani ambako alihudhuria Tuzo za Grammy, huku kifo chake kikiacha Mshtuko Mkubwa barani Afrika.
Jitihada za kuupigania uhai wake zilishindikana katika Hospitali yake maalum ya Reddington, Victoria Islands, katika Jiji la Lagos, ambapo Madaktari waliokuwa wakimhudumia hawakuwa na budi kutangaza kifo cha Goldie.

NA FRANK M JOACHIM


MNADA BANNER