REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

UKIMWAGA MBONGA.......: BAADA YA JUSTIN BIEBER KURUDIANA NA SERENA GOMEZ, HATIMAYE THE WEEKEND AMCHUKUA EX MWINGINE WA JUSTIN BIEBER

1:40:00 AM Add Comment

Na Rich Sam   
Watu Wa Mungu Msanii The Weekend ameamua kuuthibitisha Ule Usemi wa "Ukimwaga Mboga, Namwaga Ugali", na hali halisi iko Hivyo tena hadharani sasa Hivi

Kama utakuwa una kumbu kumbu swadakta kabiosa, Baada ya Justin Bieber kuachana na Srerena Gomez kipindi cha Nyuma, The Weekend aliamua kuchukua nafasi hiyo na mahaba yakawa Mahaba Kweli kiasi kwamba wengi tukaamini mabo yataenda vizuri sana

lakini Mwezi uliokata, iliibuka taarifa kuwa Serena Gomez ameapigana Chini na The Weekend , kama haitoshi ni kama karudisha mahaba yake kwa aliyekuwa Mpenzi wake, JUSTIN BIEBER, na hivi sasa wako karibu sana

Sasa Bwana, Usiku wa Kuamkia Jana, The Weekend naye ameamua kujibu mapigo  kwa kuamua kujiweka kwa Ex- wa Justin Bieber anayeitwa YOVANNA VENTURA

Yovanna ambaye ni mwanamitindo kutoka Miami, alikuwa ndani ya Mahaba Mazito na Bieber kipindi ameachana na Serena Gomez , wakati huo Pia Serena alikuwa ameshaopolewa na The Weekend

Wawili hao walinaswwa pamoja usiku wa manane wakitokea kunako kiwanja kimoja kinachoitwa HYDE, ambapo Wawili hao walikuwa wamekaa Seat ya Nyuma ili wasionekane


Hata Hivyo inadaiwa kuwa, The Weekend na Ex- wa Bieber walikuwa pamoja pia katika Birthday party ya French Montanah huko Beverly Hills, NOVEMBER 9, na walikaa pamoja kwa kila u=ishara ya mahaba mpaka Usiku wa manane ambapo waliondoka pamoja pia na kuelekea kusikofahamika

KWISHA MANENOOOOO: KI-BEN-TEN CHA MARIAH CAREY NDICHO KI-MENEJA CHAKE KWA HIVI SASA !!!!

1:14:00 AM Add Comment

Na Baba Juti   
Oh My God !!!, Watu Wa Mungu sijui kama mtaitafsiri kama ni Good News ama Lah, lakini hali halisi iko Hivyo waungwana

Siku Kadhaa zilizopita, Msanii  Mkongwe wa Muziki wa R&B na POP, MARIAH CAREY, aliamua kupigana Chini na Meneja wake wa Muda Mrefu, STELLAH kutokana na namna ambavyo ukiukwaji wa makubaliano yao ilikuwa ukifanyika hasa katika Misinging ya Kazi.

Ingawa haikuwekwa wazi hasa katika Mandishi, pia haikufahamika zaidi ni nini hasa kilisababisha wawili hao kuacha kufanya kazi kwa pamoja, lakini vyanzo vya karibu vinadai kuwa, Boy Friend wake, yaani ki-Ben Ten chake Mariah Carey, Byan Tanaka ndiye chachu ya kuvunjika kwa Wawili hao

Kilichokuja kudhihirisha zaidi kuwa Ni Kweli Brian Tanaka ndiye chanzo cha kila Kitu, ni Mara Baada ya Mariah Kumtangaza Rasmi Boyfriend wake huyo kuwa ndiye Msimamizi wa kazi zake na Fani yake Kiujumla

Katika kukazia Zaidi, Ikatoka taarifa kuwa, katika makubaliano yao, Bryan Tanaka atakuwa analipwa USD 12,000 kwa Wiki sawa na Tshs. 27,420,000

Aidha mmoja kati ya Wahusika kunako Management ya Mariah Carey, aliweka wazi kuwa, Mwisho wa Mariah Carey na Brian Tanaka, ni kama Mwisho wa Kelvin Ferdeline na Britney Spears.

Tunamnukuu
"Mariah Carey ni Msanii na Brian Tanaka ni Back Up Dancer Wake. Hata kama taeandelea kumsimamia, Brian hajui lolote kuhusu Managerment ya Muziki na masuala ya Muziki na kumsimamia Msanii ambaye ana taswira kubwa kwa Dunia.... hata hivyo, Brian amekuja kuharibu kila kitu katika Muziki wa Mariah Carey na maisha yake kiujumla"

OH MY GOD !!!: FETTY WAP ANATARAJIA KUFIKISHA IDADI YA WATOTO 8

12:42:00 AM Add Comment

Na Baba Juti    
Watu Wa Mungu kuna kitu ambacho binafsi natamani kufahamu pia kutoka kwenu kwa sababu vitu hivi vinahitaji  uzoefu kidogo.

Rapper Fetty Wap inawezekana kabisa baada ya kuona kama soko la Muziki limeanza kuwa na changamoto kubwa sana kwake, sasa ni bora zaidik kuwekeza katika Watoto ama familia.

Kwa mujibu wa Taarifa ambazo tuko nazo mpaka Hivi sasa, Rapper Fetty Wap ambaye ana Umri wa Miaka 26 kwa Hivi sasa, anatarajia kupata watoto wengine wawili , wa kike na wa kiume, ambapo atakamilisha Idadi ya Watoto Nane ambapo Sita alionao hivi sasa ndio wanaotambulika

Awali Hitmaker huyo ambaye aliukunjua Ulimwengu kupitia Track yake ya TRAP QUEEN, aliingia katika Mgogoro mzito na Mzazi Mwenzake MASYKA baada ya kudaiwa kuukataa ujauzito miaka kadhaa iliyokata, lakini baadaye mambo yalienda Fresh

Ukiachilia mbali Masyka, Fetty Wap pia ana mtoto na wanawake wengine ambao ni Lezhae Zeona, Lez na Alexis, na mtoto wa kike anayesubiliwa, ni kutoka kwa mwanamitindo ALEXIS SKYY na yule wa kiume, haifahamiki ni kutoka kwa nani.

MNADA BANNER