REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

KAMA ULIKUWA UNASUBIRI MECHI YA SIMBA NA YANGA, KUNA MABADILIKO HAYA

6:42:00 AM Add Comment


Na Dina Ismail, DAR ES SALAAM
MECHI ya watani wa jadi, Simba SC na Yanga SC mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara iliyokuwa ichezwe Oktoba 12, mwaka huu imefutwa na sasa tarehe mpya itatajwa kesho.


Taarifa ya TFF leo imesema kwamba, hiyo iantokana na mchezo wa kirafiki wa kimataifa baina ya Taifa Stars na Benin ambao kwa ujumla utabadilisha ratiba ya Ligi Kuu na marekebisho hayo yatatangazwa kesho (Septemba 26 mwaka huu).

Taifa Stars inashuka uwanjani Oktoba 12 mwaka huu kuikabili Benin katika mechi ya kirafiki ya kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).


Mechi hiyo itachezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni. Programu ya Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager kwa ajili ya mechi hiyo itatangazwa baadaye na Kocha Mkuu Mart Nooij.

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) linaendelea na taratibu nyingine kwa ajili ya mechi hiyo ikiwemo usafiri wa Benin kuja nchini, ambapo timu hiyo inatarajiwa kutua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Oktoba 10 mwaka huu ikiwa na msafara wa watu 28.
Pambano la Stars na Benin litatanguliwa na mechi ya kudumisha 

upendo kati ya viongozi wa dini ya Kikristo na Kiislamu.
Wakati huo huo: Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi anatarajia kufunga mafunzo ya uongozi kwa viongozi wa vyama vya mpira wa miguu wa wanawake vya mikoa ya Tanzania Bara.

Hafla ya kufunga mafunzo hayo itafanyika kesho (Septemba 26 mwaka huu) saa 5 asubuhi kwenye ofisi za TFF, Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.

Mafunzo hayo ya siku tano yalishirikisha viongozi 34 wakiwemo baadhi ya waandishi wa habari na Meneja wa Twiga Stars, na yaliendeshwa na Mkufunzi wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Henry Tandau.

RAIS KIKWETE ANAHITAJIKA KUTOA USHAHIDI MAHAKAMANI

6:20:00 AM Add Comment

KUTOKA Arusha, TANZANIA 
Rais Jakaya Kikwete ni miongoni mwa mashahidi wanaotarajiwa kuitwa na walalamikaji katika shauri dhidi ya nchi za Kenya, Uganda na Rwanda linaloendelea katika Mahakama ya Afrika Mashariki (EACJ).

Wakili Jimmy Obeid anayewawakilisha walalamikaji katika shauri namba 9/2013, jana aliieleza Mahakama kuwa miongoni mwa mashahidi watakaoitwa kujenga kesi hiyo ni pamoja na Rais Kikwete.

Shauri hilo lilifungulliwa na Watanzania watatu, Ally Hatib Msangi, David Makatha na John Bwenda wakidai kitendo cha Kenya, Uganda na Rwanda kufanya vikao bila kuzishirikisha Tanzania na Burundi ni ukiukwaji wa mkataba wa kuanzishwa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC)

Miongoni mwa vifungu vya mkataba wa EAC vinavyodaiwa kukiukwa ni namba 3(3) (c) kinachotaka ushiriki sahihi kuimarisha ushirikiano ndani ya ukanda wa Afrika Mashariki na Kifungu cha 6 (a) (b) (d) na (f) kinachozitaka nchi wanachama kuzingatia misingi ya kuanzishwa kwa jumuiya hiyo.

Katika ushahidi wake, Rais Kikwete ataombwa kuthibitisha hotuba yake kwa Taifa aliyoitoa bungeni Novemba 7, mwaka jana ambayo ilielezea jinsi Tanzania na Burundi zilivyotengwa na baadhi ya nchi wanachama wa EAC.

“Kutokana na uzito na majukumu ya Rais Kikwete tunayepanga kumwita kama mmoja wa mashahidi wetu, naiomba Mahakama muda wa mwezi mmoja kuwasilisha orodha ya mashahidi na hati za viapo,” alisema Obeid. Jopo la majaji watano wakiongozwa na Jaji Kiongozi, Jean-Bosco Butasi, Naibu Jaji Kiongozi, Isaac Lenaola na wengine Faustin Ntezilyayo, Monica Mugenyi na Fakhi Jundu walikubali ombi hilo na kupanga Oktoba 24, mwaka huu wadai kuwasilisha hati ya kiapo na orodha ya mashahidi.

Wadaiwa katika shauri hilo ni Katibu Mkuu wa EAC, anayewakilishwa na wakili Dk Antony Kafumbe wakati mdaiwa wa pili ni Mwanasheria Mkuu wa Kenya anayewakilishwa na mawakili wawili, Muthoni Kimani na Peter Ngumi, mdaiwa wa tatu ni Mwanasheria Mkuu wa Uganda anayewakilishwa na mawakili watatu, Elisha Bafirawala, Richard Adrole na Maureen Ijang’ na mdaiwa wa nne ni Mwanasheria Mkuu wa Rwanda anayewakilishwa na wakili Malaala Aimable.

Wadaiwa hao watawasilisha majibu kabla ya Novemba 7 mwaka huu na kutoa maelezo ya ziada Novemba 14 mwaka huu kabla ya Mahakama kupanga siku ya shauri hilo kusikilizwa na pande zote zitapewa wito maalumu.

Septemba 2, mwaka huu, wadai waliondoa mahakamani ombi la zuio la muda dhidi ya vikao vya muungano wa wenye nia (coalition of the willing), baada ya Tanzania na Burundi kuanza kushirikishwa kwenye vikao viwili vilivyofanyika Februari 24 na Mei 2, mwaka huu.

LAMBORGHINI YA DHAHABU IMEONEKANA NCHINI UFARANSA..CHEKI PICHA ZAKE HAPA. INAUZWA DOLLA MILIONI 6

5:00:00 AM Add Comment





DAH: MKE WA WIZ KHALIFA, AMBER ROSE, AFUNGUA MADAI YA TALAKA…..INASEMEKANA NICK CANNON NDIYE CHANZO

2:03:00 AM Add Comment

LOS ANGELS, Marekani
BIG News nay a kushtua ni hii ambayo TTM tumekutana nayo ikizunguka kunako Mitandao Mbali mbali ya Kijamii, kuhusu Kuvunjika kwa Ndoa ya Amber Rose na Wiz Khalifa, iliyodumu kwa Muda wa Mwaka 1 na Miezi kadhaa..FULL STORY iko Hivi…

Mpaka Hivi sasa, tayari Amber Rose ameshafungua jalada la Kudai talaka kutoka kwa Mumewe Huyo CAMERON THOMAZ, maarufu kama Wiz Khalifa.

Ingawa Mpka hivi sasa Wiz Khalifa hajatoa Taarifa Maalum kuhusu chanzo cha wawili hao Kutemana, Lakini huwezi amini, tatizo kubwa linaloonekana kuwepo, Ni Usaliti baina ya wanandoa hao wawili, ambapo kila mmoja anamlaumu mwenzake kwa Kujihusisha na UCHEPUKAJI mkubwa.

Licha ya Miezi kuadhaa Amber Rose kupost Picha ya Ndoa yao, wakipongezana kwa Kutimiza Mwaka Mmoja katika Ndoa yao, lakini hivi sasa Ni KWISHA HABARI, hakuna cha Amber Rose , wala Wiz Khalifa Kuhusiana na Ndoa.

·        Ugomvi Ni Mkubwa:
Kama Ilivyokuwa kwa Nick Cannon na Mariah Carey, basi safari hii imekuwa hivyo Hivyo kwa upande wa Wiz Khalifa ambaye anafanya Vema na Albam Yake ya BLACCHOLLYWOOD iliyosheheni mangoma Makali likiwemo la WE DEM BOYS. Chanzo kilicho karibu na wawili hao, kinadai kuwa, Ugomvi ulioko baina ya wanandoa hawa wawili, ni Mkubwa na Mchungu , maana hata ukiangalia Documents za kudai talaka, ni Chungu balaa

·        Nick Cannon Kuhusika Katika Kuvunjika Kwa Ndoa Hiyo.
Hivi majuzi tu, Aliyekuwa Mume wa Mariah Carey, Nick Cannon ambaye nayeye Ndoa yake iliingia katika Noma Kubwa na Madai ya talaka Kufunguliwa, alisikika akisema kuwa, anataka kumfanya Amber Rose awe Maarufu kupitia Televisheni na Huenda akashirikiana naye hasa Kibiashara.
Kauli hiyo iliwafanya wengi wajiulize maswali, hasa ukizingatia inasemekana kuwa Eti, Amber Rose na Nick Cannon wameshawahi kushiriki katika Mkunjuko wa Kimapenzi.
Hali Hiyo ilizua Utata sana, huku wanahabari wakidhani kuwa huenda Nick cannon anazingua, lakini walipomhoji Amber, alikiri kuwa ni Kweli, atafanya kazi na Nick Cannon,

·        Nick Cannon Amejibu Hivi:
Kwa upande wake Nic Cannon ambaye kwa asilimia kubwa ni HOST katika Vipindi mbali mbali hasa AMERICA HAS GOT TALENT, amesema kuwa yeye hajahusika kwa namna yoyote ile, katika kuvunjika kwa Ndoa ya Wiz khalifa na Amber Rose
Pia Cannon ameongeza ya kwamba, Yeye na Amber Rose, walikubaliana wafanye Mishe za kibiashara tu, na hakuna ushauri wa kudai talaka uliotoka kwake hata Siku moja.

Fahamu Haya Machache:
  • ·        Kipindi cha Awali, Amber Rose amewahi kuwa STRIPPER, yaani Mcheza Utupu/Uchi wa Night Clubs
  • ·        Amewahi kukunjuka na Rapper Kanye West ingawa hawakudumu sana katika Mahusiano yao, huku ikiaminika kuwa Kanye alikuwa akigawa kifinyo kwa Amber Rose
  • ·        Amber Rose aliwahi kumzawadia WIZ KHALIFA saa yenye Thamani kubwa, aliyowahi kupewa na Kanye West wakati wapo Katika mahusiano.
  • ·        Amber Rose anataka apewe haki za malezi na Usimamizi wa Mtoto wao, SEBASTIAN THOMAZ “The Bash”, na anataka Wiz Khalifa awe anamtembelea Tu. Mtoto wao ana Umri wa Mwaka mmoja

“ADAM JUMA ANALIPWA VILE VILE,YAANI ANLIPWA KAWAIDA..ILA TUANGALIE AMETUTOA WAPI”-KAULI YA RIC MAVOKO

1:58:00 AM Add Comment

DAR ES SALAAM, Tanzania
NI KWELI Kipindi cha Nyuma Video kali kama Vile, SHE GOTTA GWAN ya Ngwea, ICE CREAM ya Noorah, CHUNGWA ya Suma-Lee na Nyinginezo kibao, tulikuwa  tunazielewa na kuzipenda sana kupitia mkono wa ADAM JUMA wa VISUAL LAB

SASA, Muimbaji na Mkali wa FOLLOW ME ambaye Soon anaaachia mzigo Mpya wa PACHA WANGU, Rich Mavoko, amewasihi wasanii wa Tanzania kukumbuka Mchango wa Adam Juma hasa pale walipo hivi sasa, na Kiasi wanachomlipa.

Akizungumza kuhusiana na Hilo, MAVOCO amesema kuwa, wasanii hawatakiwi kulalamika juu Adam Juma kuhitaji Mkwanja Mrefu kufanya Video, pasipo kukumbuka Mchango wake katika Video Industry hapa Nchini Tanzania
Hapa Tunamnukuu akisema:

 “Lakini tuangalie pia ametutoa wapi. Movement zake kuhusu music video Adam Juma ameitoa wapi. Tuapreciate kitu ambacho amekifanya. Mimi naweza nika-appreciate media, maDj, na wasanii wenzangu basi tuapreciate pia (Adam J) ametutoa mbali ujue.”

Tofauti na hilo, Rich Mavoco ameongeza kuwa mpaka hivi sasa, kwa asilimia kubwa Adam Juma analipwa Kawaida, na Analipwa Vile Vile.
Aidha kuhusu Video yake hiyo Mpya, mavoko amedai kuwa, adam Juma na Timu yake Nzima, walisafiri Mpaka Cape Town, na wametumia Vifaa vya Kisasa, huku kazi Nzima ikifanyikia huko huko Afrika ya Kusini.


Adam Juma amewahi Kutengeneza Hit Songs za wasanii wa Muziki wa Kizazi kipya ambao Hivi sasa wamekimbilia Production za Kimataifa kama Vile OMMY DIMPOZ (Nai Nai & Baadaye) pamoja na DAIMONDS ( Kamwambie , Mawazo,Mbagala , nitarejea & Moyo wangu)

SHAVU KWA SHAVU: DIAMONDZ PLATNUMZ APATA UBALOZI, YOUNG DEE APATA UBALOZI..

1:47:00 AM Add Comment

DAR ES SALAAM, Tanzania
WAKATI Diamonds akitoa tamko Rasmi kuhusu Kuwa balozi wa Application ya MZIIK hasa kunako SMART PHONES, Muda huo Huo pia tukapata Info kuwa YOUNG DEE naye karamba Ubalozi wa Channel moja hivi ya kampuni ya STAR TIMES..sasa Hii ni Kupitia Account zao za Instagram

·        Kwa Upande Wa Diamondz “Dangote”
“Chibu Dangote” ama Nasib Abdul alikutana na Shavu la kutosha kwa Kuwa Balozi wa Application Mpya ya Simu za aina ya Smart Phones, inayoitwa MZIIKI.
Hapa tunanukuu Kauli yake
“Ningependa kukutaarifu Shabiki yangu Mpendwa kuwa, Kijana Wako sasa Ni balozi wa Application Mpya iitwayo #MZIIKI
Akamaliza Chib dangote huku kwa Chini akiitafsiri kwa Lugha ya Kiingereza kwa wale wasiofahamu Kiswahili

·        Kwa Upande Wa Young Dee
Naye rapper Young Dee ambaye hivi sasa anafanya Poa na Mkwaju mpya wa SIO MCHOYO, naye alitoa Mtonyo kuwa ni Baalozi wa Channel ya Q-YOU ya Star Times….hapa tunamnukuu

“Thanks #StarTimes for Such a Deal…..New Ambassador of #Qyou Chanel….. Its Official Now
Kwa Upande wetu TTM, tunawatakia kazi Njema, hasa katika kutangaza Bidhaa walizokabidhiwa. Ameeen


MNADA BANNER