REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

TUKIO: WAKALA MAARUFU WA M-PESA AJIPIGA RISASI..KISA?, SOMA HAPA

11:18:00 PM Add Comment

WAKALA Maarufa wa M-pesa Vodacom na Mkazi wa Kibaoni mjini Singida Mashaka Omari Makiya (30) amejipiga risasi kichwani na kusababisha kifo chake papo hapo.

Mashaka maarufu kwa jina la Mashakom, amejipiga risasi kwa kutumia bastola yake aina ya ‘silencer’ usiku wa Desemba 27 mwaka huu, nyumbani kwake Ipembe mjini hapa.

Shuhuda wa tukio hilo,Shija John amesema Desemba 28 mwaka huu saa saba mchana askari polisi walifika nyumbani kwa marehemu iliyopo mkabala na nyumba ya kulala wageni ya Meatu eneo la Ipembe.

Amesema askari polisi hao waliingia chumbani kwa Mashaka ambapo walikuta mwili wa mfanyabiashara huyo ukiwa sakafuni.Pia walikuta bastola yake ikiwa pembeni mwa mwili huo pamoja na simu zake tatu.

“Taarifa nilizonazo ni kwamba mfanyakazi wa Mashaka aligundua tukio hilo na kisha alitoa taarifa kituo kikuu cha kati cha polisi na askari walifika mara moja”,amesema.

Katika hatua nyingine, mwandishi wa habari hizi aliweza kufika kwenye moja ya maduka yake matatu ya M-pesa na kushuhudia ujumbe wa maandishi ulioachwa na Mashaka ndani ya gari lake jeusi.

Pamoja na askari polisi kukataa kutoa kibali kwa waandishi habari  kusoma ujumbe huo au kuupiga picha,watu waliobahatika kuusoma ukiwa ndani ya gari wamedai kuwa marehemu amemhusisha na kifo chake mfanyabiashara mmoja (jina tunalo) aliyekuwa na mahusiano ya karibu ya kibiashara pia marehemu Mashaka ameagiza kuwa nyumba na fedha zake wapewe wadogo zake.

Kifo cha Mashaka kimezua hofu kubwa na kazi ya uwakala wa M-pesa kwa madai kwamba katika miaka michache waliokuwa wafanyabiasha wa uwakala huo,Tembs na Rweyemamu wote wamepoteza maisha kwa kupigwa risasi.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, SACP Geofrey Kamwela amesema bado hajapata taarifa hizo na ameahidi kulifuatilia na kutoa habari ili jamii iweze kujua kilichojiri.

HII NI KUTOKA TIGO

11:14:00 PM Add Comment

Mratibu wa Promosheni za Tigo Pesa Mary Rutta akipiga simu kupata washindi watano wa shilingi milioni 10 katika droo ya pili ya promo ‘Shinda Kitita na Tigo Pesa’ mapema leo. Wengine 20 walijishindia milioni 20 kila mmoja na wengine 350 walijishindia laki 2 kila mmoja iliyofanya jumla ya shilingi milioni 160 kuzolewa. Katikati ni Meneja Bidhaa wa Tigo Husni Seif na Msimamizi kutoka Bodi ya Michezo Tanzania Humudi Abdulhussein.

JUMLA ya fedha taslimu shilingi milioni 160 zimezolewa na wateja wa Tigo mara baada ya kampuni hiyo ya simu kuchezesha droo yake ya pili katika promosheni yake ya ‘Shinda Kitita na Tigo Pesa’ iliyofanyika mapema leo katika makao makuu yao Makumbusho jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Waandishi wa Habari wakati ya droo hiyo Mratibu wa promosheni za Tigo Pesa Bi. Mary Rutta alisema kwamba wateja watano walijishindia milioni 10 kila mmoja, wateja wengine 20 wamejishindia shilingi milioni 20 kila mmoja na wengine 350 walijishindia shilingi laki mbili mbili.
Washindi watano wa zawadi nono ya shilingi milioni 10 ni  Bi. Irene Francis Mushi (25) mfanyabiashara wa vipodozi kutoka Moshi, Bi. Magadalena Daniel Asei (37) mfanyakazi wa DHL mkazi wa Kigamboni – Dar es Salaam na Bi. Hilda Laurence Nyambo (56) mfanyakazi wa kampuni ya Bima kutoka Kinondoni, Dar es Salaam.
Wengine ni Bi. Maria Juma Mbata (26) mhitimu wa Chuo Kikuu mkazi wa Iringa na Bw. Aloyce Idrisa Njole (23) mwanafunzi wa chuo cha ufundi anayetoka mkoani Morogoro.

“Tigo inafuraha kubwa sana kwa sababu imeweza kuleta tabasamu katika nyuso za wateja wake katika kipindi hiki cha mwaka mpya. Tunaamini kwamba zawadi hizi zitawafurahisha na kuwafanya washerehekee sikukuu hii ya kuuaga mwaka 2013 kuingia 2014 kwa namna ya kipekee,” alisema Bi. Rutta.

Aliongeza, “Kwa ujumla zawadi zilizoshindaniwa leo ni milioni 50 kwa washindi watano waliopatikana, milioni 40 kwa washindi 20 na milioni 70 kwa washindi 350 ambapo kila siku wateja 50 walikuwa wanajishindia shilingi laki 2 kila mmoja, iliyofanya jumla kuwa shilingi milioni 160.”

Kwa mujibu wa Mratibu huyo wa Promosheni droo hii ilikuwa ya kuanzia tarehe 24 hadi 30 Desemba.

Utaratibu wa shindano hili unaruhusu wateja waliosajiliwa na Tigo Pesa kushiriki katika promosheni hii kwa kutuma fedha, kununua bidhaa kupitia Tigo Pesa, kutoa fedha, kununua muda wa maongezi au kulipia huduma mbali mbali kupitia Tigo Pesa.

EXCLUSIVE: D'BANJ NA GENEVIEVE NNANJI..... MULE MULE

12:34:00 AM Add Comment

Ulalalaaa..Tunaweza kusema hii Iko Byee Byee kinoma, coz Wakati huku Bongo yanaenea kuwa WEMA NA DIAMOND  wamerudisha mahusiano yao, Basi Kudaadeki huko Nigeria nako mambo si mabaya.
Huu Sio umbea wala Udaku, ni kweli kabisaaaaaaaa.

D’Banji Mr KOKOMASTER himself pamoja na Muigizaji Balaa wa NOLLYWOOD, GENEVIEVE NNANJI wamerudiana Rasmi.
Aidha baada ya Kutengana Muda Miaka Miwili, D’ Banj ambaye ana umri wa Miaka 33 na GENEVIEVE ambaye anaumri wa Miaka 34, wamerejesha Mahaba ya Dhati, na inasemekana kuwa, GENEVIEVE  anaishi Nyumbani kwa D’Banji

Aidha kwa ujibu wa Mtonyo halali ni Kwamba, wawili hao hivi sasa wanazungumzia masuala ya Ndoa na kila kitu kitakuwa Byee kwa Kudra zakemwenyezi mungu

Kama ulikuwa hujui, basi tunakukumbusha kuwa, D’Banj na GENEVIEVE walianzisha mahusiano yao Mnamo Mwaka 2009 na Kumwagana mwaka 2011, huku sababu kubwa ikiwa ni D’ Banj kuwa Busy sana na kazi na hata kumsahau honey wake huyo ambaye ni Talk Of Screen

2013: RADIO NA WEASEL WANAFUNGA MWAKA KWA STAILI HII....

12:23:00 AM Add Comment

Ikiwa Ni Siku Juma Moja Tu limepita tangia KANYE WEST azungumze hadharani kuwa hatozungumza baya Lolote kwa Mtu yeyote Mwaka 2014, Finallly Mabeste wawili wanaounda kundi la GOODLIFE, Radio na Weasel nao wametoa tamko lao Rasmi….

Wakali hoa kutokea The Kaguta land (UGANDA), wamesema kuwa Mwaka huu ndo umekuwa Mwisho kwao kujihusisha na Sifa Mbaya Mitaani ikiwema Mabifu ya hapa na Pale ambayo yanaweza kuwaletea Sifa Mbaya kwa mashabiki.
Pia wameongeza kuwa, badala yake watajikita zaidi kuchomoa Mikwaju Mikali ambayo itawapa Heshima katika Muziki wao unaowika zaidi Kimataifa.


Ili kuthibitisha hilo, majembe hao wa SWEETER THAN KUKU waliingia katika page yao ya Facebook na kuandika kuwa wasanii wanatakiwa kutoa Muziki Mzuri na Mkali kwa ajili ya Jamii, na Sio kujihusisha na matukio mabaya, kwani haijengi Muziki Mzuri. Hivyo kwa Mwaka huu wamemaliza Tofauti zao na BEBE COOL pamoja na JOSEE CHAMELEONE, hivyo hawana beef hata kidogo, so wako katika Mahusiano Mazuri.

2013: HAWA WAMEIMALIZA HIVI

12:15:00 AM Add Comment

MWAKA 2013 ilikuwa ni Bonge moja la Kicheko kwa Baadhi ya wasanii Nchini marekani kutokana na kuweza Kuhit kwa Mikwaju yao na hata ALBAM zao, bila kusahau Mixtapes ambazo walikuwa wameziachia kwa nyakati tofauti.
Mfano Mzuri ni Kwa Msanii wa Kipindi hicho kutoka katika Crew ya CLIPSE, PUSHA T,ambaye Mwaka huu amechekelea balaa baada ya Albamu yake ya MY NAME IS MY NAME iliyokuwa ikisubiriwa kitambo, kufanya poa na kumrudisha rasmi katika Ramani ya Muziki.
Pia Ukimzungumzia Mtu kama Kanye West na Album yake ya YEEZUS, Eminem na Albam Yake ya MMLP2, BEYONCE na Albam yake ya BEYONCE na Wengineo wengi, utakuwa unawazungumzia wasanii ambao wameweza kufanikisha kile ambacho walichokipanga katika Kufanikisha Mchakato Mzima wa Kuvuna mikwanja ya kutosha.

Lakini Ukirejea Upande wa LIL WAYNE alionekana Kuboronga Vilivyo katika mauzo ya Albam yake ya I AM NOT A HUMAN BEING 2 ambayo pia ilimnyima nafasi kadhaa katika Tuzo Kubwa Nchini Humo kama Vile BET HIP HOP AWARDS na nyinginezo.
Tofauti na WEEZY F. BABY Kuharibu kihivyo, Pia Mkali wa DANCE, BIG SEAN, naye hakufanya Vema kupitia albam  yake HALL OF FAME, na hata kuhesabika kama projects ambavyo hazikufanya Vema.
Hata Hivyo, Lil wayne aligundua tatizo lake na kuwaomba radhi mashabiki wake huku akiahidi kufanya vema katika Mchakato Ujao, na Kuachia Mixtape ya Dedication 5 ambayo inafanya vema mpaka hivi sasa, huku track yake ya ORIGINAL SILENCE ikizidi kukata Anga za Kumwaga

MNADA BANNER