REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

VIDEO: MTOTO WA LIL WAYNE AZICHAPA NA KUNDI LA WASICHANA

2:21:00 AM Add Comment
KUSHOTO-Reginae Carter Na Mama Yake Mzazi, Picha Ndogo- Reginae Carter wakati wa Kichapo
Na Baba Juti
DAH! Hii ni hatari juu ya Hatari, na ndio maana tunasema hata uwe Mpole Vipi, ukichokonolewa tu, Lazima Kinuke Mazee

REGINAE CARTER, Binti wa Kwanza Wa Rapper Lil Wayne, alijikuta akizichapa Na Kundi la Wasichana katika Usahili wa Wanafunzi wapya wa Chuo cha CLARK-ATLANTA ( Clark-Atlanta University ) Huko Nchini Marekani.
Mbabe Wao

Kwa Mujibu wa Video Clip Pamoja na Mashahidi ambao walikuwa Eneo la Tukio, inasemekana kuwa tukio hilo Lilichukua Takriba Dakika zaidi ya Kumi, huu Kundi hilo la Wasichana ambao wanasadikika kuwa wachokozi na kuwarushia Madongo ya Hapa na Pale, likimvaa Mtoto huyo wa Lil Wayne pamoja na Rafiki yake Kipenzi LOUDES

“Ugomvi Ulitokea Ghafla baina yetu na Kundi hilo, lakini Bahati Nzuri hakuna aliyedhurika. Tuko Salama Kabisa”, alifafanua Rafiki Wa Binti wa Lil Wayne, Lourdes

Hata Hivyo Mashuhuda wengine wanadai kuwa, Reginae na Rafiki yake walikuwa na Mishe zao kawaida ingawa walichokozwa na kundi hilo ambalo pia inasemekana lilikuwa limesha-boost Vichwa vyao kwa Vilevi


Wanafunzi ambao ni Wakongwe katika Chuo Hicho ndio waliookoa Jahazi kabla ya kuzama

TUMIENI AKILI NYIE: FLOYD MAYWEATHER ALIVYOCHARUKA BAADA YA MWANAE KUSHIKA NAFASI YA PILI

2:55:00 AM Add Comment

BWANA, wanasemaga Uchungu wa Mwana aujuaye ni Mzazi, na hiki ndicho ambacho Floyd Kakionesha kwa Mwanae wa Kike aisee.

Bondia Huyo ambaye ana mkwanja Mrefu sana,  alijikuta akitibuana Vikali na majaji ambao walikuwa wanasimamia Shindano la Watoto wa Kike Kucheza, linalofahamika kama CHEERS DANCE COMPETITION, baada ya Team ya Mtoto wake wa Kike mwenye miaka 12 kushinda katika Nafasi ya Pili.

Katika Tukio hilo ambalo liligharimu majibishano ya takriban dakika zaidi ya 5, Floyd Mayweather Jr alikuwa akihitaji ufafanuzi wa kwanini Team ya Mtoto wake iliyoonekana kufanya Vizuri na kukubalika ilinyimwa Ushindi wa Juu na Badala yake wakapewa watu wengine


Ingawa majaji walijitahidi kufafanua, Bado Floyd alikuwa ni Mwingi wa Jazba na kuhoji vitu vingi sana, lakini jambo Jema hakuna aliyerusha wala kurushiwa Ngumi

KAMPUNI YA BLING BLING : T.I ACHA MBWEMBWE, LIPA MKWANJA WETU

2:41:00 AM Add Comment

Na Baba Juti
KAMPUNI inayojishughulisha na Biashara ya Vito vya Thamani a.k.a “Bling Bling”, imeamua kumburuza Mahakamani Rapper T.I ili awalipe mkwanja wao wa Takriban USD Million 1 sawa na Tshs 2,285,000,000.

Kwa Mujibu wa Mashtaka hayo, Kampuni hiyo inadai kuwa T.I mnamo Mwaka 2015, alikiuka Masharti ya Mkataba wao ambao walikuwa wamekubaliana kibiashara, huku mara ya Mwisho akichukua Bling Bling zenye thamani ya USD 75,000 sawa na Tsh 171,375,000

Ingawa T.I alionekana kukana Mashtaka na Madai hayo kutoka kwa Kampuni hiyo, wao wanadai kuwa walikuwa wakimuuzia T.I Vito vya thamani vingi sana na vilivyowagharimu kwa asilimia kubwa. Biashara hiyo ilianza Mwaka 2004 mpaka 2012 ikiwemo Chain, Saa,Dog Tags za Diamonds.

Tofauti na hivyo, T.I anatuhumiwa pia kuchukua Vito vya thamani vya Diamonds kwa ajili ya Mwanamke, ingawa hatujui kama ilikuwa ni kwa ajili ya mkewe ama Lah


Kampuni hiyo ya Madini inaongeza kuwa, Awali T.I alikuwa akiwalipa Vizuri tu kupitia Open Account ambayo walikuwa nayo, lakini ghafla alistop kufanya malipo Mwaka 2013


Na Mmiliki wa Kampuni hiyo, FEYZ AYDIN anadai kuwa, alijitahidi kwa kila mali kumkumbusha T.I kulipa Mkwanja wao, lakini hakukuwa na Mafanikio, na Ndipo walipoamua kufungua Mashtaka Dhidi yake

RICK ROSS: YUKO SALAMA KABISA

2:36:00 AM Add Comment

BWANA, sijui Yule Mlengwa atajiskiaje lakini Tayari ndo mahakama imeshaamua aisee
Hatimaye Siku ya Jana ilikuwa ni Siku Nzuri sana kwa Rick Ross a.k.a Rozay ambaye ni Big Boss wa MMG, baada ya Mashtaka yake ya KUTEKA, KUTISHIA KUUA na KUJERUHI kufutwa Rasmi.

Mashtaka hayo alikutana nayo katika Tukio ambalo limtokea kipindi cha Nyuma kidogo kwa Kumpiga, Kumjeruhi na kumteka Mfanyakazi wake wa Bustani ambaye baadaye ilimlazimu afungue Kesi mahakamani

Tukio hilo Pia lilimfanya Rick Ross akane nyuma ya Nondo kwa Week Nzima na kulipa Faini ya USD  10,000 sawa na 22,800,000 za Kitanzania tukio ambalo lilitokea Mwaka 2015 kule ATL


Lakini Baada ya Hakimu kusema kuwa, Rozzay amefanya matukio hayo kwa Mara ya Kwanza, basi anaweza kufuta Makosa yake yote endapo atashusha Mkwanja aliotajiwa

KUTANA NA TALLIA STORM, BINTI ALIYEPIGA KIBUTI NA MTOTO WA DAVID BEKHAM.

7:19:00 AM Add Comment

KWELI kabisa, Wahenga hawakuwahi kukosea hata Kidogo, maana Penzi likiwa linachanua kama Maua, basi huwa Tamu Balaa, lakini Likinyauka na kukauka kabisa, nbasi Maumivu lazima uyaone

TALLIA STORM Ni Binti Mwenye Umri wa Miaka 18, na Ni Msanii wa Pop Huko Uingereza, ila alijikuta akiingia katika Headlines zaidi baada ya kuanza Mahusiano ya Kimapenzi na Mtoto wa David Bekham, BROOKLYN BEKHAM

Lakini Baada ya Muda kadhaa, Mtoto wa Bekham alimpiga Chini Tallia na Kumuachia Kovu kubwa ndani ya Moyo wake, huku Brooklyn akiendelea na Mahusiano mengine na Binti Mwingine

Sasa, Baada ya kubaini kuwa Ex Wake Tayari yupo na mahusiano Mengine, Tallia aliamua kuaamsha naye katika Njia Nyingine kwa Kumrushia Madongo ya Nje nje japo sio kwa sauti kubwa, bali ni kwa Ujumbe tu

Katika Picha ya Hivi karibuni, Tallia alipost Picha ya Dongo kwa Mtoto huyo wa Bekham iliyokuwa imeandikwa “I DATE MEN NOT BOYS”. Sasa ukichukua Ujumbe huo, unabaini kabisa kuwa ni Dongo la moja kwa Moja kwa Brooklyn Bekham, maana yeye bado ana Umri wa “Boys”

“Baada ya Kuachana, nilimuona Brooklyn (Mtoto wa Bekham) Backstage ya Tuzo za BRITISH AWARDS. Ulikuwa ni Usiku mkubwa sana kwangu. Alijaribu kunisemesha ila Sikuwa na Muda, maana ni Mpenda Drama Sana. Ninahisi watu wengi waliona Mahusiano yetu. Lakini hivi sasa Sitaki mahusiano na Watoto, bali Wanaume” Alisema Tallia

Ila akizungumzia Kipindi cha mahaba yao, Tallia anadai kuwa, ingawa Walikuwa na Mahaba ya Kitoto zaidi, ila walijitahidi sana kuyafanya yawe ya siri zaidi. Na watu wangewaona Pamoja tu labda wakiwa wametoka Out



#DakaHiiFasta: MWANASHERIA WA YOUNG THUG AMUOKOA KATIKA KESI YA TANGU MWAKA 2015

6:44:00 AM Add Comment

KUNA kila Sababu kwa Rapper Young Thug Kumshukuru Vilivyo Mwanasheria wake ambaye amemsaidia vizuri kisheria mpaka kuepukana na Kesi ambayo Ilikuwa inamkabili

July Mwaka 2015, Mjengo wa Young Thug ulifanyiwa Msako Heavy na Polisi na taarifa kutolewa kuwa, Dawa za Kulevya aina ya COCAIN pamoja na Bastola, kitu ambacho ni Kinyume cha Sheria.

Kutokana na Tukio Hilo, Young Thug alifunguliwa mashtaka baada ya kubainika kuwa ni Kweli alikutwa na Vitu kama Hivyo Nyumbani kwake

Lakini kama “zari” vile, Mwanasheria wake alimtetea kwa kutoa Taarifa kuwa, Polisi walivamia Nyumba ya Mteja wake na kufanya Upekuzi bila Utaratibu maalum, yaani walitumia mammlaka ambayo haitambuliki Kisheria

Bada ya Swali hilo kurushwa mpaka kwa Mammlaka maalum, ilibainika kabisa kuwa ni Kweli, Nyumba ya Young Thug ilifanyiwa Ukaguzi kinyume na Utaratibu, hivyo Young Thug akawa ameponea hapo

BONUS………….

YOUNG THUG ni Jina la Kutaftia Ugali, lakini Jina Lake Kamili likiwa ni JEFFERY LAMAR WILLIAMS. Alizaliwa AUGUST 16, 1991 Huko Atlanta Georgia, USA

MNADA BANNER