REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

PICHA : CHRIS BROWN BAADA YA KUPARAMIA UKUTA NA GARI LAKE, HAPO JANA, KATIKA TUZO ZA GRAMMY

10:58:00 AM Add Comment
 HAINA NOMA WASHKAJI : Hali ikiwa inaonekana kuwa shwari baada ya kuelewana na wahusika


 PRETTY BOY : Chris Brown, siku ya Tukio


 MIZINGUO : Chris Brown akionekana kuzinguana na Jamaa fulani baada ya Tukio hilo


 TUYAMALIZE : Chris Brown akizidi kubishana


SIO MAKUSUDI : Majadiliano yakisonga mbele

 POLE BABY : Rihanna Kulia akionekana kumtuliza hasira mpenzi wake Chris Brown ili kuepusha shali


SASA MNASEMAJE KUDADEKI ZENU : Chris Brown

AKIWA bado katika Msala wa kumpiga Msanii mwenzake wa R& B, jana jumamosi Msanii Chris Brown ameingia katika Msala mwingine wa kuparamia ukuta, akiwa anatoka katika event ambayo iliandaliwa na SYMHONIC LOVE FOUNDATION, mjini Los Angels katika Studio za Debbie Allen.

Kwa Mujibu wa Makachero toka Nchini humo,inasemekana kuwa Breezy aliuvaa Ukuta huo eneo la Bevery Hills alipokuwa akijaribu kwakwepa Mapaparazi (Wadaku) wawili waliokuwa waitaka kumpiga picha

Chris anaeleza kuwa, wakai akiwa ndani ya Ndinga yake aina ya POSCHE aliona Wadaku wawili wameshuka toka kwenye gari zao na kuanza kumpiga picha, jambo ambalo lilimpa kiwewe na kuuvaa ukuta.

Aidha Chris Brown hajapata majeraha, na faraja nzito ilipatikana toka kwa Shemeji yetu Rihanna.


MUNGU WANGU : HIVI KIM KARDASHIAN ANAFANYA NINI JAMANI?

10:06:00 AM Add Comment
Hii Picha, Mwanadada huyu, Kim Kardashian, ameipiga mitaa ya Brazil katika Sanam ya YESU KRISTO.....lakini sikuelewa aikuwa anamaanisha nini kufanya hivi

MUONEKANO WETU MPYA

9:25:00 AM Add Comment

NILIPOKEA maoni sambamba na Maswali mengi sana kuhusiano na Muonekano wa Blog yangu hasa kwa Mwaka huu wa 2013, pamoja na Mabdiliko ambayo yatakuwa katika uwasilishaji wa Taarifa mbali mbali kwa Wadau wangu walioko ndani na Nje ya Nchi ya Tanzania.

Ndugu wasomaji na Wadau wa BLACK TOUCHEZ, Kimya changu cha muda kama wa miezi miwili,  hivi leo kimekuja na muonekano huu ambao unauona hivi sasa katika Blog hii. Huu ndio utakuwa ni muonekano mpya kwa mwaka huu 2013. Mwaka huu, BLACK TOUCHEZ itatawaliwa na rangi za NJANO, NYESI na NYEUPE ikiwa ndizo rangi zetu kuu, huku nyingine zikiwa ni za ziada hasa katika matukio tofauti

Frank M. Joachim "Hasta La Vista Baby", C.E.O wa BLACK TOUCHEZ

Licha ya Mabadiliko hayo yote hasa kimuonekano, bado blog hii itatoa taarifa mbali mbali kama ambavyo imezoeleka, namaaniasha Burudani toka ndani na nje ya Nchi, Michezo, Habari za ndani na Nje ya Nchi, Picha mbali mbali, Matukio kadhaa katika nyanja kadhaa.

Pamoja na hayo, BLACK TOUCHEZ badi itatoa Huduma zake za Matangazo kwa Bei nafuu kabisa ili kuweza kufanikisha moja ya hatua mbali mbali za kimanufaa kwa wafanyabiashara tofauti.

BLACK TOUCHEZ bado itahakikisha kuwa inashirikiana na Vyanzo vya habari mbali mbali kitaifa na kimataifa ili kuhakikisha kuwa unapata matukio muhimu kwa wakati muafaka.

Shukrani za dhati ziwafike EDDY MO BLAZE BLOG na ERGON ELLY BLOG kwa kuwa washirika wa karibu kabisa katika kutoa taarifa na kulifikisha gurudumu hili la Mawasiliano kwa umma kupitia mitandao ya kijamii, na ninatumaini, muda si mrefu umoja wetu utaleta hamasa kubwa kwa Wanahabari wengine kufanikisha Ndoto zao

Imetolewa na
Frank Magnus Joachim,
C.E.O
BLACK TOUCHEZ
+255714 246 914

MNADA BANNER