REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

PICHA: KUTANA NA HEATHER MILLIGAN, "KISHTOBE" WA ARNOLD SCHWARZZENEGGER, AKIWA ANAENDESHA BUGATTI VEYON, YENYE THAMANI YA USD MILIONI 2

3:25:00 AM Add Comment





MTOTO WA MICHAEL JACKSON NAYE NI MILLIONEA?

3:03:00 AM Add Comment

BLACK TOUCHEZ, Marekani
KAMA utaniuliza kuwa ni mtu gani nchini Marekani anatumia ovyo Mkwanja wake, basi Fasta nitakufyatukia kuwa ni FLOYD MAYWEATHER, ambaye alianzisha ki-team Fulani hivi kinachoitwa THE MONEY TEAM “TMT”

SASA, jambo ambalo linaonekana kuwaacha watu na Mswali kibao, ni Mtoto wa Marehem Michael Jackson, PRINCE MICHAEL JACKSON, kuonekana akiwa amepiga Maandishi ya TMT katika gari lake.

Prince alionekana akiwa katika gari hilo aina ya GMC ndani ya Weekend, huku dalili za kufuata Nyayo za FLOYD zikionekana Dhahiri, ukiachilia mbali suala la kupiga TMT katika gari lake.

Kwa Mujibu wa Wadakuzi, inasemekana kuwa, Mtoto huyo wa Michael Jackson, hivi sasa yuko anapokea Mafunzo ya BOXING huko GRACIE ACADEMY, iliyoko BEVERLY HILS, Nchini Humo, hali inayoashiria huenda akawa kama Floyd Hapo Baadaye


Baadhi ya Membaz walioko katika Team hiyo, nazungumzia THE MONY TEAM, ni Pamoja na WARREN BUFFETT, JUSTIN BIEBER na LIL WAYNE

BONGO: CYRILL HAJATOSHEKA NA ALOWA..HILI HAPA LINALOMUHUSU TENA

2:23:00 AM Add Comment

BAABKUBWA MAGAZINE, Tanzania

AKIWAKILISHA Kundi la WAKACHA, Cyrill Francisco “Kamikaze”, unaambiwa hajaridhika na Mkwaju wa Alowa, ambao Video yake inazidi kufanya Vizuri kunako macho ya watu.

Hivi Karibuni, Cyrill anatarajia kuachia Mkwaju mwingine, ambao mpaka hivi sasa anadai kuwa hajaupatia Jina, lakini Producer aliyehusika, anaitwa GOOD FATHER MBEZI.

Hapa Tunamnukuu Kamikaze kama Ifuatavyo:


” Soon tu nitaachiaki Ngoma yangu Mpya niliyofanya kwa Producer Good Father Mbezi lakini bado sijaipatia jina ila soon tu nitawajuza ma Funs wangu, kwani Alowa imefanya vizuri sana na imeweza kuniapa Morari ya kuzidi kuwapa vitu vizuri kila siku na kwa hii Joint inayokuja wataipenda sana kwani Ngoma imetulia sana wasubiri jiwe lidondoke ‘.


KUNDI la Wakacha hivi sasa linatendewa haki na Wasanii wawili, namzungumzia KAMIKAZE pamoja na JUX, ingawa hatufahamu undani wa Vichwa Vingine ama Mkwaju wa kundi zima la Wakacha

NICKI MINAJ YUKO BIZE, MSIMUULIZE KUHUSU WATOTO AISEE

2:15:00 AM Add Comment

NEW YORK, Marekani
HIT MAKER wa Annaconda, Onika “Nick” Minaji ambaye hivi sasa ana umri wa Miaka 31, amedai kuwa, hivi sasa yuko Bize sana kiasi kwamba suala la kupata Mtoto haliko akilini Mwake hata Kidogo

TTM tumenyaka moja ya Interview ambayo inadhihirisha kabisa kuwa bado hayuko tayari kupata motto wa aina yoyote na boyfriend wake SAFAREE SAMUELS, kwa sababu itambidi apige kado kwanza suala la Muziki na Biashara yake nzima Kiujumla

Minaj amedai kuwa, unapoamua kuingia katika malezi, muda mwingi itakubidi uwe makini sana na mtoto wako, hali ambayo inaweza kukufanya uzorote katika Kazi ambayo unaifanya

Aidha amesema kuwa, familia imekuwa ni kitu muhimu sana kwake, na ndio maana anahitaji kuwa tayari ili kuweza kuiandalia mazingira mazuri, na endapo atakuwa tayari kufunga Ndoa ama kuolewa na hatimaye kuwa mama, basi atafanya hivyo bila ubishi

Akizungumza kuhusu Maisha ya Famila ya Jayz ambao wanafanya Muziki na Bado wanalea vizuri tu, Minaj amedai kuwa anavutiwa sana na Beyonce hasa katika namna ambavyo anamjali mtoto wake wa Miaka 2, BLUE IVY, nab ado anakamua Kunako Stage Bila Shida.


Lil Kim ambaye pia ni Mkali wa hip Hop, hivi sasa tayari ana mtoto aliyemzaa na MR PAPERS, lakini bado anafanyab Poa na mixtape yake ya HARDCORE

KITAIFA: Jaji Warioba: Siendi Dodoma makabidhiano

2:03:00 AM Add Comment

Na Fidelis Butahe na Habel Chidawali ,Dar/Dodoma.
 Wakati Katiba inayopendekezwa ikikabidhiwa kesho kwa Rais Jakaya Kikwete, Mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba amesema hata akialikwa katika sherehe hizo hatahudhuria kutokana na majukumu aliyonayo kwa sasa.

Jaji Warioba alisema angependa kuhudhuria sherehe hiyo ambayo pia itahudhuriwa na wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, wakuu wa mikoa, mabalozi na wageni mbalimbali, lakini kutokana na dharura aliyoipata haitawezekana.

Sherehe hiyo itafanyika mkoani Dodoma kesho na Mwenyekiti wa lililokuwa Bunge Maalumu la Katiba, Samuel Sitta atakabidhi nakala ya Katiba inayopendekezwa kwa Rais Kikwete na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein.

Katika hafla hiyo itakayofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri, wajumbe wa Bunge hilo walioshiriki mchakato huo kuanzia mwanzo mpaka mwisho watapewa vyeti.

Akizungumza na gazeti hili jana, Jaji Warioba alisema hadi jana hakuwa amepata mwaliko lakini hata kama akipewa hataweza kuhudhuria. “Siwezi kutoka nje ya Dar es Salaam kwa siku mbili tatu hizi kwa sababu nina dharura. Kama wakinialika nitawaomba radhi kwamba sitaweza kuhudhuria,” alisema.

Alipoulizwa iwapo Jaji Warioba ni miongoni mwa waalikwa katika sherehe hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Rehema Nchimbi alisema angetoa majibu leo kuhusu suala hilo lakini anaamini mkongwe huyo ni miongoni mwa viongozi wastaafu, hivyo kualikwa ni lazima.
Sherehe yenyewe

Mkuu huyo wa mkoa alisema sherehe hizo zitatanguliwa na dua ya kumshukuru Mungu kwa kumaliza Bunge hilo salama ambayo itafanyika leo mchana katika Bustani ya Mwalimu Nyerere.
Wageni wengine walioalikwa ni pamoja na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama, viongozi wa dini na wengine wastaafu. “Hatuna uhakika na viongozi wengine kutoka nje ya nchi maana mwaliko umetoka kwa muda mfupi, lakini mabalozi waliopo nchini wote tumewaalika na makundi mengine yote kama wakulima, wasanii, wavuvi, wafugaji na kila anayeguswa na Katiba mwakilishi wake lazima atakuwapo,” alisema Dk Nchimbi.

Kuhusu orodha kamili ya waalikwa alisema: “Kesho (leo) naweza kuwa na majibu mazuri kwa kila kitu maana tunashirikiana na vyombo vingine katika kazi hii, kwa hiyo nitawaambia kwani vikao bado vinaendelea.”

Awali, Naibu Katibu wa lililokuwa Bunge la Katiba, Dk Thomas Kashililah alisema maandalizi ya sherehe hiyo yamefanyika chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu.

MNADA BANNER