REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

STAMINA- Humwambii kitu Kuhusu Fid Q

12:58:00 AM Add Comment
Yeeeeah...!
Lazima Nijiachie, Siku chache zilizopita nilishtuka sana kumsikia Stamina akisema kuwa kamwe humdanganyi kitu kuhusu Kamusi ya Kiswahili.Duh, ametisha
Lakini kitu ambacho kilinifurahisha zaidi kuhusu Stamina Ni hiki,
Siku chache Zilizopita katika Interview yake na Kipindi cha "Hot Mix" kinachorushwa na EATV, Stamina ambaye pia ni Memba wa Kundi la "Mtu Chee" linalowahusisha Country Boy na Young Dee, alisema wazi huku akionesha hisia zake katika kumkubali Msanii Mwenzake katika Mziki wa Mahadhi ya HIP HOP, ila Kibongo bongo tunaita "Bongo Fleva" FID Q,
Ni kitu ambacho huwa ni mara chache sana kutokea kwa wasanii wenzetu hasa hapa Bongo kukubali kazi za Wenzetu
Kaeni tayari kwa Track Mpya Stamina, "NAJUTA KUBALEHE"

NI KWELI UPINZANI HAUNA CHAKE BUNGENI...

12:43:00 AM Add Comment
Jana Wakati Nikijaribu kufuatilia Shughuli mbali mbali za Bunge, Kuna kitu ambacho kiujumla kilinifungua macho.
Ishu ilikuwa Hivi,
Mheshimiwa Tundu Lisu (CHADEMA), mbunge wa Singida, alikuwa very Crashed na Naibu Spika Wa Bunge Mheshimiwa Jobu Ndugai jana Bungeni, alipotaka kuomba idhini ya kutoa Hoja ya kusitisha uchangiaji wa Bajeti ya Wizara ya Kilimo iliyokuwa ikiendelea, ili kujadili suala la Ajari ya Boti ya MV SKAGET iliyotokea siku chache zilizopita na kupoteza maisha ya zaidi ya Watu 30.
Lakini kama haitoshi, Mheshimiwa Ndugai, alionekana kumtetea Mwanasheria Mkuu wa Serikali kufuatia kauli yake "Ukiwa na Nywele nyingi, sio kuwa na Akili za kufikilia", hali ambayo iliwafanya Wabunge wa Upinzani kuondoka.....
Watanzania wengi tumeona, na kusikia Kauli ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, na Maamuzi yanayotolewa na Viongozi wa Bunge
Yap. Kuna mambo Mengine ambayo Upande wa Upinzani unakuwa hauko sawa, laikini kwenye hili, hapana....

















Mh. Tundu Lisu akichangia Jambo Bungeni

MNADA BANNER