REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

UCHUMBA KWA NICKI MINAJ : DJ Khaleed Hajakata tamaa, na hatokata Tamaa

2:55:00 AM Add Comment

IKO HIVI....
Kama Unadhani Dj Kahleed alikuwa anatania katika Hatua ya Kumuomba Uchumba mwanamama Nicki Minaji, basi jamaa hakuwa hivyo.

Akiwa katika Interview na POWER 106, CEO huyo wa WE THE BEST alisisitiza kuwa hakuwa anatania kumuomba Uchumba Memba huyo wa YMCMB (Nicki), bali ameelezea uwazi juu ya Hisia Zake

"Nilitakiwa kuwa Muwazi katika Hili. Ninampenda sana na Imenibidi niamue kumuomba Uchumba ili hatimaye Nifunge naye Ndoa. Ni rafiki angu Kweli" Alisema Khaleed , ambapo pia kauli yake iliungwa Mkono na Rafiki ake wa Karibu RICK ROSS  "The Boss"

Pia Khaleed aliongeza kuwa, anaamini Minaj na Yeye wanaendana kabisa kiasi kwamba huenda ikawa Rahisi kwao kufikia hatua Nzuri

"Kama akinitolea Nje, ni sawa coz ndio mapenzi. Minaj ni Rafiki angu na ninaliheshimu hilo. Labda atakuwa hajawa tayari kwa Ndoa. Ninahitaji watoto sasa, na mambo mengine Mengi tu"

Mpaka Hivi sasa Nicki Minaji hajajibu chochote kuhusiana na Ombi la Dj Khaleed.





MNADA BANNER