REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

 MADONNA, LADY GAGA, BEYONCE NA NICK MINAJI, NI MIONGONI MWA WASANII WA KIKE WENYE MKWANJA

5:51:00 AM Add Comment



Ladies are Getting Hot katika Kipindi Hiki….

Kwa Mujibu wa jarida la FORBES, Madonna, Nicki Minaji, Lady Gaga na Beyonce ni miongoni mwa Wasanii wa kike wanaoongoza kwa kuingiza kiasi kikubwa Cha Fedha kutokana na Shughuli zao Mbali mbali sambamba na Muziki.

Kwa Mwaka Huu, Madonna ameonekana kupata neema ya aina yake baada ya kutangazwa kuwa Msanii wa Kike anayetengeneza Fedha kupita Wote Duniani,baada ya Kuingiza kiasi cha zaidi ya Dola MILIONI 120 kwa Mwaka Huu.

Tofauti na Madonna, hasimu wake katika Muziki huo wa Pop, Lady Gaga, amedaka nafasi ya Pili kwa kutengeneza kiasi cha Dola Milioni 80, Taylor Swift akishika nafasi ya Tatu kwa Kuvuna Dola Milioni 55.

Nafasi ya Nne imebebwa na Mwanamama BEYONCE ambaye amweza Kutengeneza Kiasi cha Dola Milioni 53, huku nafasi ya Tano ikishikiliwa na Mkongwe anayejua kuachika, JENIFER LOPEZ ambaye pia ameingiza Dola Milioni 45.

Wakali wengine katika Jinsia hiyo Hiyo ya Kike, ni pamoja na Rihanna, ambaye amedaka Dola Milioni 43, Katy Perry ambaye ameingiza Dola Milioni 39, Mwanamama na Mkongwe Pink ameweza kupata Dola Milioni 32, Carrie Underwood amevuna Dola Milioni 31, Mariah Carey ambaye pia amevuna Dola Milioni 29, pamoja na Nick Minaji ambaye amevuta Dola Milioni 29 Mwaka Huu.

LIL WAYNE AMETOSWA NA MPENZI WAKE WALIODUMU KWA MUDA WA MIAKA 6?..MAANA ALICHOKIPOST HUYU DADA HATA SIELEWI

5:48:00 AM Add Comment


MNADA BANNER