REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

KUTANA NA CELEBS 5, KATI YA 10, AMBAO RAPPER DRAKE AMEKUNJUKA NAO…

2:57:00 AM Add Comment

KUTOKA BLACK TOUCHEZ,
WENGI tulikuwa tukidhani kuwa Rapper Kutoka YMCMB, Drake, alikunjuka na Robbin Fentty Rihanna Peke yake, lakini kumbe kuna Wengine ambao wanamajina yao katika Burudani Industry ulimwenguni kote.

Wafukuza mapepo Leo Tunashusha Full List ya Waliofyatuka na Dreezy katika Kitu kinachofahamika kwa Jina la Mahaba.


1. SELENA WILLIAMS-2015.
Dreezy alianza kuonekana  karibu na Serena Williams ambaye ni Mcheza Tenis asiyeshikika, aktika Baadhi ya Mechi ambazo amekuwa akishiriki. Tofauti na Hilo, Hivi karibuni, wawili ahoa walionekana kuwa pamoja katika Moja ya Migahawa , na ilikuwa ni mazingira ya Usiku.

Mnamo Mwaka 2011, Dreezy alijikuta akiingia katika Bifu kali na rapper Common baada ya kusadikika kuwa anakunjuka na Serena, ikiwa kipindi hicho Common na Serena walikuwa ndo kwanza wamepigana Chini.

Common alifikia hatua ya kuthibitisha kuwa ni kweli amepigana Chini na Serena, na alifahamu kabisa kuwa Drake na Serena Walikuwa na mahusiano, kitu ambacho hakuwa na Shida Nacho. Lakini kilichomfanya aanzishe noma na Dreezy, ni baada ya kuhisi kuwa, Nyimbo Nyingi zilizokuwa zikitungwa na rapper Huyo kutoka Toronto Canada, zilikuwa zikimhusu Yeye (Common)


2. RIHANNA : 2009-2010
UHUSIANO wao ulianza kufahamika kuanzia Mwaka 2009 mpaka 2010 ambapo wawili hawa hawakuweza kupiga hatua Nyingine.

Kipindi Hicho Riri alikuwa amepigana Chini na Breezy, lakini Mwisho wa siku akajikuta akiangukia Mikononi mwa Rapper Huyo aliyevunja na Mkwaju wa STARTED FROM THE BOTTOM.

Lakini baada ya Kupigana Chini, Dreezy alifyatuka kuwa, Kitendo ambacho Rihanna alimfanyia, ni malipo ya kile ambacho Drake mwenyewe aliwafanyia wanawake wengine ambao aliwahi kuwa nao katika mahusiano.


3.TYLA BANKS.
INGAWA Hakuweza kudandiana naye Kimahaba, Darke alithibitisha kuwa, aliwahi kumfukuzia Bibi Huyu ambaye ni hatari katika Suala Zima la mitindo.

Akikiri hilo, Dreezy alidai kuwa ni kweli aliwahi kuenjoy naye vizuri katika Date Night yao, ambapo walienda eneo pendwa sana Nchini marekani, DISNEY.


4. CAT WASHINGTON : 2009
CAT WASHINGTON alifahamika sana kupiti Kipindi cha TV kinachofahamika kwa jina la BAD GIRLS CLUB.
Dreezy alikutana na Bibie huyu kupitia Video ya BEST I  EVER HAD, na ilikuwa ni Mwaka 2009.

Washington anadai kuwa, aliweza kuenjoy sana na Drake, na kila mmoja alikuwa amekufa ameoza kwa mwenzake, hivyo lilikuwa ni Penzi tamu sana.


5. KEISHA CHANTE.
KEISHA amewahi kuwa Mtangazaji wa Kipindi cha 106 & PARK cha BET,. Na aliweza kutengeneza Jina kubwa sana kupita Maelezo.

Kwa mujibu wa maelezo yake, Keisha na Drake waliwahi kuwa na mahusiano wakiwa na Umri wa Miaka 14, kitu ambacho anadai walikifurahia sana.


Keisha anasema kuwa, walikutana baada ya Yeye kuhamia Toronto-Canada kwa ajili ya Shughuli za Muziki, na kipindi hicho Drake alikuwa yuko katika Tasnia ya Burudani.

PICHA NNE: LOWASSA AKIWA KATIKA SOKO LA TANDALE

2:42:00 AM Add Comment

Mgombea Uraisi wa Chadema anayewakilisha UKAWA Mh Edward Lowassa leo ameendelea na ziara yake ya kutembelea wananchi katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam! Leo asubuhi alitembelea eneo la Tandale.




ZITTO KABWE: “WASANII WA TANZANIA, KAMPENI ZIKIISHA, NA THAMANI YENU IMEISHA”

2:38:00 AM Add Comment

KUTOKA BLACK TOUCHEZ
MGOMBEA Ubunge kwa Jimbo la Kigoma Mjini Kwa Tiketi ya ACT-MAENDELEO, Zitto kabwe, ameamua kuwatolea Uvivu wasanii mbali mbali Nchini Tanzania, ambao kiujumla hivi sasa wameelekeza Macho yao katika Siasa.

Katika Kufafanua zaidi, Zitto ameonekana kukwazwa zaidi na namna ambavyo wasanii ambao hivi leo wanawaimbia Viongozi wa Siasa ambao Kiujumla hawakuwahi hata kuzungumzia Suala lolote linalohusu Mslahi yao.

Zitto kayasema hayo Kupitia Instagram account yake, ikiwa ni baada ya Kupost Picha ya Mohamed Mwikongi-Frank, ambaye anagombea Ubunge Pia kwa Ticketi ya ACT.

Tunamnukuu
“Wasanii wa Tanzania, wakati tunatetea kazi zenu kurasmishwa ili mfaidi jasho lenu, hawa mnaowaimbia Leo hawaikuinua mdomo wao kuwatetea. Kampeni zikiisha na thamani yenu imeisha. Tulipopaza sauti kupinga unyonyaji wa makampuni ya simu kwenye RBT hawa wanaoahidi kuwatetea Leo hata habari walikuwa hawana. Naomba mtafakari sana hatma ya tasnia yenu.”


MNAZUNGUMZIAJE KAULI YA ZITTO.

TAARIFA KUHUSU UJAUZITO WA MARIAH CAREY

1:45:00 AM Add Comment

MITANDAO mbali mbali ya Kijamii Nchini marekani, ilianza kutoa taarifa kuwa Mariah Carey (45) hivi sasa ni mjamzito.

Lakini kama haitoshi, jamaa ambaye alitajwa kuhusika na Ujauzito huo, ni Billionea JAMES PACKER, tajiri ambaye anamiliki CASINO mbali Mbali Nchini Marekani.

Lakini Baada ya taarifa Hizo Kuzagaa na hata kupambwa haswa, hatimaye Mtandao wa Gossip Cop ulifyatua jibu kuwa, Carey na Mpenzi wake huyo , hawatarajii kupata Mtoto yeyote, na taarifa ambazo zinazidi kusambaa, hazina ukweli wowote.


Mariah carey ambaye Hivi sasa ana watoto wawili wenye Umri wa Miaka 4, alianzisha mahusiano yake na James Packer, ikiwa ni baada ya kuachana na Mumewe wa Ndoa, NICK CANNON.

DRAKE NA SERENA WILLIAMS…HALIFICHIKI PEMBE LA NG’OMBE

1:05:00 AM Add Comment

HATIMAYE yametimia ikiwa ni dhahiri kabisa kuwa Zile Fununu za Drake na Serena kuanzisha Uhusiano wa Kimapenzi, zimekuwa KWELI.

Kwa Mujibu wa Mtandao wa TMZ, Serena na Dreezy walionekana wakipeana “Mabusu-Mahaba”  Katika Mgahawa wa CINCINNATI, Weekend Hii (AUGUST 23).

Wawili hao kwa mara nyingine walionekana wakipiga  “Dinner” Kibongo Bongo tumezoea kusema Chakula Cha Jioni katika Mgahawa wa SOTTO, ikiwa ni baada ya Serena  kutwaa Taji la WTA.

MNADA BANNER