REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

MAKUBWA !!!!!!!! : MSANII BOBBY VALENTINO KATIKA TUHUMA ZA UBAKAJI

7:36:00 AM Add Comment

Na Rich Sam  
WATU WA MUNGU mambo yanazidi kuwa makubwa sana ndani ya Mwaka huu wa 2018 ukizingatia bado ni Mapemaaaaaaaaa...kabisa aisee!

Baada ya kumaliza ile kashfa ya kumkimbia Kahaba ambaye alimtumia katika Starehe zake bila kumlipa, na siri ikafichuka kuwa kumbe yule ni Dume aliybadili jinsia na kuwa mwanamke, yameibuka mengineyo watu wa mungu dhidi ya Msanii Boby Valentino.

Bobby Valentino ambaye hivi sasa hana chochote katika soko la Muziki wa kizazi kipya Duniani, anatuhumiwa kumbaka mwanamke (jina limehifadhiwa) usiku wa Jumapili na tayari yuko Chini ya Upelelezi wa Jeshi La Polisi Nchini Humo

Taarifa za kipolisi kutoka katika jimbo la COBB COUNTY, Huko Georgia Marekani, mwanamke huyo kafungua mashtaka dhidi ya Hitmaker huyo wa SLOW DOWN hasa kwa kitendo hicho cha ubakaji ambacho ni kinyume cha sheria na haki za binadamu

Pia ripoti inafafanua kuwa, tukio hilo lilifanyika Nyumbani kwa msanii huyo, na taarifa zaidi zitatolewa mara baada ya uchunguzi kamili kukamilika

Hata Hivyo, Msemaji wa Bobby Valentino amejitokeza na kudai kuwa, kitendo anachokifanya mwanamke huyo, ni kutumia njia za uwongo ili kujipatia fedha, kitu ambacho Boby Valentino hakubaliani nacho na ni taarifa za Uwongo

TULICHOKISIKIA KATIKA INTERVIEW YA RASCO SEMBO KUPITIA JEMBE FM 93.7, KUHUSU DEEY CLASSIC, NGOMA YAKE NA MR BLUE KUTOKUPIGA HATUA, NA MENGINEYO

7:00:00 AM Add Comment

Na Baba Juti  
LEO Kupitia Interview na Kipindi cha HIT ZONE kinachomilikiwa na 93.7 Jembe Fm-Mwanza, Msanii Rasco Sembo amezungumza Mengi sana kuhusu Muziki wake hasa ikiwemo kuitambulisha Track yake Mpya inayoitwa "Changa Karata"

Akijibu maswali katika Kipindi hicho, Rasco sembo amezungumza namna ambavyo ukaribu wake ulivyo na Producer Deey Classic, ambaye wengi tunafahamu kuwa ni Meneja wake na amekuwa akimsukuma katika soko la Muziki kwa Njia tofauti

Ukiachilia mbali hayo, Pia Rasco amezungumzia namna ambavyo wadau mbali mbali hasa Wasanii Wenzake wanatakiwa kuelewa kuhusu comments zao dhidi ya kutokufanya Vizuri kwa Track ambayo amefanya na Mr Blue pamoja na Mo Music

Full Interview Hii Hapa

MNADA BANNER