REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

WAPIGANAJI 30 WA BOKO HARAMU WAUAWA

3:59:00 AM Add Comment

Wapiganaji wasiopungua 30 wa kundi la Boko Haram wameuawa kaskazini mwa Nigeria kufuatia mapigano baina yao na vikosi vya serikali ya nchi hiyo.

 Msemaji wa Jeshi la Nigeria Eli Lazarus ametangaza kwamba, mapigano makali yamejiri baina ya vikosi vya serikali na wanamgambo wa Boko Haram katika mkoa wa Yobe ulioko kaskazini mwa nchi hiyo ambapo kwa akali wapigani 30 wa kundi hilo wameuawa. 

Luteni Lazarus amesema kwamba, mapigano hayo yalidumu kwa masaa kadhaa na kwamba, kamanda wa Boko Haram katika mji wa Damaturu ameuawa katika mapigano hayo. Taarifa zaidi zinasema kwamba, mapigano hayo yalitokea baada ya vikosi vya serikali ya Nigeria kuanzisha mashambulio dhidi ya eneo moja mjini Yobe ambalo ni maficho ya Boko Haram. 

Majeshi ya Nigeria yamefanikiwa kuwatia mbaroni wapigani 10 wa Boko Haram katika mapigano hayo sambamba na kugundua na kukamata silaha nyingi, imebainisha taarifa ya jeshi la nchi hiyo.

WAISLAAM WAENDELEZA LAANA YAO...........

3:48:00 AM Add Comment

Waislamu wa pembe mbalimbali ulimwenguni wameendelea kulaani filamu ya Kimarekani ya "Innocence of Muslims" inayomvunjia heshima Mtume saw. 

Miji mbalimbali ya Iran ukiwemo mji wa Qum imeshuhudia mikusanyiko na maandamano ya kulaani filamu hiyo; ambapo waandamanaji walijitokeza katika bararaba za miji hiyo na kupaza sauti wakilaani filamu hiyo.

 "Mauti kwa Marekani", "Mauti kwa Israel" na "Labbaika Yaa Muhammad" ni baadhi ya nara zilizopigwa na waandamanaji katika mudhahara huo ambapo walikuwa wamebeba mabango na maberamu yaliyokuwa na maandishi ya yaliyokuwa na jumbe mbalimbali. 

Mji wa  Karachi nchini Pakistan, nao umeshuhudia maandamano makubwa ya Waislamu ya kulaani filamu hiyo ya Kimarekani inayomtusi na kumvunjia heshima Mtume wa Uislamu. 

Wakati huo huo, habari kutoka London Uingereza zinasema kuwa, Waislamu wa mji huo wameandamana na kulaani filamu hiyo huku wakitoa wito wa kupasishwa sheria za kupiga marufuku kuvunjia heshima Uislamu na matukufu yake.

MNADA BANNER