REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

EMMY'S LAMODA- KWA SUPPA DADAZ WA MWANZA..UFANYE MTOKO WAKO WA KIJANJA KUWA HIVI

6:57:00 AM Add Comment




PICHA: AFRICAN BARRICK GOLD MINING WADHAMINI TIBA YA UPASUAJI BURE KWA KICHWA, MGONGO NA MISHIPA YA FAHAMU KATIKA HOSPITALI YA BUGANDO MWANZA.

6:49:00 AM Add Comment












LICHA ya kuwa na Madaktari bingwa wa upasuaji wa kichwa wasiozidi watano tu nchini, wodi za kitengo cha upasuaji wa kichwa na mifupa cha Hospitali ya Rufaa ya Taifa Mhimbili (MOI) jijini Dar es Salaam, zimefurika wagonjwa.

Mratibu wa jopo la madakatari bingwa saba wa MOI walioweka kambi maalum ya matibabu ya mgongo na upasuaji kichwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando (BMC) jijini Mwanza, Dkt Othman Kiloloma, amesema hali hiyo ni moja ya changamoto kubwa inayokikabili kitengo hicho.

Amedai, kutokana na kusubiri matibabu hayo kwa muda mrefu, baadhi ya wagonjwa wa nje ya Dar es salaam huishiwa fedha za kujikimu na hata nauli, hivyo Madkatari hao kulazimika kuwasaidiwa nauli za kuwarudisha makwao.

Dkt Kiloloma alisema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi kabla ya uzinduzi wa Matibabu ya mgongo na upasuaji kichwa unaofanywa na wataalam hao hapa, kwa kushirikiana na madakatari bingwa wa BMC. 

Matibabu hayo yanayotolewa bure kwa ufadhili wa kampuni ya African Barrick Gold katika hospitali ya Bugando, yalianza juzi (Machi 24) na yataendelea hadi Machi 28 mwaka huu ambapo wagonjwa zaidi 33 wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji mkubwa wa vichwa na kutibiwa migongo.

“Wodi zetu zimejaa wagonjwa wetu wanasubiri kwa muda mrefu, ukituletea mgonjwa atalala wapi wakati wamejaa hadi kwenye makorido lakini hatuwezi kuwafukuza.” Alieleza Dkt Kiloloma wakati akionyesha picha za wagonjwa waliolazwa MOI, walivyofurika.

Alisema kupeleka wagonjwa wa aina hiyo Dar ni gharama kubwa hivyo ndiyo maana jopo hilo kwa ufadhili wa kampuni hiyo ya uchimbaji madini nchini, limeweka kambi Bugando ili kuwasaidia wagonjwa waliopo kanda ya ziwa ambao ingebidi wapelekwe Mhimbili au nje ya nchi kwa matibabu hayo.

“Kati ya Madaktari saba tuliotoka MOI kuja Mwanza kuungana na wenetu wa Bugando kusaidia wangonjwa wa Kanda hii ya ziwa, mabingwa wa upasuaji wa kichwa tupo watatu. Tanzania nzima ina mabingwa wa Upasuaji kichwa wasiozidi watano, hivyo wawili ndio wamebaki Dar.” Alieleza bingwa huyo na kudai upungufu wa wataalamu hao ni changamoto kubwa inayolikabili taifa.
Alieleza kwamba kukamilika kwa jengo la ghorofa nane linalojengwa MOI kutasaidia kuondoa mlundikano wa wagonjwa ambao sasa wanakosa pa kulala licha ya wengine kuwa nje ya wodi wakisubiri matibabu. 

“Tunapasua wagonjwa 600 kwa mwezi lakini kutokana na kusubiri matibabu kwa muda mrefu kidogo, baadhi au wauguzi wao huishiwa fedha za kujikimu na kulazimika kuwasaidia nauli ya kurudi kwao, wengine (akina mama) hukuta waume zao walisha oa wanawake wengine.” Alidai.

CREDIT: G-SENGO

PICHA: SIO MBIO TU, HATA HUKU YUPO. MCHEKI MWANARIADHA BOLT AKIJIACHIA

2:57:00 AM Add Comment


BABY MADAHA ATUSUA …TRACK YAKE NA JOE CANDY YAPIGA TOP 5 UK CHART REVERBNATION.

2:18:00 AM Add Comment

CANDY n CANDY RECORDS Nchini Kenya huenda ikazaa matunda na hata kupata Sifa kama Lupita Nyong’o ambaye hivi sasa ni talk of the World.

The real Good News ni Kwamba, Track ya NICE & SLOW ambayo Mtanzania BABY MADAHA na JOE CANDY waliifanyia vema, imeweza kushika NAMBA 4 Mpaka hivi sasa Kupitia TOP 30 CHART UK katika Mtandao wa REVERB NATION.

Aidha Track Hiyo ambayo imejaa Utamu wa Kutosha, imehusisha Sauti Fulani hivi za kimahaba zikiwa zinanong’oneza, ambazo ahusika wa sauti hizo ni wa Kujiita QUEEN OF SWAGGZ – BABY MADAHA, huku Vocal La kiume kutoka kwa JOE CANDY, likijibu kwa mbali maneno Fulani hivi.

Tofuti na Audio Hiyo ambayo inazidi kupeta kama hivyo,  Video ya Track hiyo NICE & SLOW imeshakamilika na jana ndo imeingizwa rasmi kunako mtandao wa Youtube.

Video hiyo Clean kabisa ikiwa na vikolombwezo kibao, imesimamiwa na kampuni ya PLATNUM –HYP FILMS kwa ushirikiano mzuri na Candy n Candy Records.


Big Up Kwa Baby Madaha na Candy N Candy Records Nchini kenya

CHECK VIDEO YAKE HAPA..

NIGERIA: OLAMIDE AKANUSHA KUTARAJIA MTOTO NA MPENZI WAKE WA MUDA MREFU..AUSHAMBULIA MTANDAO ULIOPOST TAARIFA HIYO…

2:09:00 AM Add Comment

RAPA Olamide kutoka OBINAH LAND, NIGERIA, amekanusha vikali Taarifa Feki ambazo Zilitolewa na mtandao wa LINDA IKEJI kuwa Yeye na Mpenzi wake wa zamani wanatarajia kupata Mtoto Muda si mrefu.

Taarifa hiyo ambayo ilianza kupata macho ya kutosha Kutoka Kwa wasomaji, ilijieleza kuwa Olamide anatarajia kuungana na mastaa wengine nchini Nigeria, ambao tayari wana watoto, jambo ambalo Olamide ambaye aliweza kuteka akili ya mashabiki wake kibao wa Nigeria kupitia Track yake ya FIRST OF ALL pamoja na ELEDA MI ambayo ilitoka miezi miwili iliyopita, aliikanusha na Kusema hatarajii kupata Mtoto na Mpenzi wake Huyo ADEBUKUNMI AISHA SULEIMAN, wala Binti Mwingine yeyote.

Kupitia Account yake ya Twitter, Olamide alisema kuwa alitarajia kuona Habari Hiyo feki ikitolewa na Mitandao Njaa yote nchini humo, lakini Sio Mtanda wa Linda ikeji, maana naamini mhusika (LINDA) ni mtu anayejitambua na kutengeneza Info sahihi.

Tofauti na hilo, Olamide Pia alimkandia zaidi kuwa, hatakiwi kutumia Jina lake na hata ya Wengine vibaya kuandika mambo yasiyo na Ukweli wowote, na anasikitishwa sana na taarifa hiyo ya kipuuzi 



kupewa nafasi katika, wakati kila siku akiachia Nyimbo na Video haziwekwi kunako Mtandao huo.


Kwa Upande wake Mmiliki wa Mtandao huo, alikiri kuwa yeye anavyanzo mbali mbali ambavyo humpatia taarifa kadhaa , na ndiko alikotoa taarifa hiyo, na kuhusu suala la kutokuweka Video na Audio zake katika Mtandao wa Linda, ni kwa sababu huwa hazipati

KUNA SAA HIZI ZA BURE TOKA KWA RICK ROSS KAMA ALBAM YAKE ITAGONGA NAMBA 1 KATIKA MAUZO.

1:58:00 AM Add Comment

HATA kama Ningekuwa Mie, ningetamani Kabisa kufanya kazi na RICK ROSS kutokana na gharama ya zawadi anayotarajia kuitoa.

THE MMG BOUS, Rick “Rozay” ametangaza Kutoa zawadi ya Saa zaGharama sana kwa majembe yake DJ KHALEED, MEK MILL na WALLE ambao Wailtoa Support ya Dhat katika Kukamilika Kwa Albamu hiyo.

Ili Kuonesha kuwa Yuko Serious na Ahadi hiyo, ROZAY kutokea MIAMI alionekana katika Duka moja huko Jijini New York, linalofahamika kwa Jina RAFAELLO & CO, na Inasemekana alisalimisha Pesa nyingi sana.

Rozay alionekana akinunua Saa Hizo sita ambazo zitahusika kwa Wote ambao Pia walishirikishwa Kunako Albamu Hiyo ya MASTERMIND ambayo iliingia Sokoni rasmi, March 12

KANYE WEST AANGUKIA TENA DANGER ZONE…

1:54:00 AM Add Comment

ULALALAAAAA….
Chochote Kinachotuhusu Lazima TTM tukupe Mtonyo kama kawaida, sasa Iko Hivi

RAPA Kutoka kunako Jiji la CHICAGO, Nchini marekani, Kanye West, usiku wa kuamkia leo aliingia kunako danger Zone yake baada ya kujikuta akiwa amezungukwa na watu anaowachukia kupita kitu chochote, yaani mapaparazi.

Unaweza kujiuliza ni hatua gani ambayo YEEZY aliichukua maana huwa anapiga Ngumi na mateke pale anaposumbuliwa na Mapaparazi hao, lakini hali hiyo ilikuwa tofauti kutokana na kutumikia kifungo Cha Nje cha Miaka miwili, baada ya kukutwa na hatia ya kumpa kipigo Mpiga Picha Mmoja huko LOS ANGELS.

Tukio hilo lilitokea katika uwanja wa Ndege huko huko Nchini Marekani, ambapo baada ya kutoka tu maeneo ya Nje, alikutana na nyomi hilo la wana habari, huku mmoja wa Wapiga picha hao kutokea TMZ akimuuliza swali kuhusu Picha yake na Kim Kardashian Kuonekana kwenye Front Cover ya jarida la VOGUE.


Licha ya Kuulizwa maswali mengi sana na wapiga picha hao huku Upigaji Picha ukiendelea, Kanye West bado alionekana kuwa Mdogo kama Pilitoni, na kugoma kujibu Kila swali ambalo liliulizwa maeneo hayo.

MNADA BANNER