REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

DEEY CLASSIC: FRED SWAGG ALIWAPA CHANGAMOTO YOUNG KILLER MSODOKI NA KADGO KATIKA TRACK HII.

7:02:00 AM Add Comment

LEO Ilikuwa ni Official Release ya Track Kali ya THE LYRICKS iliyowahusisha FRED SWAGG YOUNG KILER na KADGO kupitia TTM ya JAM SESSION , 99.4 MHz- METRO FM, Mwanza.

Kuachiwa Huko rasmi kulijumuisha Interview kutoka kwa DEEY CLASSIC pamoja na FREDD SWAGG ambaye ndiye mmiliki wa Track Hiyo.

Katika Melezo Yake DDEY ambaye hivi sasa Ni Producer waRevolution Sound, amesema Kuwa Fred ambaye Hivi sasa ni MSANII wa LABEL yake, alikuwa Ni Changamoto kwa Rapa Young Killer na Kadgo, hasa Baada ya Kumsikia (Fred) katika Verse ya Pili.


Msikilize DEEY na FRED:





BIG DADY OXS OKELEKY: MUZIKI WANGU, FLOW ZANGU, ZINA KILA HAKI YA KUITWA CLASSIC.

6:20:00 AM Add Comment

BAADA ya Kuachia Track mbili Mfululizo kutoka katika maktaba ya Nyimbo zake, RPA Kutoka Jijini Mwanza, OXS OKELLEKY amesisitiza Kuwa Muziki wake bado unadai katika Soko la Rap Music, na hata Flow zake bado ni zaidi ya Ubora unaodhaniwa.

OXS ambaye ameachia Track zake Mbili hapo jana, Ikwemo Track ya HOPE ambayo ameshirikiana na Producer Q-THE DON na ZOMBIE, amesema kuwa Experince Yake katika Muziki, mara nyingi imemfanya Awe tofauti na wasanii Wengine wa Mwanza , jambo ambalo anaamini linamfanya awe UNIQUE.

Pia Big dady ameongeza Kuwa, muda mwingi alikuwa amehifadhi hizo Nyimbo, ili kuangalia Soko la MUZIKI wa HIP HOP unamapokeo gani jijini Mwanza na hata Tanzania.

Pia Oxs ameshiriki katika Production ya Track ya WASHAMBA iliyoimbwa na Marehemu ALBERT MANGWAIR akiwa amemshirikisha DARK MASTER, huku Producer Mkuu akiwa ni Q-THE DON







KUDADADEKI…KUMBE GARI LA JUSTIN BIEBER HAJANUNULIWA YEYE….

3:17:00 AM Add Comment

ULALALALAAA..KWELI JUSTIN BIEBER ATABAKI KUWA THE MAJANGA BOY SABABU KILA ANALOFANYA HUWA NI SEHEMU YA MAJANGA.

BAADA ya Siku ya Jana TTM ukupa full mtonyo kuwa Bwana Mdogo Bieber amepewa Zawadi na YMCMB Boaus BIRD MAN, Finally tumefunguliwa macho kuwa, Ndinga ile aina ya BUGATTI yenye Thamani kubwa sana Kimkwanja, hakupewa zawadi na Birdman, Bali kuna tetesi kuwa, huenda akawa ameazimwa na Birdman kwa ajili ya matumizi, ama akawa amekopeshwa.

Kwa Mujibu wa Chanzo ambacho kinaufahamu Mchongo mzima, kinadai kuwa, Bwana Bieber alitumia Statement ya Uongo kupitia Mitandao Mbali mbali ya Kijamii kuwa amepewa zawadi ya Bugatti na 
Birdman hivyo amefurahi sana.

Lakini Kumbe full data ni Kwamba, BIRDMAN alitoa kauli Moja Tu kwa Justin Bieber, kuwa Endapo atapenda Kutumia Gari hiyo akiwa MIAMI, basi anakaribishwa kulitumia.

So ask yourself…what next

2 CHAINS HANA HATIA …

3:13:00 AM Add Comment

JUMA LILILOPITA , TTM TULIKUPA MTONYO KUWA RAPA 2 CHAINZ ATAPANDISHWA KIZIMBANI KUWEZA KUPOKEA HUKUMU YA MASHTAKA YANAYOMKABILI YA KUKUTWA NA DAWA YA  CODEIN AMBAZO HUTUMIKA KUTENGENEZA DAWA ZA KULEVYA AINA YA SIZZURP.

Baada ya KICHICHI (KITENGO CHIMBUA CHIMBUA) ya TTM kufuatilia kwa Ukaribu kuhusu ishu hiyo, finally tumezinyaka kuwa, Rappa huyo amekutwa hana hatia na kesi inayomkabili

Kwa mujibu wa TMZ, inasemekana kuwa Kesi hiyo wala haikuchukua Mud asana, na Info zilizozagaa ni kwamba 2 Chainz Maarufu kama TITY BOY amekutwa hana hatia.


Iwapo Rapa huyo angedakwa na hatia, basi Angekaa Nyuma ya Nondo kwa Muda wa Miaka 3

50 CENTS APIGWA CHINI KATIKA KESI YA HEADPHONES.

3:06:00 AM Add Comment

KAMA UTAKUWA NI MDAU MZURI TU WA RAPA 50 CENTS, TTM INAAMINI UTAKUWA UNAFAHAMU KUWA RAPA HUYO YUKO NDANI YA “BIG” BEEF NA KAMPUNI YA SLEEK AUDIO KWA MADAI YA KUIBA DESIGN YA HEADPHONES PAMOJA NA BAADHI YA DATA AMBAZO ZILIKUWA ZINATUMIKA KISIRI SIRI

TTM tumenyaka Updates kuwa Ishu hiyo ama Kesi hiyo ilikuwa ikiendelea, na Kwa mara nyingine tena, RAPA FIF amejikuta akishindwa katika Kesi hiyo ambayo Wengi wanaamini ilimuumiza Sana kichwa.

Mnamo 2013, 50 Cents aliifungulia mashtaka Kampuni hiyo ya SLEEK AUDIO huku akilalamika Kuwa, anaidai kampuni hiyo jumla ya DOLAR za kimarekani 261,000, lakini Mwisho waSiku majibu yalikuja tofauti baada ya FIDDY kushindwa kwa mara ya Kwanza kabisa.

Kwa mujibu wa Kitengo cha Chimbua Chimbua, 50 ameamuliwa na mahakama Kuilipa kampuni hiyo kiasi cha USD Milioni 16.1 kwa Kosa la kutumia Designing ya kampuni hiyo pamoja Baadhi ya Data kutoka katika kampuni Hiyo hiyo, bila taarifa Maalum.

SLEEK AUDIO waliongeza Kuwa, awali walitakiwa kushirikiana na RAPA huyo wa Track ya PILOT, lakini baada ya Kushindwana katika makubaliano yao, walishangaa kuona Designing zao na Vitu vingine vikitumika katika Headphone hizo za 50 CENTS.

Licha ya Kutumia vibaya baadhi ya vitu vyao pasipo makubaliano hasa ya Kifedha, kampuni ya SLEEK AUDIO pia Imesema kuwa 50 na Msaidizi wake, waliiba na Kutumia Baadhi ya maelezo kutoka katika WEBSITE yao Bila idhini yoyote, jambo ambalo ni Kinyume na taratibu za Kibiashara, na ni uharibifu wa Soko lao.


Mpaka hivi sasa, mahakama imemuamuru 50 Cents ambaye jina lake halisi ni JACKSON CURTIS,  kiasi cha USD 11,693,247 kwa ajili ya Uharibifu, pamoja na USD 4,488,331 kama malipo ya Usumbufu kwa Mwanasheria wa SLEEK AUDIO

NEW TRACK: THE LYRICS- Fred Swagg Feat Young Killer "Msodoki" & Kadgo (VERY HOT)

12:41:00 AM Add Comment

MNADA BANNER