REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

ZIMEVUMA….RIHANNA NI MJAMZITO

2:24:00 AM Add Comment

ULALALALALAAAA……
WALA UsijiulizeMaswali Mengi sasa Hivi kuwa baba Wa Mtoto huyo ni nani Kati ya Drake na Chris Brown, lakini acha tukupe Mtonyo wa Dhati kabisaaa hivi sasa.

Kitengo cha CHMBUA CHIMBUA kimeshusha Big report Kuwa kuna Uwezekano mkubwa kabisa, msanii wa POP na R&B kutoka katika Visiwa vya BARBADOS, ROBYN FENTY RIHANNA, Ni Mjamzito.

Taarifa kutoka hizo ambazo RIRI hajazithibitisha, zimetokana na Moja ya Picha ambayo imenaswa hivi majuzi na Mtandao wa MEDIA TAKE OUT, ikionesha Kitumbo cha Rihanna kikiwa kimetuna kidogo, na Wala , siyo shibe ya Chakula.

Aidha mtandao huo ulizidi kusasambua kuwa, riri amepunguza kwa asilimia kubwa Matumizi ya Sigara, Pombe kali, na hata Mmea Korofi wa BANGI, tofauti nna ilivyokuwa Imezoeleka.

Wakati watu bado wazidi kujiuiza kama ni kweli riri ana Ujauzito ama La, Yamezuka maswali mengine ya Kutosha kuwa nani ambaye ni Dady wa Kichanga hicho, kati ya Chris Brown ambaye walitemana Muda 
Kidogo, ama Drake ambaye hivi sasa ana mahusiano naye.


Aidha baada ya Mtandao huo kutoa Picha hiyo ya Kitambi kiduchu cha Mkali Huyo wa MAN DOWN, finally Zimepatikana Picha nyingine akiwa anatokea CLUB huku amevaa vazi kubwa (Tshirt) la Kuficha Kitambi Kisionekane.

Doh !

BIRDMAN AMSHUSHIA NDINGA AINA YA BUGGATI JUSTIN BIEBER..

2:14:00 AM Add Comment

AWALI zilivuma Tu kwamba Huenda Bwana Mdogo JUSTIN BIEBER akapiga Collable na mmoja kati ya Membaz wa kundi la YMCMB, MOHHONE, lkini amini usiamini, TTM tumenyaka zaidi ya hilo.

BAADA Ya Big Bous huyo wa CASH MONEY RECORDS kuweka Picha za kuchora tattoo yake Mpya ya RG (yaani RICH GANG) kunako upande wake wa Shavu la kulia, hatimaye Ameachia Picha ya Ndinga aina ya Buggati , ambayo aliinunua kama zawadi kwaThe Majanga Boy JUSTIN BIEBER.


Aidha ili kuonesha kuwa amevutiwa na zawadi hiyo, Bwana Bieber alichukua time yake Pia Kuonesha BUGATTI hiyo yenye rangi Nyekundu , huku akimshukuru Birdman kwa Kumnunulia Gari aina hiyo, ikiwa ni ya Kwanza


Hii sio mara ya Kwanza kwa Birdman Kumnunulia Msanii yeyote gari kutokana na kukubali kazi yake (msanii husika), bali ameshawahi kumnunulia Lil wayne,  na wengineo ambao hakika anakubaliana nao katika Music industry.

NYOTA NDOGO NA MUSTAPHA COLONEL BADO HAPAKALIKI..

2:10:00 AM Add Comment

LINAWEZA Kuwa Ni Drama lakini kadri linavyozidi kwenda maswali mengi yanazidi kujaa kunako kichwa  Zetu.
Wiki kadhaa Zilizopita, Mustapha Colonel aliomba radhi kwa Nyota Ndogo na baadhi ya Wanawake ambao waliitisha maandamano kwa ajili ya Kumpinga Mustapha na Uzalilishaji wake wa kupiga Picha za Nusu utupu na Huddah

Lakini hali baada ya Kudhaniwa kuwa imeisha, limezuka linguine tena baada ya Nyota Ndogo kumtolea Uvivu ya MUSTAPHA Kudai kuwa, aliamua Kufanya hivyo, yaani kumuomba Radhi Nyota Ndogo , ili kuepusha kuvunjika kwa Ndoa ya Star Huyo aliyehit na WATU NA VIATU.


Aidha wakati akipiga Story kunako Moja ya interview Nchini Kenya Hivi karibuni, MUSTAPHA aliyevuma na Kwaju la MTAANI.COM, alidai kuwa, kuna kubwa zaidi lililopo baina yake yeye na Nyota Ndogo, tofauti na Zile Picha alizopiga na Huddah, lakini anamstahi kwa Sababu hataki Kuivunja Ndoa yake.

Sasa TTM imenyaka Majibu Kutoka Kwa Nyota Ndogo ambaye alijibu Hivi..TUNAMNUKUU

 “Nimekua kimya toka mustafa alivyo omba msamaha. kwanini?kwakuwa shida yangu ilikua aombe msamaha story kwisha. lakini chakushangaza ni kuona huyu babu bado anatafuta mengine. eti hataki kuvunja ndoa ya mtu? Mwambie avunje tuone kama wacha kuvunjika, kama tu itabambuka.


Pia anasema kuwa kuna kitu na taka kwake. jamani mbona anajivuta vuta hivi kama shoga? ni aseme anachofikiria nataka kwake. sijakataa watu wameniita nyanya. sasa wamwambie babu yao awache maneno.maneno tulimaliza tu alipoomba msamaha. Mimi nimekuwa kimya, na yeye anatafta story kutoka kwangu.”

LUDACRIS AKUTANA NA MKOSI MWINGINE TENA.

1:59:00 AM Add Comment

LUDA CRISS safari Hii amekumbana na Misukosuko Mikali ambayo huenda ikamfanya akapata athari hasa Kisaikolojia, endapo hatokuwa makini.

Miezi kadhaa iliyopita, rapper Huyo kutoka ATLANTA alifunguliwa mashtaka na Mzazi mwenzake, TAMIKA FULLER, kwa madai ya kushindwa kumhudumia mtoto wao ambaye walikubaliana kumpatia Kiasi kadhaa cha fedha kwa ajili ya matumizi mbali mbali.

Lakini katika Utetezi wake, Ludda alidai kuwa hakuwa Vizuri kifedha, baada ya Kifo cha Paul walker kusitisha Zoezi la Utengenezwaji wa Filamu ya FAST AND FURIOUS 7 , aliyokuwa akiitegemea kwa hali na Mali.

Sasa, hivi majuzi TTM tumezinyaka Kuwa, Hitmaker huyo wa WHAT THEM GAL WANTS alifungua mashtaka Dhidi ya Mzazi Mwenzake huyo, kwa kuvujisha Nyaraka za Mahakama ambazo Kimsingi hazikutakiwa kufikishwa katika mitandao mbali mbali ya kijamii kama ambavyo iliamriwa na Mahakama.

Kwa mujibu wa madai ya LUDA akiwa mahakamani, alisema kuwa, TAMIKA alivujisha Nyaraka Hizo katika Mtandao wa Kidaku zaidi nchini marekani, MEDIA TAKE OUT.COM, na Ushahidi alikuwa nao kabisa.

Baada ya Hakimu kupitia Ushaihidi huo, bado alipiga Chini madai ya Luda katika mahakama hiyo ya FULTON COUNTY, huku akimuamuru Luda Kumlipa Mwanasheria Wa TAMIKA kwa usumbufu aliousababisha.

MNADA BANNER