REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

OH MY GOD...TUNAOMBA LISIWE BIFU JIPYA KATI YA HEMED NA SHETTA

7:10:00 AM Add Comment

BLACK TOUCHEZ/BONGO 5/ Hemed Twitter account
Ni Possible Kabisa “Baba Kayla” –SHETTA akaingia kunako Kutokuelewana na Baadhi ya wasanii, baada ya kuachia Kauli kuwa, safari hii, hatohitaji kufanya “Collable” na Msanii yeyote wa Ndani (Yaani Bongo), ili atanue Wigo wake…

Kwanini Tunasema hivyo, sababu tayari dalili zishaanza kuonekana huku yeye akijitetea kuwa hajaeleweka


HEMEDI PHD AMEFUNGULIA:
Msanii Mwenzake katika Music na Movie, HEMED SULEIMAN “PHD”, amekuwa wa Kwanza kumfungukia “Ex-Mswati” kuhusu that Statement.
Na Hiki Ndicho alichokisema kunako account yake ya Twitter

Oh ! My God!...let this isiwe New Bifu in 255.


“HEMED HAJANIELEWA….”: SHETTA.
Shetta “amefyatuka” na Mtandao wa BONGO 5, na kusema kuwa, Statement yake iliwasilishwa Vibaya na Vyombo vya Habari, kwani yeye alilenga Kutanua wigo wake kimataifa, maana ameshafanya kazi na Baadhi ya wasanii hapa Bongo. Ingawa, kama kuna “Artist” yeyote atahitaji kupiga naye kazi, Milango iko wazi



Pia amesema kuwa, hana tatizo na “PI-HECHI-DII” (hemedi)


SPORTS: MTOTO WA BEKHAM ASAIN MKATABA NA CLUB YA ARSENAL

6:37:00 AM Add Comment

BLACK TOUCHEZ/ DAILY MAIL
MTOTO wa Kwanza wa David Bekham, Brooklyn Bekham ,amesaini Mkataba Wa Muda Mfupi na Academy ya Timu ya Arsenal

Ingawa Awali alikuwa anahitajiwa sana na Club ya Chelsea na Manchester United ambayo Baba ake aliwahi kuchezea, Kinda huyo ambaye ana umri wa Miaka 15, alisaini mkataba baada ya kiwango chake kuwavutia Makocha

Brooklyn amekuwa Mazoezini na The Gunners, na anachezea Club hiyo katika Mechi za “Under 16”, ambapo awali ameshakutana na Club kama Vile Chelsea, Man U, Fulham na Queens Park rangers

Brooklyn atakula Mkataba wa Muda Mrefu endapo Kiwango chake kitavutia haswa katika Mapambano kadhaa na hata Muda wa Mazoezi


Licha ya Kwamba david Beckham alikuwa ni Msukuma kabumbu wa Manchester United na Club Nyinginezo, lakini ana Mapenzi na mahusiano mazuri na Club ya Arsenal







PICHA: ILIVYOKUWA KATIKA MASHINDANO YA MBIO ZA MITUMBWI JIJINI MWANZA

5:35:00 AM Add Comment






G-SENGO BLOG
KIKUNDI cha Wanaume wapiga kasia cha Costantine Lusalage kutoka Sengerema Mkoani Mwanza kimeibuka na ubingwa wa Mkoa wa fainali za kimkoa mbio za mitumbwi chini ya udhamini wa bia ya Balimi Extra Lager zijulikazo kama “Balimi Boat Race 2014” na hivyo kuzawadiwa pesa taslimu Shilingi 900,000/= pamoja na tiketi ya kuwakilisha Mkoa wa Mwanza kwenye fainali za  Kanda zinazotarajiwa kufanyika Desemba 6 mwaka huu jijini Mwanza.

Nafasi ya pili ilichukuliwa na kikundi cha Elisha Jacob kutoka Misungwi ambacho kilizawadiwa pesa taslimu Shilingi 700,000/= pamoja na tiketi ya kuwakilisha mkoa katika fainali za Kanda jijini Mwanza pia, wakati nafasi ya tatu ilichukuliwa na kikundi cha Emmanuel Masanyiwa kutoka Luchelele ambacho kilizawadiwa pesa taslimu Shilingi 500,000/= na nafasi ya nne ilichukuliwa na kikundi cha Daniel Genha kutoka Misungwi ambacho kilizawadiwa Shilingi 400,000/=

Nafasi ya tano hadi ya tisa walipewa kifutajasho cha pesa taslimu Shilingi 250,000/= kila kikundi ambavyo ni kikundi cha Mussa Msalaba kutoka Sengerema, Joseph Jacob kutoka Misungwi, Katula Msese kutoka Kigoto, Faustine Daud kutoka Ibanda, Lubongeja Manyasiwa kutoka Sengerema na Simon Salala kutoka Misungwi.

Upande wa Wanawake kikundi cha Joyce Alon kutoka Misungwi kilifanikiwa kutwaa ubingwa na hivyo kuzawadiwa pesa taslimu Shilingi 700,000/= pamoja na nafasi ya kuwakilisha mkoa katika fainali za Kanda jijini Mwanza. 

Nafasi ya pili Wanawake ilichukuliwa na kikundi cha Tabu Daudi kutoka Misungwi ambao walizawadiwa Shilingi 600,000/=,washindiwa tatu ni kikundi cha Ntabo Hussein kutoka Luchelele ambao walizawadiwa Shilingi 400,000/= na nafasi ya nne ilichukuliwa na kikundi cha Leah William kutoka Misungwi ambao walizawadiwa Shilingi 300,000/= na nafasi ya tano hadi ya kumi walizawadiwa kifuta jasho cha Shilingi 200,000/= kila kikundi ambavyo ni kikundi cha Winifrida William kutoka Misungwi, Revina Magafu kutoka Kigoto, Anna Elias kutoka Kigoto, Moshi Maji kutoka Kigoto, Kizuka Kapani kutoka Bwiru na Robby Mwita kutoka Mwaloni.

Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi Meneja wa bia ya Balimi Extra Lager, Edith Bebwa  kwanza alishukuru vikundi vyote vilivyojitokeza kushirika mashindano hayo lakini pia aliwapongeza wale wote waliofanikiwa kupata zawadi na kuwaomba waliofanikiwa kupata nafasi ya kuwakilisha Mkoa wa Mwanza kwenye fainali za Kanda wafanye mazoezi ya kutosha na mwisho wasiku ushindi ubaki Mwanza kwa mwaka 2014.

Edith alisema washiriki wote mliofanikiwa kupata zawadi mkatumie vizuri hizo pesa kwa maendeleo yenu na pamoja na maadalizi ya mashindano mengine mwaka ujao.

Fainaliza Kanda zambio za mitumbwi zijulikanazo kama “Balimi Boat Race 2014” zinatarajiwa kufanyika Desemba 6, mwaka huu jijini Mwanza katika ufukwe wa Mwaloni.


WHAT?..RIHANNA NDANI YA WHITE HOUSE?..NA KITENGE?

4:06:00 AM Add Comment




Thank You Bad Gal Riri kwa kufanya hiki kitamu.

 Siku ya Jana Rihanna alikuwa katika “White House” ya Nchini Marekani, na Hivi ndivyo alivyong’aa..
Kiafrika zaidi..Noma

CHECK PICHA HIZO 






DEEJAY VICTOR WELCOMES A NEW BABY BOY

3:58:00 AM Add Comment
PROUDLY FATHER: Deejay Victor "Blessed Hands" amekaribisha Mtoto wa Kiume katika Familia Yake


BLACK TOUCHEZ, Mwanza
DEEJAY wa Kituo cha Redio cha METRO (METRO FM-99.4 MHz,) Kilichopo Jijini Mwanza, VICTOR STANLEY “DeeJay Victor” amekaribisha Mtoto wa Pili Wa Kiume Katika familia yake, Siku ya Jana
 
WELCOME TO THE WORLD: Mtoto aliyekaribishwa Katika familia ya Deejay Victor
DJ Victor ambaye pia hufanya Kazi zake CLUB FUSION iliyoko Jijini Mwanza, ameonesha Furaha yake Pia Kupitia Account yake ya Facebook, ambako amepost Picha ya Mtoto Huyo (Jina Hatujalinyaka Bado)

Tofauti na Mtoto Huyo, Dj Victor ana Mtoto wa Kiume Mwingine KELVIN, ambaye ni Mtukutu na hupenda kupita Njia za baba yake hasa katika “Turn Table”
 
I'M A BROTHER NOW:Kelvin, Mtoto wa Kwanza wa Deejay Victor
BLACK TOUCHEZ inampongeza Deejay Victor na Mkewe kwa Kumleta Deejay Mpya katika Ulimwengu huu

MNADA BANNER