REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

NEW VIDEO : SNURA in "SHOGA AKE MAMA"

9:18:00 AM Add Comment

Nah Aboud Jr.
IKO HIVI MAZEE.....
Finaly ile Video mpya iliyokuwa ikizungumziwa kwa saaaaana na Mkali wa FILAMU hapa Area 255, SNURA, Hivi sasa Iko Tayari.
Kwa Mujibu wa Dar Talk, Snura amesema Video Hiyo itakayokwenda kwa jina la "Shonga ake Mama", itaanza Kuonekana Muda Si Mrefu.

TIRIRIKA MAMA...
"Video imetoka sasa, na Mashabiki wangu wataiona muda si Mrefu. Kikubwa Malengo yangu ni kufanya kitu tofauti, na Baada ya kazi Hiyo kwenda hewani, nitaanza show za Kuitambulisha ili iweze kupokelewa Vizuri"

DAR EXPRESS NUSURA IPATE AJALI CHALINZE

9:05:00 AM Add Comment



Na Nah Aboud Jr, Morogoro


Basi la Dar Express lililokuwa likitoka Dar es Salaam kwenda mkoani Arusha limenusurika kuanguka baada ya kuacha njia na kugonga ukingo wa barabara ya Chalinze, Segera kama linavyoonekana katika picha


SOURCE : Wavuti.com

MISRI YAAHIDI KUTANGAZA VIVUTIO VYA KITALII VYA TANZANIA

2:37:00 AM Add Comment



Marwa Tawfik (Kulia) mmoja wa wajumbe waliowakilisha vyombo vya habari nchini Misri kuja Tanzania kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii akifafanua jambo kwa wajumbe wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya kile walichojionea walipofanya ziara katika vivutio mbalimbali vya utalii Tanzania Bara na Zanzibar.Wengine ni baadhi ya wawakilishi kutoka Misri.
                                              **************************************************
DAR ES SALAAM
VYOMBO vya habari nchini Misri vimeahidi kutangaza vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo nchini katika kuhakikisha Tanzania inapata watalii wengi zaidi jambo litakaloendelea kudumisha mahusiano mema yaliyopo kati ya nchi hizo.



Hayo yalisema Dar es Salaam juzi na mmoja wa wawakilishi wa vyombo vya habari nchini Misri, Marwa Tawfik alipozungumzia ziara waliyofanya katika vivutio vya utalii nchini ambapo waliahidi kutumia vyombo vyao kutangaza walivyoviona.



Ujumbe wa watu sita uliowakilisha vyombo mbalimbali vya habari nchini Misri yakiwemo magazeti na televisheni chini ya Ofisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini humo Jestas Nyamanga walifanya ziara ya siku tano nchini kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii Tanzania Bara na Visiwani chini ya uratibu wa Bodi ya Utalii nchini (TTB).



Alisema wanaporudi nchini kwao watakaa na uongozi wa vyombo vyao na kuangalia jinsi ya kupata vipindi maalumu  katika televisheni na makala katika magazeti jambo litakalowezesha taarifa za utalii za Tanzania kuwafikia watu wengi zaidi nchini mwao na nchi nyingine za ukanda huo.



Tawfik alisema ana imani ziara hiyo pamoja na kazi watakayoifanya ya kuvitangaza vivutio husika itasaidia Tanzania kupata watalii wengi zaidi kutoka nchini mwao na katika nchi za ukanda wa kiarabu. “Tumeona utajiri wa asili wa ajabu uliopo Tanzania,sisi tunaahidi kutumia vyombo vyetu kutangaza vivutio hivi katika kuhakikisha watu wengi zaidi wanahamasika kuja Tanzania na hatimaye kuwaongezea pato lenu kupitia utalii,” alisema Tawfik.



Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TTB Aloyce Nzuki alisema ziara hiyo pamoja na nyingine ni muendelezo wa jitihada za bodi hiyo ya kuhakikisha sekta ya utalii inakua ndani na nje ya nchi.



Alisema ujio wa ujumbe huo kutoka Misri utaongeza idadi ya watalii kutoka nchi hiyo pamoja na nyingize za ukanda huo ambapo takwimu za sasa zinaonyesha Tanzania inapata watalii 25,000 kutoka nchi za ukanda huo.



Nzuki alisema pamoja na ujumbe huo kuahidi kutumia vyombo vyao kutangaza walivyoviona pia bodi hiyo inaendelea na jitihada za kuhakikisha matangazo ya vivutio vilivyopo nchini yanawekwa katika lugha ya Kiswahili katika kukuza utalii wa ndani.



“Tumekuwa na jitihada endelevu za kuhakikisha vivutio tulivyonavyo vinajulikana ulimwenguni kote jambo litakalosaidia kupata watalii wengi zaidi kutoka nje lakini pia tunaendelea na jitihada za kuhakikisha utalii wa ndani unakua,” alisema Nzuki.

HII NDIYO SABABU ILIYOSABABISHA DIAMOND PLATNUM KUPATA AJALI MBAYA....

2:12:00 AM Add Comment







Na Frank Magnus Joachim. DSM

FUNGUKA PLATNUM...
"Tarehe 10 ya mwezi wa 11 siku ya juma mosi ni moja ya siku ambazo sitozisahau maishani mwangu.

Baada ya kumaliza majukumu yangu ya kila siku, nilikwenda masaki kumwona mmoja wa jamaa zangu wa karibu nikiwa na Blogger wangu Bestizzo pamoja na mwanafamilkia ya wasafi Dumi(Dancer) Mishale ya saa moja hivi nikiwa maeneo ya masaki karibu na kona ya msasani nilipata ajali ambayo haikuwa kubwa sana ingawa imesababisha uharibifu kwa kiasi kikubwa, Kama mjuavyo barabara ya msasani ni ndogo na gari huwa haziko katika mwendo wa kasi... ghafla dereva wa pikipiki alikatisha mbele yangu na katika kujaribu kumkwepa nikagonga gari ndogo aina ya Rav 4 ambapo ilisababisha dereva wa pikipiki kuanguka katikati ya gari zote mbili. Hiyo ndio hali halisi ya ajali niliyokutana nayo jumamosi iliyopita.

Namshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kutunusuru wote bila majeraha makubwa zaidi ya maumivu tu ya hapa na pale."


MIKWAJU MIPYA

1:39:00 AM Add Comment
TMK WANAUME FAMILY : "Tutaonekanaje"


NIKKI WA PILI, G- NAKO & JOH MAKINI : "Niache Kidogo"

Itafute Haraka Upate Radha Matata..

MTOTO ALIYEFANYIWA UKATILI NA MAMA YAKE MDOGO NA KULAZIMISHWA KULA KINYESI CHAKE...AKATWA MKONO

1:22:00 AM Add Comment





Na Nah Aboud Jr, 
MAJENGO,MBEYA

HALI IKO HIVI.......


MTOTO aliyejulikana kwa jina moja la Aneth (pichani) anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka miwili, mkazi wa eneo la Majengo Kaskazini jijini Mbeya ameunguzwa vibaya mwili wake na kulazimishwa kula kinyesi na Mama yake Mdogo aliyejitambulisha kwa jina la Revina.

Tukio hilo la kikatili liligundulika juzi eneo hilo majira ya saa tano asubuhi ambapo mwandishi wa habari hizi alifika eneo la tukio na kuukuta umati wa watu na mtuhumiwa akimuogesha mtoto huyo.

 MTOTO MWENYEWE ANSEMAJE?
Mtoto huyo alipoulizwa kuwa ilikuwaje, aliongea kwa woga akisema kuwa alikuwa amefungwa mkono na kumwagiwa maji na kupigwa.

 DAH....MAMA MDOGO ALIYEFANYA UKATILI HUO NAYE AKAWA HIVI
Mtuhumiwa huyo alipohojiwa alikataa kusema chochote na kuishia kutaja jina lake moja la Revina, kisha wananchi wakaamua kumchukua mtoto huyo na mtuhumiwa na kuwapeleka kituo cha Polisi cha Kati.

 MASHUHUDA JE?
Mashuhuda wa tukio hilo walisema kuwa baada ya kutomuona mtoto huyo mwenye historia ya kuteswa na mama yake huyo mdogo anayeelezwa kuwa mama yake mzazi, Bahati Mkandara alifariki, wakaamua kumuuliza binti huyo ambapo aliwajibu kuwa mtoto huyo alikuwa kucheza na walipompiga ndipo akaamua kukimbilia chumbani na walipoingia wakamkuta mtoto amesimama akiwa uchi.

 SERIKALI IKO WAPI?.....
Kwa upande wake, Mwenyekiti  wa Mtaa wa Majengo Kaskazini, Shack Mwakanyamale alisema kuwa binti huyo amezoea kumtesa mtoto huyo huku mtoto wake akiwa na afya njema ambapo aliwatuliza wananchi wenye hasira kali na kuongoza msafara wa kumpeleka katika kituo cha polisi mtuhumiwa huyo.

MNADA BANNER