REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

TUMIENI AKILI NYIE: FLOYD MAYWEATHER ALIVYOCHARUKA BAADA YA MWANAE KUSHIKA NAFASI YA PILI

2:55:00 AM Add Comment

BWANA, wanasemaga Uchungu wa Mwana aujuaye ni Mzazi, na hiki ndicho ambacho Floyd Kakionesha kwa Mwanae wa Kike aisee.

Bondia Huyo ambaye ana mkwanja Mrefu sana,  alijikuta akitibuana Vikali na majaji ambao walikuwa wanasimamia Shindano la Watoto wa Kike Kucheza, linalofahamika kama CHEERS DANCE COMPETITION, baada ya Team ya Mtoto wake wa Kike mwenye miaka 12 kushinda katika Nafasi ya Pili.

Katika Tukio hilo ambalo liligharimu majibishano ya takriban dakika zaidi ya 5, Floyd Mayweather Jr alikuwa akihitaji ufafanuzi wa kwanini Team ya Mtoto wake iliyoonekana kufanya Vizuri na kukubalika ilinyimwa Ushindi wa Juu na Badala yake wakapewa watu wengine


Ingawa majaji walijitahidi kufafanua, Bado Floyd alikuwa ni Mwingi wa Jazba na kuhoji vitu vingi sana, lakini jambo Jema hakuna aliyerusha wala kurushiwa Ngumi

KAMPUNI YA BLING BLING : T.I ACHA MBWEMBWE, LIPA MKWANJA WETU

2:41:00 AM Add Comment

Na Baba Juti
KAMPUNI inayojishughulisha na Biashara ya Vito vya Thamani a.k.a “Bling Bling”, imeamua kumburuza Mahakamani Rapper T.I ili awalipe mkwanja wao wa Takriban USD Million 1 sawa na Tshs 2,285,000,000.

Kwa Mujibu wa Mashtaka hayo, Kampuni hiyo inadai kuwa T.I mnamo Mwaka 2015, alikiuka Masharti ya Mkataba wao ambao walikuwa wamekubaliana kibiashara, huku mara ya Mwisho akichukua Bling Bling zenye thamani ya USD 75,000 sawa na Tsh 171,375,000

Ingawa T.I alionekana kukana Mashtaka na Madai hayo kutoka kwa Kampuni hiyo, wao wanadai kuwa walikuwa wakimuuzia T.I Vito vya thamani vingi sana na vilivyowagharimu kwa asilimia kubwa. Biashara hiyo ilianza Mwaka 2004 mpaka 2012 ikiwemo Chain, Saa,Dog Tags za Diamonds.

Tofauti na hivyo, T.I anatuhumiwa pia kuchukua Vito vya thamani vya Diamonds kwa ajili ya Mwanamke, ingawa hatujui kama ilikuwa ni kwa ajili ya mkewe ama Lah


Kampuni hiyo ya Madini inaongeza kuwa, Awali T.I alikuwa akiwalipa Vizuri tu kupitia Open Account ambayo walikuwa nayo, lakini ghafla alistop kufanya malipo Mwaka 2013


Na Mmiliki wa Kampuni hiyo, FEYZ AYDIN anadai kuwa, alijitahidi kwa kila mali kumkumbusha T.I kulipa Mkwanja wao, lakini hakukuwa na Mafanikio, na Ndipo walipoamua kufungua Mashtaka Dhidi yake

RICK ROSS: YUKO SALAMA KABISA

2:36:00 AM Add Comment

BWANA, sijui Yule Mlengwa atajiskiaje lakini Tayari ndo mahakama imeshaamua aisee
Hatimaye Siku ya Jana ilikuwa ni Siku Nzuri sana kwa Rick Ross a.k.a Rozay ambaye ni Big Boss wa MMG, baada ya Mashtaka yake ya KUTEKA, KUTISHIA KUUA na KUJERUHI kufutwa Rasmi.

Mashtaka hayo alikutana nayo katika Tukio ambalo limtokea kipindi cha Nyuma kidogo kwa Kumpiga, Kumjeruhi na kumteka Mfanyakazi wake wa Bustani ambaye baadaye ilimlazimu afungue Kesi mahakamani

Tukio hilo Pia lilimfanya Rick Ross akane nyuma ya Nondo kwa Week Nzima na kulipa Faini ya USD  10,000 sawa na 22,800,000 za Kitanzania tukio ambalo lilitokea Mwaka 2015 kule ATL


Lakini Baada ya Hakimu kusema kuwa, Rozzay amefanya matukio hayo kwa Mara ya Kwanza, basi anaweza kufuta Makosa yake yote endapo atashusha Mkwanja aliotajiwa

MNADA BANNER