REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

CHAMELEONE KUBONGA NA WANA-MWANZA LEO PALE CCM KIRUMBA

4:18:00 AM Add Comment

The Badder Than Anybody katika Music Industry Barani Africa akiwakilisha UGANDA, Dr.Jose Chameleone, anataraji "KUZIMA" Rock City Nzima (Mwanza ) Leo Katika TUBONGE CONCERT itakayoshushwa Leo DECEMBER 24.
Mpaka Kufikia Hivi sasa, Chameleone Yuko Mwanza na Hizi ni Picha tofauti wakati Chameleone alipoongea na Vyombo Vya Habari Hapa hapa Jijini Mwanza











NONINI ANATAKIWA KUOKOKA:

12:11:00 AM Add Comment



Ushalalalaaa….Ukisikia Dawa Imepata Mgonjwa basi Ndo Hii hapa..
All The way kutoka Nchini yenye Area Code za 254, Kenya, Nonini ametakiwa Kuokoka ili Maisha yake yaende Vizuri na kumtumikia Mungu..CAN YOU BELIEVE THIS?

Sasa Iko Hivi, Mkongwe wa Muziki wa kizazi kipya nchini Kenya ambaye kwa Hivi sasa ameokoka, BAMBOO jana ametoa kali baada ya kutamka mbele ya Kipaza akimshauri NONINI aokoke na aachane na Muziki wa Kidunia ambao unaonekana kutokuwa na Faida yoyote ukizingatia unaaminika kuwa unamuweka Mbali Msanii na Mwenyezi Mungu.

Tofauti na Hilo, BAMBOO ambaye ametimiza Miezi Minne sasa akiwa ameokoka na huku akiandamwa na maneno ya hapa na pale kutokana na kauli zake za hapa na pale kuhusu muziki aliokuwa akiufanya, pamoja na kujitenga na rafiki zake wa Awali kisa hawajaokoka, pia alifunguka na kusema kuwa kwa hivi sasa amewanyamazisha Wanafiki Wake wanaomchukia, na ameachana kabisa na Muziki wa Kidunia.

Tofauti na hayo, kama ulikuwa hujui, Bamboo kwa hivi sasa Pia amebadilisha Jina lake ambalo Tumekuwa tukilizoea siku zote, kwa maana hiyo sasa Hivi ataitwa ABRAHAM,

AVRIL: SIJAMPENDEA PESA JAMANI

12:03:00 AM Add Comment



Wakati Marya akisema kuwa yuko In love na Mtu ambaye hajamtambulisha rasmi, Finally Track mate wake AVRIL Amechumbiwa rasmi.

Avril ambaye alifanya kweli kunako Trak ya Chokoza na track yake ya HAKUNA KAMA YULE (MISSING YOU), hivi sasa amechumbiwa na Mfanya Biashara Mkubwa na tajiri Nchini Afrika .

Lakini baada ya wiki kadhaa kupita, kumekuwa na Stori nyingi kwa Mitaa kuwa Avril amefuata Mkwanja a.k.a Chapaa kwa Jamaa huyo, jambo amvbalo Avril amelikanusha Vikali kupita maelezo.


Katika Kujibu Shutuma hizo, Avril amedai kuwa, amefahamiana na Mchumba wake huyo kwa Muda mrefu, na kama angekuwa amependa Mkwanja kwa jamaa huyo, basi angekuwa anaendesha RANGE ROVER.

Tofauti na hayo, Avril hakusita kuzungumzia Mpango wa Pilau na Dua, yaani Ndoa, ambapo amedai kuwa, Ndoa haitakuwa mapema Kiasi hicho, maana Ukizingatia Jombaa ni Mzulu na Avril Mwenyewe ni Mkikuyu, kwa mantiki hiyo Masuala ya kimila yanatakiwa kuhusika kwa namna yoyote.

Pia limalizia Kuwa, familia Zote, yaani pande zote mbili zinafahamu Kuhusu uhusiano wao na Mipango ya Ndoa, na kwa hivi sasa yeye na mchumba wake wako MOMBASA wanajiandaa kula bata za Christmass, na baada ya hapo watakwea Tank mpaka Kwa Mzee madiba, SOUTH AFRIKA, kwaajili ya Bata za Mwaka Mpya.

MNADA BANNER