REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

BT NEW HIT: MADEE FEAT. P.UNIT- POMBE YANGU REMIX

11:50:00 PM Add Comment

LIcha ya Kukandiwa Sana Kuhusu VIDEO ya POMBE YANGU ambayo Ilifanywa na OGOPA VIDEOZ Nchini Kenya, Kuwa Mbovu na Haina Mvuto, Madee alisema Yeye hatokoma kufanya kazi Nchini Humo, na alisema Atawaziba Vidomo domo wale Wote wasiopenda Mafanikio yake.

Baada ya Wengi Kusubiri Nini Kitafuata, Huu Ndio Mkwaju ambao Binafsi TTM tumelipitisha Asilimia 1000

BT NEW HIT: P.SQUARE- TEST THE MONEY (TESTIMONY)

11:31:00 PM Add Comment

Baada ya Kufanya Vizuri Kupitia PERSONALY, na Hata ALINGO, Finally Twin Brothers, PETER NA PAUL OKOYE, Maarufu kama P.SQUARE, wameachia rasmi Track yao Mpya Hiyo, ya TEST THE MONEY, au TESTIMONY

BT NEW TRACK: BEN PAUL-UNANICHORA

11:09:00 PM Add Comment

TOfauti na Wasanii Wengine, BEN PAUL ameamua Kuachia Track yake Mpya ya Unanichora, sambamba na ALBAM yenye Nyimbo 20. Albamu hiyo haitauzwa Kama Ambavyo Imezoeleka,bali Itauzwa na kununuliwa kwa Njia Ya Mtandao.

ALBAM hiyo itapatikana katika Mitandao ya XBOX,BEAT  MUSIC,SHAZAM,SPOTFY na GOOGLE PLAY.

THE WAY TO VALENTINE: CINDY ATEMANA NA MUMEWE..YAANI YUKO SINGLE

12:36:00 AM Add Comment

INAWEZA Kukupa Utata Kidogo Ukizingatia Tumebakiza Siku kama Mbili tu Kufurahia Valentine day, lakini It is What It Is.

The Sexy Singer kutoka Nchini Uganda, CINDY SANYU, amethibitisha Kutemana na aliyekuwa Mme wake MARIO BRUNETTE, Kupitia Mtandao wa FACEBOOK.

Ili Kuthibitisha Hilo, KITENGO CHIMBUA CHIMBUA cha TTM, kilitembelea Ukurasa wa CINDY, ambako kulipatikana POST ambayo Ilitafsirika Kwa Lugha Ya Kiswahili kama Hivi “SIJUI NAMNA YA KUSEMA HILI, HIVYO NITALISEMA TU. NIKO SINGLE KWA MARA NYINGINE”

Cindy ambaye Pia Ni Ex-Member wa BLUE 3, alifikia hatua hiyo, Huku aliyekuwa mumewe huyo, MARIO, ambaye ni Mfanyabiashara Mkubwa nchini Uganda akimlaumu kwa hali ya Juu.

Mario alisema Kuwa, CINDY ambaye aliteka EAST AFRICA nzima na Kwaju lake la NA WEWE, amekuwa akileta Suala la Umaarufu katika Ndoa yake, jambo ambalo limekuwa ni Usumbufu Mkubwa Katika Mahusiano yao, na kusababisha kuvunjika Kwa Ndoa yao .

Akizungumza kwa Hisia Zote. Mario alinukuliwa akisema, Mwanaume Ni  Mwanaume katika Ndoa, ingawa Ni lazima Aiheshimu Ndoa Yake na familia yake Kiujumla. Licha ya Kwamba CINDY ni maarufu sana, alitakiwa Kuniheshimu, sababu mimi ni Mumewe”.


Mario na Cindy wameachana rasmi na Hivi sasa kila mmoja ana Maisha yake, ingawa bado Jamaa anamlaumu sana Mkewe kwa Kuwa chanzo cha Kuvunjika Kwa Ndoa yao.

ON THE WAY TO VALENTINE: T.I AMTOLEA UVIVU MKE WAKE TINNY BAADA YA KUPOST PICHA TATANISHI KATIKA INSTAGRAM

12:21:00 AM Add Comment

WAY  TO VALENTINE DAY inamengi sana kama ulikuwa hujui, alkini Inabidi tukubali tu kwamba lazima Mengi yatokee.

RAPA T.I Kutoka Nchini MAREKANI, amemtolea Uvivu Mke wake wa Muda mrefu sasa, TINNY, baada ya Kupost Picha ya MAKALIO yake katika Account yake ya INSTAGRAM.

Tofauti na Kuhisi kuwa labda T.I angempigia Simu Mkewe huyo na Kumpasukia kuhusu Hilo, Badala yake T.I aliamua Kupost Comment  ambayo ilimuambia Kuwa, TINNY anamabo mengi ya Kufanya Kuliko Kupost Picha ya makalio yake, ingawa Picha Ni Nzuri na Amependeza.


Baada ya Kuona Comment hiyo, KITENGO CHIMBUA CHIMBUA Kilisikilizia Jibu kutoka Kwa Tinny ambaye Jina lake halisi ni TAMEKA  COTTLE.

Lakini kama Tulijua, baadaye Mwanamama TINNY alijibu Comment ya T.I na Kusema Kuwa Dhamira yake haikuwa Kuonesha WEZERE Yake, bali alidhamiria Kuonesha Kiuno yake aliyobarikiwa na Mungu, huku katika Kiuno Hiyo Kukiwa na TATOO ambayo Kwa fasta TTM hatukujua ilimaanisha Nini.


TINNY na TI, wamekuwa katika mahusiano kwa Muda Mrefu, Kuanzia Mwaka 2001, na hatimaye waliweza Kufunga Ndoa  JULAI 30, 2010, Huko MIAMI BEACH, FLORIDA.


Mpaka Hivi wawili hao wameweza kupata watoto ambao Ni Clifford "King" Joseph Harris III,aliyezaliwa August 25, 2004, na Major Philant Harris, aliyezaliwa May 16, 2008, Ingawa T.I ana watoto Wengine Nje ya Ndoa hiyo

THINGS ARE GETTING BIGGER: HATIMAYE ASHANTI AMEACHIA LIST YA ALBAMU YAKE.

12:15:00 AM Add Comment

Wiki Kadhaa Zilizopita TTM Tulikupa Mtonyo wa Uhakika Kuwa The Kept Silence Singer , ASHANTI, anarudi rasmi Kwenye Gemu na ALBAMU ambayo Mwenyewe anaiaminia balaa.

Sasa, baada ya Kuchelewa kwingi, Huku COVER ya Albam Hiyo ya BRAVEHEART ikibadilishwa Mara Kadhaa, finally Mikwaju 13 ambayo itapatikana katika ALBAM Hiyo imeachiwa Rasmi

ALBAM Hiyo ambayo Itahusisha Kwaju la I GOT IT ambalo amemshirikisha RICK ROZAY, Itashushwa SOKONI Rasmi MARCH 04 Mwaka Huu, huku Vichwa Vingine vikali akiwemo FRENCH MONTANA, JEREMIAH, na BENIE MAN, wakionesha Ushirikiano wa hali ya balaa

Aidha Video ya I GOT IT hivi sasa Ipo katika Mchakato wa Kukamilika, baada ya Ashanti Mwenyewe Pia Kuachia Baadhi ya PICHA za BEHIND THE SCENE

TRACK LIST
1. Intro/Braveheart
2. Nowhere
3. Runaway
4. Count
5. Early In The Morning (Feat. French Montana)
6. 3 Words
7. Love Games (Feat. Jeremih)
8. Scars
9. Never Should Have
10. She Can’t
11. Don’t Tell Me No
12. I Got It (Feat. Rick Ross)
13. First Real Love (Feat. Beenie Man)/Outro

Target bonus songs:
1. Bonafide Survivor

2. RIP

MNADA BANNER