REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

NEW VIDEO: RICK ROSS FEAT. FRENCH MONTANAH & P.DIDDY

11:17:00 PM Add Comment

DRAKE NI MWANAUME PEKEE KWA RIHANNA

6:57:00 AM Add Comment

DREEZY Drake anaweza kuwa moja kati ya Furaha kubwa sana aliyo nayo ROBIN FENTY –RIHANNA hivi sasa….

Kupitia Mtandao wa Hollywoodlife, chanzo Kimoja kimebaini kuwa, Dreezy ni mtu ambaye anampa raha zaidi Rihanna hivi sasa, tangia ametemana na Ex Boy Friend wake CHRIS BROWN

Aidha Chanzo hicho kimezidi kuvujisha kuwa, Dreeezy ambaye ana umri wa Miaka 27, amekuwa akifanya Hivyo sababu anajua Kile ambacho Rihanna mwenye Miaka 26 amepitia na hata kukumbana nacho wakati yuko katika mahusiano na Chris brown

Pia inasemekana kuwa, Drake amekuiwa akifanya Vitu mbali mbali ambavyo vinamfanya Rihana aione Thamani yake hasa katika Ulimwengu wa kupendwa, maana amekuwa naye karibu sana, na amejitahidi kumfurahisha kupitia Mishe mbali mbali ambazo ni sehemu ya kumfanya aondoe Upweke na Stres

Katika kufahamu zaidi, Chanzo hicho kilizidi kutonya kuwa, Drake amekuwa akimheshimu Rihana kuanzia Hisia zake, maisha yake Kiujumla, pamoja na kuweka uelewa Mkubwa sana katika kazi yake ya Muziki.

Lakini kama ulikuwa hujui, TTM tunakupa hii Exclusively kabisa kuwa, DRAKE, hata Siku moja hamuiti Rihanna jina Lake la STEJIN yaani la Kisanii, ambalo ni Rihanna, bali anamuita Jina lake hal;isi, jambo ambalo linamfanya ajione amethaminiwa kuliko Maelezo

D’BANJ AMETEMWA NA KANYE WEST?

6:43:00 AM Add Comment

The Most Shocking Stuff ni Kwamba Eti kuna uwezekano wa D’Banj kutemwa na Mtu Mzima Kanye West ambaye alikuwa ni Meneja wake katika kazi zake, huku akimpa Support ya kutosha pale GOOD music.

Baada ya Kudaka Mtonyo Huo, TTM tulizama kiundani na kubaini kuwa, D’BANJI ambaye ni Msanii Mkali balaa anayeiwakilisha vema Nchi ya Nigeria, amefuta Details Zote kuhusu Kuwepo GOOD MUSIC katika Account yake ya Twitter, jambo linalotufanya Tujiulize kama Ni kweli , mkali huyu wa FALL IN LOVE ametemana na KANYE WEST ambaye alikuwa kama meneja wake.

Pia Mpaka hivi sasa ambapo Tunaingia Mtamboni, bado D’BANJ hajaweka taarifa yoyote kuhusu Kuwepo ama Kutokuwepo GoodMusic,  na hata katika taarifa zake kunako Mtandao wa Twitter bado hazijakaa sawa kuhusu hilo.

D’Banj alilambishwa Mkataba katika LABEL Hiyo ya GOOD MUSIC inayosimamiwa na Kanye West, mwaka 2011, na amefanikiwa kufanya kazi nzuri ambazo zilimuweka pazuri katika Soko la Muziki ikiwemo OLIVER TWIST na FINALLY ambayo still ina bang huku na kule,…

Tuambie D’banj Kama ndo mambo yameenda MBWADIDI…ama Mapwidida..

JAGUAR NA STL..KUNA KINACHOENDELEA?

6:40:00 AM Add Comment

Unaweza kushangaa ama kustuka lakini Minong’ono ya Chini Chini inayoendelea kutoka kwa Dadaz and Kakaz wa Nchi ya Kenya ni kwamba, kuna uwezekano Kuwa Jaguar na STL, yaani STELLA MWANGI, wanafukuziana katika kukamilisha Mchakato Mzima la Mahusiano ya Kimapenzi…Sssshhhh..Zima ..ni Mtonyo tu ambao ttm tumeudaka..

Kwa Mujibu wa Watafutaji wa Info za mastaa kutoka Nchini Kenya, Inasemakana Kuwa, JAGUAR na STL wamreonekana si zaidi ya mara moja katika maeneo tofauti, ambayo yanadhihirisha kuwa, wawili hao wana jambo ambalo linaendelea.

Kama Sio ishu ya kupiga kazi, basi kuna la zaidi ya hapo, maana Tangia STL arudi Nchini Kenya kutokea Norway, inasemekana eti ameahirisha Safari ya Kurudi Norway Kisa jaguar.


Aidha Mtonyo Mwingine ukakazia kuwa, wawili hao walionekana Jumapili iliyopita, Usiku, wakiwa pamoja na baadhi ya wasanii Nchini Uganda, na ikasemekana tena kuwa, JAGUAR ambaye hivi sasa anakuna Kiu ya Burudani na Kwaju lake la KIOO, amemshawish STL kuongeza Siku za Kubaki 254 Kenya, na atamgharamikia safari ya kurudi Norway

VIDEO YA KATY PERRY NDANI YA MSALA

6:38:00 AM Add Comment

WAKISEMAGA WAACHE WAFANYE WANACHOKITAKA mi huwa nakaa Kimya kabisaaaaa

Video ya Wimbo wa KATTY PERRY inayoitwa DARK HOUSE imeingia katika Msala wa Kibaba baada ya Taasisi ya Dini ya Kiislam Nchini Uingereza

Kwa Mujibu wa Uchimbuzi waKitengo cha Chimbua Maovu, TTM tumebaini kuwa TAASISI hiyo inayofahamika kwa jina la SHAZAD IQBAL, wametaka Video hiyo iondolewe katika Mtandao wa Kuuzisha Sura video za watu, wa YOUTUBE, kwa Madai kuwa Inamkashifu Mwenyezi Mungu 

Aidha katika kukazia zaidi, Taasisi hiyo imedai kuwa, kipande ambacho kinapatikana ndani ya NINGA HILO la katty Perry, kinalomuonesha Mtu akiwa amevaa Cheni iliyoandikwa Jina ALLAH yaani MUNGU, wazungu wanavunja yai kwa Kusema ALMIGHT GOD, halafu akashindwa na Nguvu za Giza za KATTY PERRY, zinaonesha kuidhihirisha sana Dini hiyo ya Kiislam na hata kuidharirisha Heshima ya Mwenyezi Mungu


Taasisi hiyo ambayo tayari imeshakusanya sahihi 40,000 za kusitisha Video hiyo na kuiondoa Youtube, imedai kuwa wanaamini Video hiyo itatolewa YOUTUBE kama walivyoomba, na kitendo kama hicho hakisameheki kwa Mwenyezi Mungu, na wala hakivumiliki…

MNADA BANNER