REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

DULLY HAKUKAA KIMYA

12:12:00 PM Add Comment
Matukio ya Kulawiti yamekuwa Ndiyo "Habari Ya Mujini" tangia tumeuanza Mwaka mpya wa 2013, ambapo hivi jana tu, Wanafunzi wa IFM nao walipandisha Munkari na Kuandamana huku source kubwa ikiwa ni wanafunzi wenzao wawili kulawitiwa, na Jana Jamaa mmoja Morogoro amekula "Kifinyo" cha Hatari baada ya Kumlawiti Mtoto.

Msanii Dully Sykes ambaye jamaa wake wa karibu na Baunsa Wake Alafati Ngumi Jiwe anakabiliwa na Kesi ya Kumlawiti Mtoto Mdogo, ameomba Radhi kuhusiana na Tukio hilo.
 Alifunguka kama Ifuatavyo

"Yaani imeniuma sana baada ya kupata taarifa hizi za Arafat Ngumi Jiwe, ingawa sijui kama ni za Ukweli au Lah. Lakini mbali na hyao ni habari chafu ambazo zinaweza kunichafua hata mimi, kwa sababu huyo ni jamaa yangu wa Karibu. Kitendo hicho cha kulawiti mtoto na mimi nikiwa kama baba, kinanigusa kwa uchungu sana, na kama ni kweli, sheria itachukua mkondo wake ili kudhibiti uchafu huo"

PICHA :NEY ALIPENDELEA MAKABULINI

12:01:00 PM Add Comment



Kama ambavyo unamuona, Hii ni Location ya Makabulini ambayo Msanii Nay wa Mitego alikuwa akitengeneza Video yake mpya ya "Wamenichokoza".

NA SISI TUMELETA MAONI KATIKA KATIBA MPYA

5:53:00 AM Add Comment
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Jospeh Warioba (kulia) akiongea na Mawaziri leo  katika ukumbi wa ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dar es Salaam katika mkutano uliolenga kupata maoni ya Mawaziri kuhusu Katiba Mpya.picha na Tume ya katiba mpya

HATIMAYE : Rais Mwai Kibaki atia Saini Mswada wa Malipo na Marupurupu

5:48:00 AM 1 Comment

Rais Wa Kenya , Mwai Kibaki. (Picha na Maktaba)
RAIS Mwai Kibaki ametia saini mswada unaompa malipo ya kima cha shilingi milioni 25 na marupurupu ya shilingi milioni moja kila mwezi baada ya kustaafu.
Mswada huo ni miongoni mwa miswada 30 iliyotiwa sahini na kiongozi huyo wa taifa, kuwa sheria, saa chache baada ya kufanyika maandamano ya kumtaka kutotia saini mswada unaowapa wabunge mlipo ya kiinua mgongo cha mabilioni ya pesa.

Hata hivyo, rais Kibaki HAKUTIA saini miswaada inayowapa waziri mkuu, makamu wa rais, jaji mkuu na maafisa wengine wa serikali malipo ya pindi wanapostaafu.

Mapema jumatatu, mashirika ya kijamii yaliandaa maandamano katikati ya jiji la Nairobi wakimtaka rais kutotia saini mswaada ambao ungewapa wabunge kiinua mgongo cha shilingi milioni 9.3 kila mmoja pamoja na marupurupu mengine.

BALAA : NGUO YA LADY GAGA ILICHANIKA HIVI AKIWA JUKWAANI..

5:30:00 AM Add Comment


Iko Hivi
Mwanadada huyu mkali wa Muziki wa Pop, alikutana na "Msala" huu alipokuwa katika Moja ya Maonesho yake, mitaa ya kunako Vancouver, Canada.

Hali hii iliwafanya mashabiki wote waliohudhuria katika Onesho hilo ijumaa ilopita, kula bonge moja la "deo" la kibaba bila Malipo baada ya Nguo hiyo kuachia bin kutatuka alipokuwa aitupia Swaggz na Mbwembwe zake pale kwa Stage...BRAAAH

MNADA BANNER