REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

BUNGE LA SOMALIA KUAMUA MBIVU NA MBICHI

2:58:00 PM Add Comment


Na Frank M Joachim

Bunge la Somalia leo linapiga kura ya kumchagua rais katika uchaguzi ambao umetajwa na Umoja wa Mataifa kuwa ni wa kihistoria.

 Uchaguzi huo wa rais ambao umeakhirishwa mara kadhaa umetajwa kuwa na umuhimu mkubwa na ambao utafungua ukurasa mpya wa kisiasa katika nchi hiyo ya Pembe ya afrika.

Balozi Augustine Mahiga mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa, uchaguzi huo ni wa kihistoria na una umuhimu mkubwa katika kusukuma mbele juhudi za kuunda serikali mpya katika nchi hiyo iliyoharibiwa vibaya na vita.

 Wawakilishi wa Bunge jipya la Somalia ambao wamechaguliwa siku chache zilizopita kutoka makundi kadhaa ya nchi hiyo wakiwemo viongozi wa makabila, ndio watakaopiga kura za kumchagua rais. Licha ya wanasiasa kadhaa wa Somalia kujitokeza kugombea kiti hicho cha rais, lakini ushindani mkubwa unatarajiwa kuwa kati ya rais wa sasa Sheikh Sharif Sheikh Ahmed, Spika anayemaliza muda wake Sharif Hassan Sheikh Aden na Waziri Mkuu Abdiweli Mohammad Ali.

MASIKINI KENYA....

2:52:00 PM Add Comment

Na Frank M. Joachim.

Habari kutoka eneo la Tana River nchini Kenya zinasema kuwa idadi ya watu waliouawa kwenye machafuko ya kikabila katika eneo hilo imepanda na kufikia 40.



 Maafisa 9 wa polisi ni miongoni mwa waliouawa kwenye ghasia hizo. Kitovu cha machafuko hayo ni katika kijiji cha Kilelengwani ambapo magari kadhaa ya polisi yamechomwa moto na vituo kadhaa kuharibiwa. Makabila ya Pokomo na Ormo yamekuwa yakipigania ardhi ya malisho kwa muda mrefu na mwishoni mwa mwezi uliopita mvutano huo wa ardhi uligeuka na kuwa mapigano ya silaha.

 Utulivu wa kiasi fulani ulirejea lakini mwanzoni mwa wiki iliyopita, machafuko hayo yakaanza upya. Habari zaidi zinasema mamia ya watu wamejeruhiwa kwenye ghasia hizo.

Maafisa zaidi wa usalama wamepelekwa katika eneo hilo ili kutuliza hali ya mambo lakini wakazi wameilaumu serikali kwa kushindwa kuwalinda pamoja na mali zao.

MNADA BANNER