REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

PICHA : PAPA BENEDICT WA XVI Aki-tweet kwa Mara ya Kwanza !!

10:23:00 AM Add Comment

"ADAM JUMA ANATAKIWA KUKUA"-Q Chillah

10:17:00 AM Add Comment
Na Frank M. Joachim "Hasta La Vista Baby"

Wengi sana tushazoea kusikia kuwa Q Chilla ana Bifu na Msanii Fulani...kutokana na Sababu Fulani..ila Hii sasa imekuwa ni nyingine kabisa kabisa.

Q-CHIEF Msanii wa Kizazi Kipya Nchini Tanzania Maarufu kama Bongo Flava, Leo amempasukia Vilivyo Director wa Visual Lab, Adam Juma kwa Madai kuwa ameshindwa kumfanyia Video yake Mpya.

Kwa Mujibu wa "YOU HERD" ya XXL ya Clouds Fm inayokamatiliwa na GOSSIP COP Mwenyewe "Sudd Brown", Chiilah amediriki kumuambia ADAM kuwa antakiwa kukua na kufanya vitu vya kiutu uzima, kwani kamwe hatofanya nae kazi tena kutokana na Sababu hiyo.


Aidha kwa Mujibu wa Chief Kiumbe The Boss ambaye ndiye alilipia Video hiyo, amesema kuwa, yeye ndiye aliyeamua Gharama za Video ya Q-CHILLAH ambazo zilishakabidhiwa kwa Adam,kufanyia Video mpya Ya Shettah inayotambulika kwa BONGE LA BWANA kutokana na Maelezo aliyopata kwa Adam Mwenyewe kuhusu ugomvi wake na Chillah

"Adam alikuwa ameshashoot Video nzima ya Chilla, na kazi iliyobaki ilikuwa ni kumalizia kazi. Iloa kwa Mujibu wa Adam ni kwamba, Laptop yake ilidondoka chini kidogo na kupata Mushkeli, hali iliyosababisha baadhi ya Clips kutoonekana. Baada ya Adam kuona hivyo, alimtaarifu Chilah na Kumwambia kuwa inabidi waanze upya kabisa Video Nzima katika Kushoot, jambo ambalo inasemekana Chilla hakukubaliana nalo, na baadaye akamjibu Adam maneno makali na kuzua kutokuelewana baina yao wawili. Baada ya kuona Adam amegoma kufanya Kazi tena Chillah, ikabidi gharama zote ambazo nilimlipa kwa ajili ya Video ya Chillah zisiende hivi hivi, bali zitumike kutengeneza Video ya Shetta BONGE LA BWANA, na Kuzungumza na Q Chillah kuhusu ni wapi atapenda kufanyia Tena Video na mimi nitamgharamikia maana Chillah Ni Mtu wangu wa Kitambo tu." Alisema CHIEF KIUMBE

Kwa upande wake Chillah, huku akionekana kuwa na hasira haswa, alisema kuwa kamwe hawezi kufanya kazi tena na Adama, na asitegemee kuwa atashoboka na Rangi za Video ambazo zinawababaisha wasanii wengine, kwani bado baadhi yao wanaonekana na Sura mbaya licha ya kupoambwa na Rangi ambazo hazina Msingi.
HILI NI BIFU TAYARI?...au?

LEO KATIKA BIRTH DAY...NI hawa Hapa!!

6:03:00 AM Add Comment
 FATMA SHEMWETA,Mtangazaji wa STAR TV ya SAHARA COMMUNICATIONS Jijini Mwanza....Hivi Sasa Yuko Arusha Kikazi Pia.
Fatma Shemweta amekuwa akihost Shows kamaVile "BONGA NA STAR TV, AFRICAN BEATS,n.k. Nck Nameanayotumiani "FASHY WHITE"
HAPPY BIRTHDAY FATMA
                                            
 NAHREEL,Ni Producer Mkali wa Muziki wa BongoFlava Nchini,na Ametengeneza Mikwaju kadhakama Vile KIUJAMA (Nikki Wa Pili),RIDHI WAN (Izzo B),nk.
Pia Nahreelni Msanii wa Kundi la PAH ONE ambalohivi sasa linatesa na Mkwaju wa I WANNA GET PAID",Ukiwa umepikwa na Nahreel Mwenyewe
HAPPY BIRTHDAY NAHREEL

ROMA Mkatoriki ndo jina analotumiaMara Kadhaa katika Fani yake ya Mziki wa HIP HOP. Hivi sasa Yupo katika LABEL ya TONGWE RECORDS ambayo anaifanya Sanaa yake ya Muziki wa HIP HOP
ROMA aefanikiwa kuchukua TUZO Mbili za Kilimanjaro Music Awards 2012 ikiwa ni MSANII BORA WA HIP HOP na WIMBO BORA WA HIP HOP
Mkwaju ambao ulimtambulisha Mshikaji ni TANZANIA,huku MR PRESIDENT,PASTOR,MECHI ZA UGENINI na MATHEMATICS zikifuatia.
HAPPY BIRTHDAY ROMA

TUKO BIZE

5:18:00 AM Add Comment

Balozi wa Canada nchini, Mheshimiwa Alexandre Leveque akizungumza na Waziri wa Nishati na Madini, Mheshimiwa Profesa Sospeter Muhongo alipomtembelea wizarani leo. Serikali ya Canada imeonyesha nia ya kuwekeza katika sekta ya umeme.

PICHA NA MJENGWA BLOG

KIMATAIFA:Israel Yaonywa

5:08:00 AM Add Comment


Washiriki kwenye kongamano la kimataifa la kuonesha mshikamano na wafungwa wa Kipalestina wanaoshikiliwa na utawala wa Kizayuni wa Israel wameuonya utawala huo ghasibu juu ya ukiukaji wa haki za wafungwa wa Kipalestina na Kiarabu.

Katika sherehe za ufunguzi wa kongamano hilo, Rais Jalal Talabani wa Iraq amesisitiza kuwa, hadi sasa hakuna juhudi zozote zinazofanywa kwa shabaha ya kukomesha machungu na mateso wanayopata wafungwa wa Kipalestina wanaoshikiliwa kwenye jela za Israel na kufichuliwa siasa zisizo za kibinadamu zinazofanywa na utawala huo dhidi ya wananchi wa Palestina. Ameongeza kuwa, kadhia ya Palestina ni kadhia ya ulimwengu wa Kiarabu na Kiislamu tokea  miaka 60 iliyopita na kusisitiza kuwa, kushiriki kwa wingi shakhsia mbalimbali wa kisiasa na kijamii kwenye kongamano hilo kunaonesha jinsi fikra za waliowengi zinavyochukizwa na siasa za ukandamizaji za Israel.

Nabil al Arabi, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu amesema katika kongamano hilo kuwa jinai zinazofanywa na Israel dhidi ya wananchi wa Palestina hazitafumbiwa macho na kusisitiza kwamba viongozi wa Israel wanapaswa kufunguliwa mashtaka kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) kwa jinai za kivita walizotenda dhidi ya wananchi wa Palestina. Nabil al Arabi amesema kuwa, tokea mwaka 2000 hadi sasa wanajeshi wa utawala wa Israel wametia mbaroni watoto na vijana karibu 2000 wa Kipalestina na jambo hilo linaonesha ukiukaji wa wazi kabisa wa makubaliano ya kimataifa ya kuwalinda watoto.

Kongamano la kimataifa la kuonesha mshikamano kwa Wapalestina limeanza leo mjini Baghdad mji mkuu wa Iraq likihudhuriwa na wawakilishi kutoka nchi 70 duniani.

MNADA BANNER