REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

OH MY GOD !!!! : INAWEZEKANA PUA YA JANET JACKSON IKAHARIBIKA MUDA WOWOTE

1:48:00 AM Add Comment

Na Rich Sam    
KWA Mujibu wa Jicho la Mtaalamu wa Masuala ya Upasuaji wa kuboresha Muonekano, Pua ya Janeth Jackson inaweza kuharibika Muda wowote

Kauli hiyo imetoka kwa mtaalamu huyo anayeitwa Dr. MATTHEW SCHULMAN ambaye ana jina kubwa kwa shughuli yake hiyo hiyo katika Jiji la New York

Dr Schulman ingawa sio yeye ambaye kamfanyia Upasuaji wa Pua Janeth Jackson, lakini anaamini kuwa Msanii huyo mkongwe katika tasnia ya Muziki wa R&B na Pop anaweza kukumbana na hali hiyo na tayari dalili zimeshaanza kuonekana mapema hivyo anatakiwa kuwa makini sana

Kukazia Zaidi, Daktari huyo kasema kuwa, inawezekana kabisa kuwa Vipodozi anavyotumia Janeth Jackson, haviendani na havikubaliani na aina ya upasuaji aliyofanya Bibie huyo, nahilo aliliona katika Picha za Red Carpet ya OUT100 Gala’s Music Icon Awar, ambapo pua yake ilikuwa haijakaa sawa kabisa.

Tunamnukuu
 Inaonekana kuna kuharibika kwa Pua na kukaa vibaya kwa pua katika muonekano wa maumbile ya Pua. Hii inaweza kutokana na kufanyiwa upasuaji waPua mara kwa mara na huenda kuna maumivu ambayo alipata, na hii pia huchangiwa na aina ya Vipodozi ambavyo anatumia"

KUDADEKI !!! : SAFAREE SAMUELS ANAUHITAJI UTAMU WA NICKI MINAJ TENA

1:06:00 AM Add Comment

Na Baba Juti   
KAMA kweli ni kubaniana, basi inawezekana Safaree Samuels alibaniwa vitu vingi sana na aliyekuwa Mpenzi wake kipindi kileeee, Nicki Minaj, na ndio maana uvumilivu umemshinda kiukweli

Zaidi ya Masaa Matano yaliyopita, Safaree Samuels alioneshwa kushindwa kuvumilia baada ya kuona Utamu ambao Nicki Minaj anauonesha sasa hivi , na wala hakuwa kumuonesha kipindi kile wako pamoja katika Mahusiano yao

Safaree alipost picha ya Front Cover ya Jarida la PAPER ambalo Nicki Minaj alionekana kuwa Mbele zaidi kwa picha ambazo zinamfanya kila mtu atoe mimacho na mate ya kutosha

Picha hiyo inamuonesha Nicki Minaj akiwa katika Positions tatu tofauti ambazo zilionekana kumchanganya sana Ex wake huyo ambaye waliachana kwa vimbwanga vya hali ya juu

aliandika Hivi
"tunaweza kugundua Kitu hapa tafadhari?, hizi ndizo aina ya picha ambazo  kila mara nimekuwa nikitaka uzipige kwa ajili yangu ! Wow.... "

UPO HAPO !!!!?: RICK ROSS AUNGANA NA WAANDAMANAJI PHILLADEPHIA KUPINGA HUKUMU YA RAPPER MEEK MILL

12:46:00 AM Add Comment

Na Baba Juti   
Watu Wa Mungu, Sasa mambo yameanza kuwa na uzito idogo ikiwa ni baada ya kutolewa Hukumu ya Rapper Meek Mill.

Hali imekuwa sio shwari katika Mji wa Philladephia Nje ya mahakama ya Mji huo, ikiwa ni baada ya Wananchi na mashabiki wa Rapper Meek Mill kwa wingi kujitokeza na kuanzisha Maandamano ili kupinga Hukumu yake

Kuanzia November 13, Supporters hao waliingia Mtaani na kuanza kupinga hukumu ambayo imempata Meek Mill huku wakidai kuwa kumekuwa na ukandamizaji wa hali ya juu hasa katika Maamuzi ya mahakama huku Masuala Binafsi yakiwa ndani yake sanjari na ubaguziwa Rangi

Yote Tisa, Kumi ni baada ya Rapper Rick Ross naye kuamua kuingia mtaani kuungana na waandamanaji hao ili kuhakikisha kabisa kuwa haki kwa msanii ambaye yuko Chini ya Records label yake, anapata haki ya Msingi

Basi Nne kubwa zikiwa na ujumbe wa "SIMAMA KWA AJILI YA MEEK MILL" zilionekana zaidi ya Mbili katika Bara bara tofauti, zikiwa na shughuli moja tu, kupinga hukumu ya Rapper Huyo

MNADA BANNER