REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

USWAZI-TAKE: BIASHARA YA CHIPS USWAHILINI- SOMETIMES INAKUBALI, SOMETIMES INADODA

10:18:00 AM Add Comment




MFUNGWA ALIYEANDIKA NYIMBO 3000 AKIWA GEREZANI, AMEWAFUNGULIA MASHTAKA JAY Z, RIHANNA, KANYE WEST, BEYONCE NA CHRIS BOROWN, KWA KUMUIBIA NYIMBO

1:48:00 AM Add Comment

Kama ambavyo tumeweza kukuambia jana, moja kati ya watu ambao wanatafunwa na Mbwadidi la Wizi wa Nyimbo, Idea, Beats na kadharika, ni wasanii wakubwa, tena wenye Majina na Heshima Kubwa tu, kunako music industry Ulimwenguni Kote

Baada ya jana kukupa Mtonyo kuwa DJ KHALEED yuko kunako Msala Mzito wa kuiba idea ya Cover ya Msanii Mwingine na Kuitumia, This Time TTM tumenyaka Nyingine kuwa Kuna Mfungwa Mmoja ambaye amewafugulia mashtaka JAY Z, KANYE WEST na RIHANNA kwa Madai ya kuibiwa Ngoma Yake.

Unaweza ukajiuliza kuwa Mchakato huo Ukoje, ila kwa Mujibu wa data za kutosha kutoka Kunako KITENGO CHIMBUA CHIMBUA, inasemekana kuwa Mfungwa Huyo kutoka Jijini CALIFONIA, anayefahamika kwa Jina la RICHARD DUPREE, anaweza kuwa mmoja kati ya Waandishi wa Nyimbo wa Kuogopwa  katika Karne Yetu, baada ya Kudai kuwa, JAY Z, KANYE WEST, RIHANNA, BEYONCE na CHRIS BROWN wamemuibia Baadhi ya Nyimbo kati ya Mikwaju 3000 aliyoiandika akiwa Jela.

Kwa Mujibu wa Maelezo ya Mfungwa Huyo, Amesema kuwa kutokana na Wizi huo ambao anauhakika nao kabisa ikiwemo Ngoma ya RUN THIS TOWN ya Jay Z, Kanye West na Rihanna, amefungua Mshtaka ya Madai ya Fidia katika Utumikaji wa Mikwaju yake bila Idhini yake, na Kiasi ambacho anahitaji ni USD MILLION 2.4, ingwa haitakuwa kazi rahisi kwake kuzipata hasa katika kipindi hiki.

Lakini KITENGO CHIMBUA CHIMBUA kimezidi kumimina Ripot kuwa, Dupree anadai kuwa Njia ambazo Zilitumika kuiba Nyimbo zake ambazo alikuwa akiziandikia GEREZANI, ni Mashirika ya Kiusalama Nchini Humo, CIA,JESHI LA POLISI na FBIYONCE kupata Nyimbo hizo.

Mashtaka hayo yamefunguliwa katika Mahakama ya Mashariki Mwa CALIFONIA, mnamo APRIL 21

KESI YA CHRIS BROWN IMEPANGIWA TAREHE YA KUSIKILIZA

1:39:00 AM Add Comment

Pretty Boy Chris Brown Hivi sasa ameshaspend Muda wa Wiki saba Nyuma Ya Nondo yaani Gerezani, kutokana na Kukiuka Masharti ya 

Rehab pamoja na Adhabu ambazo zilikuwa zikimkabili.
Siku ya jana Chris Brown alitokea kunako Mahakamani ili kufahamu hatma ya Kesi yake kusikilizwa pamoja na hukumu Kutolewa

Akiwa Mnyonge, amedhoofika Kidogo, Chris Brown alionekana akiwa Mwenye nidhamu huku akipokea maamuzi kutoka mahakamani juu ya kusikilizwa kwa Kesi yake

Kwa Mujibu wa Mahakama, Breezy ambaye amewahi Ku-Hit na Mikwaju kadhaa ikiwemo BEAUTIFUL PEOPLE, YEAH X 3, Kesi yake itasikilizwa Mnamo MAY 9 Mwaka Huu, lakini Breezy bado atabaki Jela, kunako Gereza la LOS ANGELS (L.A)


Breezy amekuwa Nyuma ya Nondo kuanzia MARCH 14 baada ya Kutimuliwa Rehab, na endapo atabainika kuwa na Makosa, basi huenda akahukumiwa Kifungo cha Miaka 4 Jela

MNADA BANNER