REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

VERA SIDIKA: USIJICHUBUE OVYO , KUNA FAIDA ZAKE

7:07:00 AM Add Comment



 Na Baba Juti
#WatuWaMungu kama kuna wale Watoto wa Kike hapa Nchini Tanzania huwa wanajichubua na Kujiongezea Mvuto hasa kimaumbile kwa sababu ya kuvutia wanaume ama kufuata Mkumbo, basi tumieni akili sana, Kenya wanawafunika kupita Maelezo

Wanawake Wengi Nchini Kenya, hutumia Gharama Nyingi sana kuboresha Muonekano Wao, kitu ambacho wao kama wao wanadai kuwa kinarudisha Gharama hizo walizotumia pamoja na kupata Faida Juu.

VERA SIDIKA, binti ambaye mara Nyingi hutolewa Mfano katika Kujichubua na Kuongeza Maumbile ya Mwili wake hapa Afrika Mashariki, yeye ni mmoja kati ya Wale ambao hawajutii kufanya hivyo sababu kuna Vitu vingi sana ambavyo anafaidika Navyo kutokana na hatua yake

Akifafanua kuhusu Kile ambacho kinaendelea Juu yake, Vera anadai kuwa, yeye kama yeye, alijichubua na hata kuongeza Ukubwa wa Matiti na makalio, ila ni kwa sababu ya faida ambayo ameipata Mpaka Hivi sasa

Vera amedai kuwa, Tangu amejichubua, basi ameng’arisha Brand yake  na alifanya hivyo kwa sababu alitaka aishi maisha ya Furaha ambayo anayataka

Katika faida aliyopata, Vera anadai kuwa ameweza kuhost Events Nyingi ambazo zimepatikana kutokana na Muonekano wake, Amepata Watu Wengi ambao wanamfuatilia, Bookings Nyingi za Events, Dili Nyingi sana za Kibiashara ambazo zinamjia mpaka hivi sasa, Kufanya Kazi na makapuni makubwa ya Kibiashara, na bado anashughulikia Kipindi chake Cha TV , pamoja na mambo Mengi ambayo yako Njiani

Lakini katika Suala Zima la Kuboresha Muonekano wake, VERA anadai kuwa Ilimgharimu almost Shilingi za Kenya Milioni 15, nab ado watu walikuwa wanahisi kuwa hatofika Mbali na atakuwa ameshaharibika, ila mambo yamekuwa Tofauti

WAHUJUMU: BEYONCE ANATUKANDAMIZA SANA KWWENYE HII KESI

6:56:00 AM Add Comment



  Na Baba Juti  
#WatuWaMungu kwa kumbu kumbu zetu,. Tumewahi kuwaambia kuwa mamito BEYONCE aliwafikisha Mahakamani wamiliki wa Mtandao mmoja ambao umekuwa ukitumia Sehemu ya Jina lake na Kazi zake kuzalisha Bidhaa kinyume cha Utaratibu.

   ILIKUWAJE?  
BEYONCE alifungua Mashtaka Dhidi ya Wafanya biashara Wawili ANDRE MAURICE na LEANA LOPEZ ambao walikuwa wanamiliki wa kampuni ya MERCH ambao walikuwa wanatengeneza bidhaa mbali mbali zenye jina la FEYONCE ambalo linatokana na kila kitu cha Jina lake la BEYONCE hasa lilivyotumika katika album yake aliyoipa jina la BEYONCE

Kampuni hiyo ilikuwa inazalisha vitu kama Vile TISHRT za Kike na Vitu vinginevyo, lakini wakitumia Logo Hiyo. Tofauti na hilo, walianza kuzalisha Tshirt na Bidhaa nyingine zenye maneno ya PUT A RING ON IT, maneno ambayo yalitumika katika wimbo wa Beyonce unaoitwa SINGLE LADIES

  WANACHODAI WATUHUMIWA 
Kwa Mujibu wa Malalamiko yao Mapya, Wawili hao kutpoka kunako Kampuni hiyo, wanadai kuwa BEYONCE amekuwa akiwakandamiza sana katika Kesi hiyo kitu ambacho kinawanyima Uhuru wa kufanya Vitu vyao vingine

Mnamo May 11, wawili hao walidai kwamba wamefanya kila liwezekanalo kufuta matangazo ya Bidhaa hizokwenye website ambayo inatangaza bidhaa hizo ingawa bado inakuwa Ngumu

Ukiachilia hilo, Wawili hao wanazidi kudai kuwa Beyonce amekuwa akitumia Jina lao kuzuia Riziki ambazo zinakuja kwao, kitu ambacho kimewakosesha Fedha Nyingi sana mpaka Hivi Sasa
Hivyo, wanaomba Mahakama Kupiga Chini Kesi hiyo ili wafanye Shughuli zao Nyingine

MNADA BANNER