REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

UNAHITAJI KUFANYA SHOW NA DMX?..ANDAA BOX 3 ZA KONDOM

11:49:00 PM Add Comment

Na Frank M. Joachim, BLACK TOUCHEZ
KUNA VITU ambavyo Wasanii Wengi Maarufu ambao tayari wameshakuwa na majina, huvihitaji kila wanapoenda katika Show Fulani ambayo imeandaliwa kwa ajili yao, au wameandaa wao Binafsi.

Nchini Marekani, BLACK TOUCHEZ BLOG imeweza kunasa baadhi ya Mahitaji ambayo Wasanii wakongwe hawa  huvihitaji katika Vyumba ama Mahali wanapofikia kabla ya kupanda kwa Show, na hata Baada ya Kumaliza Show



KANYE WEST:
KIPINDI cha awali, KANYE WEST alikuwa akihitaji Urembo Mweupe mahali ambako angefikia kabla ya kupanda Kunako Stage, lakini kwa kuwa hivi sasa ni baba wa North West, basi huhitaji Watu wa kumtizama Mtoto wake huyo, Chumba maalum ambacho kitakuwa na TV maalum yenye Program maalum anazopenda Binti ake huyo (North West), na hugharim USD 8000.

Pia Kanye West Huhitaji Mpish Maalum ambaye ataandaa chakula maalum kwa ajili ya Mtoto wake…na hasa kile anachokifurahia.


JAY Z:
Chanzo Kimedai kuwa, Kipindi ambacho Jigger alikuwa katika Tour na Justin Timberlake, waliyoipatia jina la LEGENDS OF SUMMER TOUR, alihitaji Club maalum kwa ajili yake na wenzake mahali ambako alifikia.
Na moja kati ya vitu ambavyo alionekana kupendelea sana kutumia, ni pamoja na Sigara


DMX
Rapper Huyu hapa ambaye awali alivuma sana na Kundi la RUFF RIDERS, inasemekana yeye huwa hana Mbwembwe nyingi na mizunguko Mingi, kuhusu maandalizi ya mahali ambako atafikia kwa ajili ya Show.
Chanzo kimedai kuwa, DMX huwa yuko wazi kabisa kuwa anahitaji uwepo wa Box 3 za CONDOMS (Kinga) na Gallon moja ya HENNESSY


BEYONCE:
MAMITO huyu ambaye mwaka huu anaumaliza Vizuri, inasemekana kuwa katika Chumba anachofikia, hupenda kuwa Muwazi katika Bidhaa za Kibiashara ambazo huwa anafanya nazo kazi. Hivyo huhitaji Bidhaa ziwepo Chumbani Kwake, (Mfano PEPSI, HONEY NUT CHEERIOS, nk.)
Pia Beyonce Huhitaji Choo kiwe safi kabisa ili kuepuka Maradhi, na inasemekana kuwa huwa hapendelei Chumba chake kiwe na Chocolate au Vitu Vitamu Vitamu kama Vile PIPI.


SEAN COMBS “P.DIDDY”
MKONGWE Huyu anafahamika sana kwa kupenda Maisha ya “BATA” na raha tele. Sasa kama unamuhitaji katika Tour ama Show yako, basi andaa vitu Vifuatavyo katika Chumba atakachofikia:
TAULO 204, SABUNI 20, CHUPA 2 ZA HENNESY, CHUPA 2 ZAsanta Margherita Pinot Grigio, CHUPA MBILI ZA Veuve Clicquot, CHUPA MOJA YA  Dom Perignon, Grey Goose vodka, MAUA MEUPE , na GARI AINA YA MAYBACH yenye Bullet Proof, inayogharimu USD 300,000


PHARELL WILLIAMS:

HITMAKER huyu wa Happy, huhitaji akina dada ambao hucheza style ya BELLY DANCE (Belly Dancers)


MNADA BANNER