REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

REDSAN KAFANYA FUJO...TAARIFA HII HAPA

3:37:00 AM 1 Comment

Na Baba Juti
MAPEMA asubuhi ya leo, taarifa zimefikishwa katika dawati la "Hit Zone" kuhus kitendo cha Producer SAPPY kutoka jijini Mwanza ambaye muda mwingi hufanya kazi zake Nchini Kenya, kuvamiwa na kujeruhiwa akiwa studio kwake Nchini Humo

Kwa mujibu wa Taarifa kutoka kwa ERVIX ambaye pia ni Msanii kutoka nchini Tanzania anayefanya kazi Nchini humo chini ya SAPPY MUSIC LAB inayomilikiwa na Producer Sappy, tukio hilo limetokea Siku ya jana na Vurugu hizo ziliznzishwa na msanii nguli kutoka nchini Kenya, REDSAN.

Msanii huyo amezidi kueleza kuwa, chanzo cha ugomvi huo, ni kitendo cha wao (Ervix na Sappy) kutokuhudhuria katika Uzinduzi wa Album ya REDSAN ilihali Sappy ndiye aliyeproduce nyimbo nyingi zinzopatikana katika Album hiyo.

Sababu ambazo ziliwafanya wawili hao kutokuhudhuria katika Uzinduzi huo, ni pamoja na Sappy kupata safari ya kikazi Mombasa, kutokuelewa mustakabali wa faida ambayo ataiapata sababu ameproduce nyimbo kadhaa na hajui atanufaika vipi maana nyimbo iliyolipiwa ni moja, Ervix kutokuhudhuria katika Shughuli hiyo sababu ya mizunguko ya hapa na pale....

SIKILIZA sauti ya ERVIX

SUBIRI KWANZA !!!!! : JUSTIN BIEBER NA HAILEY BALDWIN WAMEFUNGA NDOA TAYARI?

2:57:00 AM Add Comment

Na Hezroni Munisi  
WATU WA MUNGU inawezekana kabisa kuwa Justin Bieber na Mchumba wake HAILEY BALDWIN wakawa wameshafunga ndoa "Kimya Kimya" ?

Kipindi cha nyuma kidogo, taarifa zilikuwa zimeshaenea kabisa kuwa Justin Bieber ambaye awali alikuwa katika mahusiano na Selena Gomez, amezama kwa bibie huyo ambaye anatokea katika familia ya watu maarufu hapa ulimwenguni.

Sasa baada ya kutokuambiwa Ndoa ya wawili hao ni lini, huku wao wakificha licha ya kwamba wameshavalishana pete ya Uchumba, hatimaye Mjomba wa Hailey Baldwin, muigizaji ALEC BALDWIN amejikuta akitoa taarifa ambayo inashabiliana kabisa na wawili hao kufunga Ndoa tayari na ilikuwa ni ya Siri haswa

Akiwa katika upande wa "Red Carpet" kunako Tuzo za EMMYS (Emmys Awards 2018), Alec ambaye ni Mjomba wa Hailey alisema kuwa wamefunga ndo ya Haraka na ya siri kwa asilimia kubwa kwa sababu kwao , suala zima la ndoa, ndicho kitu ambacho wamekuwa wakikitamani muda mrefu na kitawaunganisha na kuwapa Furaha

"Kilichotokea mahakamani, ni kitu cha mahakamani na ni suala la kisheria. Ila Ndoa, ni pale ambapo watu wawili wanaweka wakfu mbele ya mwenyezi mungu na watu wanaowapenda...."
alisema Mjomba mtu

RAPPER WALE AZUIWA KUKAA KATIKA DARAJA LA KWANZA KWENYE NDEGE YA AMERICAN AIRLINES

2:10:00 AM Add Comment




Na Rich Sam
WAKATI mataifa mengi na wananchi wengi ndani ya mataifa hayo yakiendelea kupinga kabisa kitu kinachoitwa "UBAGUZI WA RANGI" safari hii huenda mambo yakawa magumu haswa kwa shirika la ndege Nchini Marekani (American Airlines) baada ya kulalamikiwa kwa mara nyingine tena

RAPPER Kutoka Nchini humo ambaye asili yake ni Nigeria Barani Afrika, WALE, ametoa kilio chake kup[itia account yake ya Twitter kwa madai kuwa alifanyiwa ubaguzi wa Rangi baada ya baadhi ya Wahudumu kumwambia kuwa hakustahili na hana hadhi ya kukukaa katika daraja la kwanza ndani ya ndege hiyo

Tukio hilo limetokea hivi karibuni ikiwa ni baada ya Wale kulalamika kuwa alikuwa amekata Ticketi ambayo ni sahihi na alitakiwa kukaa katika Seat yake sahihi kabisa, lakini baadaye alizuiwa kuingia katika daraja hilo kwa Takriban dakika 30 mpaka 45, na kisha baadaye safari yake kuahirishwa


Wale ambaye ni "member" wa MMG, kundi ambalo liko chini ya Rapper Rick Ross, aliona hana budi kulalamika kupitia Twitter huku akiripoti kuwa ataenda kuwashtaki polisi kwa kitendo hicho

"Vipi kuhusu wafanyakazi wenu MEGUUMI na DON waliponiambia kuwa sitakiwi kuwa katika Daraja la Kwanza?... ninawapigia Polisi" alilalamika hivyo Wale

Ukiachilia mbali Twitter hiyo, Wale alidirikikuhoji ni hatua gani zitachukuliwa zidi ya wafanyakazi hao wawili

"Nyie nyote ni wabaguzi wa Rangi. Ninataka kujua ni hatua gani itachukuliwa. MEGUUN na DON ndio majina yao"



MNADA BANNER