REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

OZIL KATIKA KASHFA YA KUMTUMIA MESEJI ZA KIMAPENZI MPENZI WA MCHEZAJI MWENZAKE WA ARSENAL

11:05:00 AM Add Comment
 Na Frank M. Joachim & Daily Mail
Ndio Maana mie mara Nyingi huwa nakiri kabisa kuwa Sitaki namba ya Mke/Mchumba/Mpenzi wa rafiki yangu, hali kadharika Sipendi namba ya Mke/Mchumba/ Mpenzi wangu ipatikane katika Simu ya rafiki yangu. Iko Hivi

MCHEZJI wa Arsenal ambaye ametokea katika Club ya Real Madrid, MESUT OZIL, ameingia katika Tuhuma kama sio Kashfa, ya kumtumia Meseji Tata, Girlfriend wa Mchezaji Mwenzake (shemeji), katika Club ya Arsenal,

Tukio hilo limeanza kuchukua Sura Mpya baada ya hali kuwa Si hali, huku Mchezaji mwenzake na Ozil, CHRISTIAN LELL akimpiga Chini Girlfriend Huyo aliyetumiwa Meseji na Ozil, MELANIE RICKINGER
Meseji hizo ambazo zimekuwa zikitumwa kwa njia ya Mtandao wa WHATSAPP, inasemekana zilikuwa za kimahaba Fulani hivi, na zilikuwa zikitoka kwa Mesut Ozil.

KUHUSU MCHUMBA WA OZIL
BAADA ya hali kuwa Tete bado, BLACK TOUCHEZ tumenyaka Picha ambazo zinadhihirisha kuwa, Mchumba wa Ozil, CAPRISTO, anahamisha Vitu vyake kutoka katika Jumba la Ozil, hali inayoashiria kuwa, bibie huyo ambaye ni msanii wa Muziki aina ya POP STAR.
Vitu ambavyo vimeonesha kuwa bibie huyo ni kweli “anasepa”, ni Piano lake na baadhi ya Vitu kupakiwa katika Gari, kwa ajili ya kuondoka katika jumba hilo lililoko Jijini London

GIRLFRIEND WA RAFIKI WA OZIL ANASEMAJE
Girlfriend wa Christian Lell, Melanie amekiri kuwa Msg Hizo zilikuwepo kweli, lakini alishazifuta, na inawezekana Christian alizirudisha

OZIL ANASEMAJE
Ozili amegoma kuzungumzia Chochote Mpaka Hivi sasa















ANGEL BENARD: NEED YOU TO REIGHN, THE LORD'S MESSENGER

8:03:00 AM Add Comment

NA FRANK MAGNUS JOACHIM, Black Touchez
KUNA muda inabidi tuamue na kukubali hasa pale tunapobaini ni kipi hasa ambacho tunatakiwa tukifanyie haki katika Maisha Yetu ya Kila Siku.

Jambo hili hakika linamfurahisha sana Mwenyezi Mungu, ambaye tunaamini kuwa Ndiye Shujaa, na Mmiliki Pekee wa Ulimwengu huu, na kila kilichopo Ndani Yake.

Hakika, ukipitia maneno yake Mengi katika Ukurasa wake wa FACEBOOK, unabaini ni hazina iliyoje, ambayo wazazi wa Binti huyu, wamejaliwa kuwa nayo, hasa kutoka kwa Mungu.

Nimemfahamu kwa jina la ANGEL BENARD, ikiwa ni katika Pita zangu za Huku na kule kwa ajili ya kulisha Wasomaji Wangu. Binti huyu ni Msanii mwenye Kipaji cha aina yake, ambayo Binafsi maishani mwangu Sijawahi kukutana nacho.

Angel ni Msanii wa Muziki wa Injili (GOSPEL) hapa Nchini Tanzania, na ameshafanya Kazi kadhaa ikiwemo NIKUMBUSHE WEMA  WAKO, SHUJAA na ule ambao ni zaidi ya Hisia katika Moyo wangu, NEED YOU TO REIGHN, alioachia Video yake rasmi OCTOBER 23,2014, kupitia account Yake ya YOU TUBE (Angel Benard)

  • ·        Muziki Wake:
HAKIKA Muziki wa Angel, sina budi kukiri kuwa, ni Vionjo ambavyo vinabeba Ujumbe Mzuri sana kutoka kwake Mwenyezi Mungu. Anatumia Kipaji na Uzuri wa sauti aliyonayo, kutoa Ufahamu Mzuri sana kuhusu kile ambacho Mungu ametuumba tukifanye, na hata tukizingatie wakati ambao tunastahili kufanya Hivyo.

Kuna maneno ambayo Angel anayatamka katika kila Kazi anayoifanya, yanayokushawishi kuacha unachokifanya, na ukamskiliza kwa umakini, huku ukiondoka na Jambo ambalo usingelipata kwa Njia ya kawaida

Binafsi, ninahaki ya kusema kuwa, Angel ni Binti ambaye anazingatia sana kile ambacho amejaliwa. Lakini licha ya Kuzingatia ambacho amejaliwa, Angel anathamini sana Fadhila ambazo anatakiwa kuzirudisha kwa Yule aliyemjalia Kipaji na Sauti Nzuri, Yaani MUNGU. Na Fadhila Hizo, ni kutangaza Neno lake Mungu kwa Njia ya Wimbo, huku akiamini kuwa, kupitia sauti yake na Mashairi yake, Kondoo Wengi watamrudia Bwana.

Nyimbo ambazo amezifanya kwa Nguvu za Ajabu kutoka kwake Mwenyezi Mungu, ni pamoja na NIKUMBUSHE WEMA WAKO, SHUJAA, na NEED YOU TO REIGHN.

  • ·        Ukurasa Wake Wa Facebook.
Kuna mambo makubwa ya Msingi MATANO, ambayo Binafsi nimeyagundua na Kujivunia sana kukutana nayo katika Ukurasa Wake wa Facebook (Angel Benard), ambao pia una-LIKES zaidi ya 6000, tangia ameuanzisha NOVEMBER 12,2013

        i.            ANGEL IS THE LORD’S MESSENGER : Anafikisha Ujumbe Wa Mungu hasa kwa kile ambacho ukikifuatilia unaamini kuwa anakizungumza kwa Hisia ya Pekee. Anajaribu kutumia uelewa wake, Imani yake, na hata hali aliyonayo muda huo kufikisha Ujumbe wa Mungu kwa maneno machache Sana, ambayo wazungu husema “Lovely, Short and Really Clear”


      ii.            ANGEL LOVES : Angel hajui kubagua wala kushindwa kuonesha hisia zake hasa kwa kile anachokipenda kwa Dhati. Anatumia ukurasa wake kuonesha ni kiasi gani anaweza kumpenda mtu, na hata kuonesha ni kiasi gani anaguswa.


    iii.            ANGEL APPRECIATES. Unaweza kuona ni Kiasi gani anaufahamu umuhimu wa Wazazi hasa katika Dunia hii na Maisha yake Kiujumla. Niliweza kuona namna ambavyo anafikisha Shukrani zake kwa Wazazi wake na hata kujivunia Kuwa nao katika Kila aina ya Upande. Inaonekana kabisa kuwa, wazazi wake wamekuwa naye Bega Kwa Bega.


  iv.            ANGEL SUPPORTS. Si kwa sababu yeye ni Msanii, basi anatakiwa kuwa kujikita zaidi katika Kazi zake, na hata kuwasahau Wengine ambao wanafanya kazi ile ile anayoifanya Yeye. Angel Pia ameweza kuonesha ni namna gani anawajali wasanii Wenzake hasa kupitia UKURASA wake wa Face Book, pale wanapoachia kazi zao.


    v.            ANGEL PROMOTES: Kama ilivyo kwa Wasanii wengine Tofauti ulimwenguni, Nimebaini kuwa, tofauti na hayo Yote, Angel anatumia Ukurasa Wake kutangaza kazi zake za muziki ambazo zinakuja na hata ambazo tayari zimeshaachiwa.



  • ·        Video Ya Need You To Reighn.

VIDEO ya Need Tou To Reighn Imeshaachiwa tayari hasa katika Mtandao wa Facebook. Ukiifuatilia kwa Ukaribu, unagundua Furaha na Hisia ya Kile Kitu ambacho anakiwasilisha kwa Hadhira.

Kuna muda ninaamini hakumpa Wakati Mgumu Director ambaye alikuwa akifanya kazi naye hasa wakati wa zoezi la Upigaji Picha (Shooting).

Angel ameonekana ni Mtu wa Furaha pale anapotakiwa kuonesha kwanini anafuraha, Ni mwenye Kuelekeza pale anapotakiwa kuelekeza Mfano “Mahali hapa”, anaonesha mahali hapo alipo, Ni mwenye kutulia katika mahali anapotakiwa Kutulia, na ni mwenye kucheza pale anapotakiwa kufanya Hivyo.



Video Hiyo imeshatizamwa na watu zaidi ya 300 tangia imeachiwa OCTOBER 23,2014 katika Mtandao wa Youtube



  • ·        Nimependa Alivyoelezea Short History Yake:
Unaweza kuchukulia Mambo tofauti kuhusu Kipaji na Imani ya Angel, Lakini Hebu soma hapo, alichokiandika Katika Ukurasa wa Facebook

“Nilianza kuimba toka Mdogo..but rasmi makanisani hata kabla ya kumpokea Yesu since 2004 and now ni 2014. Ten years in ministry. Katika uchanga mwingi, vurugu nyingi hadi kukua pia..nimemuona Mungu.
Kama hukuniona Jana huwezi jua Leo Mungu ananifanyia maajabu kiasi gani.
Naicheka Jana yangu,Naifurahia kesho yangu.

Asante Mungu Kwa kunipa watu sahihi kwa wakati sahihi,Ili nitende yaliyo sahihi katika season yangu. Asante Roho Mtakatifu Mpenzi wangu muaminifu.

Machozi ya Furaha yananitoka nikiangalia nilipotoka na ninapoenda.

Never give up..keepbelieving keep moving.
Soon kunakucha.”

Kwa Kumalizia, Ninaomba kabisa, kama tunafahamu Kipaji, Muziki wa Hisia na Ujumbe Mzuri, tafadhari Ninawasihi sana, Tumpe Support Angel Benard.

Binafs Ninampenda Sana !!!!!..GOOD JOB

MGONJWA WA EBOLA AGUNDULIKA JIJINI NEW YORK

2:16:00 AM Add Comment

 
BBC SWAHILI
Daktari wa Marekani aliyekuwa akiwahudumia wagonjwa wa Ebola Nchini Guinea amepimwa na kukutwa na virusi vya ugonjwa huko katika hospitali ya ya mjini New York.

Dr Craig Spencer ambaye ni mmoja kati ya madaktari wasio na mipaka alianza kujisikia maumivu na homa siku chache tu baada ya kurejea Marekani akitokea Afrika Magharibi.


Siku ya Alhamisi wiki hii Craig alipelekwa hospitali kwaajili ya vipimo na kisha akatengwa kwa uchunguzi zaidi wa afya yake.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari Meya wa mji wa New York Bill de Blasio amesema watu hawapaswi kuwa na hofu kwani hatua zote mhimu zilifuatwa katika kumchunguza Dr.Craig na hadi alipobainika kuwa na maambukizi hayo.

Kubainika kuwa na virusi vya ugonjwa wa Ebola kwa Dr.Craig kunaongeza idadi ya waliobainika kuwa na ugonjwa huo nchini Marekani kutoka watatu na kufikia wagonjwa wanne.

KUNA UWEZEKANO AMBER ROSE NA WIZ KHALIFA WAKARUDIANA?.

1:59:00 AM Add Comment


NA FRANK JOACHIM & DAILY MAIL
NI KWELI, Amber Rose na Wiz Khalifa wamepigana Chini , hali iliyotokea Mwezi ulopita, lakini linapokuja suala la malezi, wawili hawa wako makini na furaha juu ya Mtoto wao Sebastian.

Hivi karibuni, Camera za Wadakuzi zilimnasa Wiz Khalifa na Rasta zake za Pink, akiwa ametoka Kumchukua Sebastian The bash, Mtoto wao Wa Kiume kutoka kwa Amber Rose, huku wengi tukiamini ni Sehemu ya makubaliano yao

Amber Rose alifungua Madai ya Talaka toka kwa Wiz Khalifa ambaye ni Mumewe halali, baada ya kubaini kuwa rapper Huyo wa WE DEM BOYZ alikuwa akimsaliti, hali ambayo ilimfanya Wiz na yeye afyatuke kuwa Amber amekuwa akimsaliti Pia

·        Mahaba Bado Yanaendelea?.
HIVI karibuni, wawili hao wameonesha Vijidalili vya kuwa na mahaba japo Kibishi ukizingatia kile ambacho kimetokea baina yao.


Katika Birthday ya Amber Rose hivi majuzi tu, Wiz Khalifa alitweet “HAPPY BIRTHDAY AMB”, na mamito Amber Rose kujibu “THANK YOU SWEETHEART #StillLoveYouNoMatterWhat”

Hali hii inaashiria kabisa kuwa, Amber Rose bado ana mahaba ya Dhati kwa Wiz, na hata Wiz pia bado ana mahaba mazito kwa Amber

·        Zile Zilikuwa Ni Hasira Tu
Licha ya maoni ya Wengi kuonekana kumuonea huruma sana Mtoto Sebastian, lakini asilimia kubwa ya watu hao, wamejikuta wakikubaliana na Kitu “HASIRA” ambazo Amber Rose alikuwa nazo baada ya kukuta kitendo cha Usaliti dhidi yake kikifanywa na mumewe, lakini kuna uwezekano wawili hao wakarudiana


Wiz Pia alikuwa na hasira za karibu ambazo zilimfanya ajibu Maneno tofauti mabaya juu ya Tuhuma za Amber Rose, lakini Ukweli ni kwamba hivi sasa hasira zimetulia, na kila mtu anaonesha Hisia kwa Mwenzake

SAUTI SOL NA IYANYA, KILA KITU TAYARI

1:47:00 AM Add Comment


Na FRANK M. JOACHIM
IKIWA ni baada tu ya kupokea  tuzo ya MTV  EUROPE MUSIC AWARDS- BEST AFRICAN ACT kwa mwaka huu wa 2014, SAUTI SOL wameamua kudhihirisha Furaha yao kupitia kazi yao na Iyanya Kutoka Nchini Nigeria.

Siku ya jana kunako Mtandao wa YOUTUBE, Sauti Sol waliweza kuachia Video yao ya SURA YAKO REMIX ambayo wamemshirikisha Iyanya kutoka Nchini Nigeria kama ambavyo awali tumekutonya.

Track Hiyo hivi sasa imeshakuwa kama Wimbo wa taifa Nchini Kenya hasa kwa kufahamika na hata kupendwa na watu wengi, inatarajiwa Kupenya Sana mpaka Nchini Nigeria, hasa baada ya kupiga Collaboration na Iyanya, pamoja na Kundi la Sauti Sol kuchukua Tuzo hiyo Muhimu sana Kwao.

TIMU iliyohusika Kusuka Video hiyo ni ya ENOS OLIKI & BOKEH FAMILY, ambayo pia ilihusika katika Video ya NISHIKE ambayo ilizua Mastori kibao sana Nchini Kenya.


·        Ilivyopokelewa:
Kiujumla Video imepokelewa vizuri na huenda ikawa na Njia ya aina yake hasa baada ya kupata Views nzuri. Mpaka TTM tunaingia kunako Hewa, Video ya SURA YAKO REMIX imepata watizamaji  5,516, na imeweza kupata LIKES 242.

Ukizungumzia Area za Comments, Wengi wameweza kupongeza Video hiyo, hasa wananchi wa Kenya, ambao pia wamejivunia kwa SAUTI SOL kuleta Heshima kwa kuwa Wanamuziki wa kwanza kushusha Tuzo kubwa kama hiyo Nchini Mwao.

F*CK WIZ KID: MANENO YA MSANII KUTOKA UGANDA, NI BAADA YA KUMDHARAU JOSEE CHAMELEON

2:50:00 AM Add Comment
KAMPALA, Uganda
USIKU wa jana kunako GOLF COURSE HOTEL Jijini Kampala, Msanii Wiz Kid kutoka Uganda alishusha Burudani tamu katika THE GUINNESS VIP PARTY

Sasa, Mbwadidi lilikuja katika kujikuta akitukanwa na Msanii kutoka Nchini Uganda katika mtandao wa facebook, hasa kutokana na kile kitu ambacho alikijibu katika Interview na Kituo cha NTV-Uganda.

ILIKUWAJE?
WIZ KID, ambaye ni Mshindi wa Tuzo ya BET AFRICAN ACT 2014, aliulizwa Swali kama anamfahamu msanii anayeitwa JOSE CHAMELEON (infact kila mtu anamfahamu Star huyu wa Uganda), lakini cha ajabu alijibu hamfahamu na wala hana wazo kama kuna mtu wa jina hilo anayemfahamu.

Tofauti na hilo, katika kujibu kwake, Wiz Kid alionesha Vitendo Fulani hivi ambavyo vilitafsiriwa kama Dharau.


Sasa, bada ya hayo kutokea, yalionekana kumkwaza sana Msanii PALLASO wa Uganda, ambaye aliamua kuingia kunako ukurasa wake wa Facebook na kushusha matusi haya:

HUYU NDIYE MSANII WA KENYA, ATAKAYEFANYA KAZI NA ROSE MHANDO.

2:41:00 AM Add Comment
KENYA
TRACK yake ambayo imemuweka mahali pazuri, inafahamika kwa jina la  AIRA MAGILANI ENKAI, ambayo kwa sehemu kubwa imepata Airtime Nchini Tanzania.

Jina lake anaitwa MARYANE TUHUMA, msanii wa Gospel mwenye Umaarufu mkubwa sana Nchini Tanzania kuliko Nyumbani kwao Kenya.
Ni Mzaliwa wa Eneo la KAJIADO huko Nchini Kenya, Maryane yuko Mbioni kuachia Kazi yake Mpya, akiwa amemshirikisha ROSE MHANDO kutoka Nchini Tanzania.

Awali alikuwa anasoma Chuo Cha Uuguzi, lakini aliachana na Chuo akiwa Mwaka wa tatu, ili kujikita zaidi katika Muziki wa Injili muda wote

§  Anamzungumziaje Rose Mhando
Maryane amesema kuwa, Rose Mhando amekuwa ni rafiki yake wa karibu sana, na ni kama mama yake, kwa sababu muda mwingi wanashauriana katika masuala ya Kidini zaidi


Wimbo Huo utakuwa katika Lugha ya Kiswahili na unatarajiwa kuwa Hitsong Balaa

TIZAMA HAPA: HIVI NDIVYO BINTI MLEMAVU ALIVYOBAKWA NCHINI KENYA

1:45:00 AM Add Comment

TYGA AMFUNGUKIA DRAKE. ASEMA NI MNAFIKI KWAKE. PIA HAZIIVI NA NICKI MINAJ

1:28:00 AM Add Comment
HNHH & BLACK TOUCHEZ
KAMA ni time ya Ku-ride Solo and Independent, basi ndiyo inayopatikana kwa rapper Tyga, ambaye hivi sasa yuko katika Mchakato wa kupigana Chini na Label yake ya YMCMB (Kwa mujibu wa Tweet Yake)

TTM tumenyaka mbwadidi jingine kuwa, Tyga “amefyatuka” kuwa hivi sasa haziivi na Vichwa viwili kutoka katika Label hiyo, DRAKE “Dreezy” na NICK MINAJ

Sababu kubwa ambayo imewafanya watu hawa kuchuniana, inasemekana kuwa ni baada ya Tyga kutweet kuwa YMCMB wanamuwekea “Kiwingu” katika Albam yake mpya, na anahisi itabaniwa kutoka katika Tarehe iliyopangwa

Kama utakuwa unakumbuka vizuri, tulikupa mtonyo kuwa Tyga alifikia hatua ya kutishia kuvujisha Albam nzima endapo haitaachiwa siku husika, na tayari ameshaachia mkwaju mpya, hali ambayo kama sio Game la biashara, basi atakuwa amepigana chini moja kwa moja na YMCMB.

Katika Maelezo yake, Tyga alisema kuwa hivi sasa hana mahusiano mazuri na wawili hao, na anajaribu kuwa Huru na watu ambao anaamini ni “kiwingu” kikubwa kwake.

v Hampendi Sana Drake Sababu Ni Mnafiki Kwake
Pia Tyga ameongeza kuwa, Binafsi hampendi Drake kwa sababu ni Mnafiki kwake, ingawa bado atazidi kupenda Nyimbo zake sababu anazipenda.

Aidha Tyga ameongeza kuwa, anaamini kuwa ni kama walikuwa wanalazimisha uhusiano baina yao wawili.

Na hiyo ni kwa sababu Lil wayne aliamua kuwaweka kundi moja ambalo ni YMCMB ndo maana wamekuwa wakifanya kazi pamoja lakini ukweli ni kwamba hampendi DRAKE.

v Hii Ndiyo Sababu Iliyomfanya Ajiunge Ymcmb
Katika kuzidi “Kubumbulua” mambo Mengi, tyga ameongeza kuwa, Mtu aliyempeleka YMCMB, ni Lil wayne, hivyo huyo ndiye aliyemfanya amwage wino kunako mkataba wa Kundi hilo. Hivyo sio Drake, wala Nicki Minaj aliyemshawishi ajiunge na Team hiyo iliyotesa sana na Mkwaju wa BED ROCK


 Pia tyga ameongeza kuwa, asilimia kubwa ya majembe yaliyoko YMCMB, si kusema kwamba ni marafiki wa Dhati, bali kuna wengine wanalazimisha uhusiano wa kirafiki ili wapige kazi, ukizingatia wako kundi moja

JIPYA KUHUSU NDOA YA JAY Z NA BEYONCE, BAADA YA UVUMI WA KUACHANA KUENEA

1:21:00 AM Add Comment
HNHH, Marekani
KIPINDI fulani hivi kulikuwa na info kuwa wawili wapendanao katika ndoa huku wakiwa na Mtoto mmoja, JAY Z na BEYONCE, wanazinguana vya hatari na huenda wakapigana Chini kama sio Kuachana

Sasa, Kwa Mujibu wa PEOPLE MAGAZINE, ttm tumepata Mtonyo wa Juu kwa juu kuwa wawili hao hivi sasa wanatarajia Kurenew Ndoa yao..
Jarida hilo limemwaga Mtonyo kuwa, ni kweli ndoa hiyo ilikutana na mbwadidi la migogoro kwa nafasi kubwa, lakini hivi sasa wameamua kuweka kando tofauti zao, na kulianzisha  upya Jahazi lao, ambalo walipeana ahadi kuwa watakomaa nalo mpaka lizame na wote wawe humo humo.

v Sababu Kubwa Ni Hii Hapa
Jarida hilo halikuishia hapo, bali limezidi kufyatua info kuwa, Sababu kubwa na maalum ambayo imewafanya wawili hao kufikia uamuzi huo, ni kuweka picha nzuri, pamoja na kuelekeza majeshi yote kwa mtoto wao BLUE IVY.

Aidha inasemekana kuwa, wawili hao wamegundua kuwa, Kumlea mtoto wao wakiwa pamoja na kukiwa hakuna Tofauti ya aina yoyote ile, basi italeta mazingira mazuri na malezi imara yenye furaha kwa Mtoto huyo


Wawili hao wamedhihirisha kupendana zaidi na zaidi hasa walipokuwa wakitembelea sehemu mbali mbali wakiwa na mtoto wao huyo, na inasemekana hivi sasa wako very Busy Studio, kupika ALBAM ya pamoja

MKUU WA MKOA: HAKUNA EBOLA MWANZA

2:06:00 AM Add Comment

Mkuu Mkoa wa Mwanza Injinia Evarist Ndikilo akitoa taarifa ya mkoa kuhusu kanusho la kuwepo kwa mgonjwa wa Ebola wilayani Sengerema


Na G.SENGO BLOG, Mwanza
TAARIFA zinazosambazwa kuwa kuna mgonjwa wa Ebola kagundulika wilayani Sengerema mkoani Mwanza, si za kweli.

Akizungumza na waandishi wa habari hii leo jijini Mwanza, Kaimu Mganga Mkuu Mkoa wa Mwanza Dr. Kengia amesema utafiti wa awali kabla ya majibu kamili ya vipimo unatosha kujidhihirisha kuwa mgonjwa aliyedaiwa kufariki dunia hivi majuzi Salome Richard (17) siyo kweli kwamba amefariki kwa Ebola.

Hata hivyo kulikuwa na uchukuaji wa vipimo vya awali ambapo, Majibu ya Vipimo vya awali yamepatikana tarehe 19/10/2014 saa 3:00 asubuhi

VIPIMO WALIVYOPIMA 
1. Dengue fever
2. Chikungunya Virus
Majibu ya vipimo hivyo walionekana ni Hasi (Negative)

VIPIMO VINGINE VINAVYOENDELEA 
(1) Liver function - kuangalia kama ini la mgonjwa ambaye ni marehemu lilikuwa kinafanya kazi vizuri au la.
(2) Bilirubin kuangalia kiwango cha protein kwenye ini kama kilikuwa sahihi au kimeongezeka.
Kaimu Mganga Mkuu Mkoa wa Mwanza Dr. Kengia.

Taratibu zinaendelea kati ya Mkuu wa Maabara ya Taifa na Wizara ya Afya kuhusu sampuli hii kupelekwa Mbeya au jijini Nairobi nchini Kenya kwaajili ya uchunguzi wa virusi ya Ebola au Marbug.

Awali kutokana na hofu ya ugonjwa huo huku taarifa zisizo rasmi zikizidi kusambazwa kwa njia ya mitandao ya simu na internet wananchi wa wilaya ya Sengerema na vijiji vya karibu walihaha katika vyombo vya usafiri husussani daladala wakikataa kugusana kwa kuwa Ebola imeingia Mwanza, huku wafanyakazi na wafanyabiashara wanaoishi mkoani Mwanza na kufanya shughuli zao wilayani Sengerema wakiahirisha kuelekea wilayani humo kutokana na vitisho vya taarifa walizopata.

MNADA BANNER