REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

MJANE WA MOWZEY RADIO : NIMEKWAZIKA KABISA !!!!

3:33:00 AM Add Comment

Na Hezron Munisi- UGANDA  
HAKUNA kitu kinauma kama pale ambapo mtu anaamua kutumia kipindi kigumu ulichopo kwa ajili ya kutengeneza pesa ama kutengeneza jina lake, ama kutafuta Sifa  hasa kwa watu mbali mbali

Na kinachokera zaidi, ni pale ambapo anatumia maneno makali na ushahidi usio na tija ili aendelee kuwaaminisha watu na aendelee kukukandamiza ili aingize mpunga zaidi kwake

Moja kati Ya Blog Nchini Uganda (jina tunalihifadhi) imejikuta akimuudhi na kumkwaza LILIAN MBABAZI mzazi mwenzake na Marehemu Radio kwa kumuandama na kitu ambacho hakina ukweli hasa katika kipindi hiki ambacho bado anaugulia maumivu ya Msiba wa Mzazi mwenzake.

Blogger anayetumia jina la Scoop alipost Picha inayomuonesha Lilian Mbabazi akipiga Kinywaji na Marafiki zake, na kisha kukoment kuwa imekuwa ni mapema sana kwa Bibie huyu kula bata mapema

Tunamnukuu
"Lilian Mbabazi, Mjane wa Mowzey Radio akiwa Out anapiga kinywaji na KARITAS KIRISIMBI na Marafiki wengine. Sio mapema kwake kutoka out na kula Bata, au ni muda wa kusonga mbele?"

Lilian aliscreen Shot Comment hiyo kisha akaandika
"Ka Jambo Scoop, kuchukua picha za Tangu Mwaka 2016 na kuzipost Sasa Hivi... MUSWADDE NYO"


#DakaHiiFasta : BEHIND OF AVRIL KUVAA MIWANI YA MACHO....

2:35:00 AM Add Comment

Na Joe Mwangi  
UKIMUONA Avril kama uko Very serious , ukasikia sauti yake inakuita, halafu unapomaliza kuitika, anaomba angalau "akuchumu", basi kama utakataa, we nii mgumu kuliko wanaume wote Duniani

Urembo tunaouona kwa Binti Huyu mwenye taji  lake la kuitwa "Mrembo na Msexy" kutoka kwangu, kuna muda huwa unachagizwa na Mavazi yake, Umbile Lake, nywele zake, tabasamu lake, lakini Pia MIWANI zake

Sasa kama ulikuwa hujafahamu, Avril mwenyewe anazungumzia kile ambacho kipo Nyuma ya Miwani ambayo huwa anavaa sometimes, ili kuweka sawa kwa wale ambao pengine wanatafsiri kuwa huwa ni swagg tu na anaongeza urembo.

Kupitia Instagram account Yake, Avril Mwenyewe kaweka wazi kuwa, Kitendo chake cha kuvaa miwani ya macho, kisitafsiriwe kama ni Urembo, ila huwa anatatizo la macho (Myopic) na amekuwa akifanya hivyo mara kadhaa maana hiyo ndioyo tiba ya mwisho kwake

Ukiachilia mbali hilo, Avril akaongeza kuwa , amekuwa na tatizo hilo tangu alipogundulika akiwa mtoto mdogo

KULIKONI TENA !!!! :HAKUNA JAMBO LA KHERI KATIKA URAFIKI WA CHRIS BROWN NA BOW WOW...

1:50:00 AM Add Comment

Na Baba Juti   
KWA mujibu wa kile kinachoonekana na kusikika katika Video Mpya ya BOW WOW inayofahamika kwa jina la DRUNK OFF CIROC, na kile kinachojibiwa na Chris Brown, ni dhahiri kabisa kuna namana gani vipi kati ya wawili hao

Siku ya Jana, Bow Weezy aliachia Video yake Mpya ambayo tumeitaja hapo mwanzo huku ndani yake akisikika kulalamika namna ambavyo ukaribu wake wa Swahiba wake Chris BNrown umekuwa Mbali sana tofauti na Kipindi cha Nyuma ambapo wawili hao walikuwa wakionekana Ku-Hang out Pamoja

Katika moja kati ya Lines ambazo zinapatikana katika Track hiyo ya Drunk Off Ciroc, inaashiria kabisa kuwa BOW WOW, hafurahishwi na anahisi vibaya sana kuona kama Chris Brown hamjali tena, hayuko karibu naye, na wala hamjulii hali , kitu ambacho anajiuliza maswali mengi mpaka sasa

Mashairi hayo yako hivi
"Niliacha kufanya Show ili Nikuone Chriss
Siku ya Kwanza, mie na wewe tumepitia Mengi
Hata iwe vipi, siku zote utakuwa mdogo wangu
Na inaniuma sana tunapokuwa katika uma na bado hatusemeshani
Huu ni Uchizi
Tumekua watu wazima, hebu tuachane na haya masuala"

Baada ya kukutana na Kitu Hicho Chris Brown aliamua kujibu kile alichokiona, kwa kupost kipande cha mashairi hayo huku akiandika

"Nimechanganyikiwa... Uko sawa Bro?" 

MNADA BANNER