REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

ETI NINI1?: NASI NA NICKI MINAJ WANA KA_MGOGORO?

2:40:00 AM Add Comment

Na Baba Juti   
"WatuWaMungu kuna Fununu za Chini chini kuwa Mahusiano ya Rapper Nas na Nicki Minaj kama yapo kwenye "Kaa la Moto" hivi

Kipindi cha Mwezi uliopita, nadhani Taarifa ndo ziliznza kuzagaa Rasmi kuwa Rapper Nas ndiye ambaye "anamtindua" Nicki Minaj kwa Hivi sasa, na Nicki Mwenyewe Alikiri suala hilo

Sasa, Kumekuwa na Taarifa za ndani kuwa mahusiano hayo kwa hivi sasa yapo katia Mgogoro ambao chanzo bado hakifahamiki mpaka hivi sasa

Mmoja kati ya Watu wa Karibu katika Familia ya Rapper Nas, amedai kuwa kwa hivi sasa ni kama kuna mvutano wa hapa na pale baina ya wawili hao, ingawa bado hawataki iwe hadharani

Pia ikaongezwa kuwa, kulega lega huko kumemfanya Nas aanzae kulike kila Picha ya Meek Mill ambaye ni Ex wa Nicki Minaj na hivi sasa wanatupiana Madogo ya hapa na pale

"Ni Kweli, sisi wenyewe hatufahamu, ingawa tunaona kabisa dalili za kutokuwepo kwa Mahusiano mazuri baina ya wawili hao kama ilivyokuwa Mwanzo" Kilidai Chanzo ambacho kipo karibu na Wapenzi hao.

TUPANIC KIDOGO: HILI NDILO JIBU LA FUTURE KWA JAY Z?

2:33:00 AM Add Comment


Na Baba Juti  
#WatuWaMungu tusipokaa vizuri linaweza kuripuka "Bifu" ambalo huenda likawa na Ukweli ndani yake ama Biashara Ndani yake

Album ya Jay-Z ambayo imepewa Jina la 4:44 ilizungumza mambo mengi, na moja kati ya Watu walioguswa katika Album Hiyo, ni Rapper Future ambaye hivi sasa anafanya Vizuri Pia na Mkwaju wa MASK OFF

Kama hukufahamu, Jay Z ndiye aliyeamsha kila kitu kwa kumtaja Rapper Future kama Baba ambaye hajui majukumu yake, na badala yake mtoto wake analelewa na Mwanaume Mwingine ambaye ndiye mume wa Sasa wa Ciara

Baada ya Madongo hayo kutoka na kuonekana yamemgusa zaidi Future, awali kabisa alipost Picha ya Mtoto wake akiwa naye Studio, kitu ambacho kilitafsiriwa kama Dongo kwa Jay Z

Na kama haitoshi, jana tu, Future alizama kuna Snapchat Account yake , na kupost Picha ambayo inamuonesha akiwa ameshikiria Burungutu la Madorali, na kisha kuandika kuwa, Kaka Kumbwa hana Mkwanja kama Ule

"Hauna Utamu kama Huu" aliandika Future

MNADA BANNER