REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

UTAMU WA KUCHIMBA DAWA !!!! : DESIGNEER "ANASWA" AKIKOJOA MBELE YA GARAGE BINAFSI YA MTU

1:55:00 AM Add Comment

Na Rich Sam   
#WatuWaMungu kila mmoja aseme Paaanda !! Paanda!! Paaanda !!! Paanda !!! Paaaandaaaaaa !!!, bonge la mzigo ambalo liliusumbua sana ulimwengu, wala tusiongee sana tukamaliza utamu

Wengi tumemmis Desiigner, uwongo?, maana zile kelele zake, fujo zake, mbwembwe zake, amsha zake, vituko vyake, ongea yake, huwa ni unique yaani hakuna msanii mwingine ambaye anafnaya akama anavyofanya Desiigner !!


Ila sasa, kuna hii ambayo binafsi tumeipenda na tukaona ni bora tukaiongeze katika moja kati ya vituko vyake, ingawa hatujui dhamira yake

Bwana Desiigner alibambwa na wakuda wa mambo akikojoa ama kutoa haja ndogo katika Private Garage ya Mtu aisee, kweupee bila hata kuogopa

Ingawa haikufahamika kama bwana Desiigner alikuwa amebanwa sana mpaka ikamlazimu kusimamisha gari lake aina ya Lamborghin na kujibanza sehemu achimbe dawa, ama ilikuwa ni makusudi, ila wengi wamestaajabishwa sana na tukio hilo

BACK AGAIN ?: TUTARAJIE TAARIFA "TAMU" KUTOKA KWA JANET JACKSON NA JERMAINE DUPRI

1:11:00 AM Add Comment

Na Rich Sam   
#WatuWaMungu inawezekana kabisa kukawa na jambo kubwa ambalo tunatakiwa kulitarajia kutoka kwa ma-ex wawili ambao walikuwa na mahaba ya dhati kipindi chao cha "mahusiano"

Kwa mujibu wa Taarifa kutoka kwa chanzo muhimu kabisa cha familia ya Janet Jackson, inasemekana ni kweli na hakika Janet na Jermain Dupri wameamua kurejesha kile ambacho kilikuwepo kipindi cha nyuma.

Kama utakuwa unafuatilia vema maisha ya wawili hawa, haikuwa mapenzi tu ndani ya maisha yao, bali pia kulikuwa na kazi ambapo Jermain Dupri alikuwa akimsimamia Janet jackson katika kazi zake na hata kumfikisha Sehemu mbili

Chanzo hicho kimeongeza kuwa, Urafiki wa wawili haop kwa hivi sasa, umekuwa ni wa karibu kuliko kawaida, hivyo muda wowote linaweza kutokea la kutokea na taarifa zikaja njema zaidi

" Jermain ni mtu muhimu sana kwa Janet, maana tangu amekuwa katika wakati mgumu, yuko naye karibu, na hicho ndicho ambacho Janet huwa anakipenda zaidi kutoka kwa Jermain. tusubiri tu, maana urafiki wao ni zaidi ya urafiki wa kawaida kabisa"

JAMANI !!!: MWANAMKE ALIYEPIGA PICHA ZA UJAUZITO WAKE UKIWA UMEZUNGUKWA NA NYUKI 20,000, AMETOA TAARIFA YA KUUMIZA !!!!

12:58:00 AM Add Comment

Na Rich Sam   
#WatuWaMungu jumatatu inabidi ianze na Story hii ambayo inashtua lakini sijui ni nini kimesababisha mpaka ikafikia hapa ilipofikia.

Kama utakuwa ni mfuatiliaji mzuri, utakuwa umekutana na hii taarifa ambayo iliwaacha kinywa wazi watu wengi baada ya mwanamke mmoja kutoka OHIO , marekani , anayefahamika kwa jina la EMILLY MUELLER (33), kuamua kupiga Picha, yaani Photoshoot ya Ujauzio wake, akiwa amezungukwa na Nyuki zaidi ya 20,000 katika Tumbo lake, yaani katika ujauzito wake.

Mwezi August, Bibie huyo ndipo aliweza kusambaa katika vyombo mbali vya habari kwa kitendo hicho, ukizingatia yeye ni mfugaji mzuri tu wa Nyuki

Lakini jambo ambalo limekuja kutokea, ni kwamba kupitia Facebook account yake, Emilly alipost taarifa kuwa Mtoto ambaye alikuwa tumboni kipindi ambacho wanapiga Picha, hakutoka Hai kama ambavyo walikuwa wametarajia, kitu ambacho kiliwauma sana yeye na mume wake

Emilly aliandika kuwa, awali yaani ndani ya week 28, hakuhisi mtoto akicheza tumboni, lakini alihisi labda amelala. lakini hali ikaendelea hivyo hivyo, na ndipo walipoamua kwenda Hospitali. Licha ya madaktari na manesi kujitahidi kwa kadri wawezavyo, hali haikubadilika na ndipo alipozaliwa mtoto akiwa amefariki.

Ingwa haijawekwa wazi kama Nyuki wale walizua tatizo lolote kwa Mtoto aliyekuwa tumboni, bado Emilly anaamini kilichopangwa na mungu ndicho hicho hicho.

Hata hivyo ana watoto watatu.



UPO HAPO!!!!? : ETI DADA YAKE NA SERENA WILLIAMS, VENUS, ANA MKOSI NA WANAUME, SAFARI HII KAANGUKIA KWA "BWABWA"

12:18:00 AM Add Comment




Na Baba Juti  
#WatuWaMungu Kuna fununu Tumezinyaka kuhus Dada Yake na Serena Williams ambaye pia ni msakata Tenis kwamba linapokuja suala la wanaume kwake, ni kama kuna ka-mkosi hivi maana huwa anaangukia pabaya 

VENUS WILLIAMS (37) ambaye anashikiria namba 5 katika Ubora wa Tenis kwa wanawake inasemekana amekuwa na kasumba ya kupata Boyfriend ama Mpenzi ambaye  anakuwa kamili na yuko serious katika suala zima la mahusiano

Sasa Kali zaidi imeibuka baada ya kubainika kuwa safari hii yupo katika mahusiano na jamaa ambaye ni "Shoga" kitu ambacho kimewastua watu wengi sana, ingawa haifahamiki kama Venus anafahamu hilo ama kuna namna ambavyo imekuwa.

Katika Shughuli a.k.a Harusi ya Mdogo wake , Serena Williams ambaye ameolewa hivi majuzi na kufunga Ndoa Rasmi, Venus alionekana akiwa na jamaa huyo na alimtambulisha kama "Mpenzi" wake mpya, huku baadhi ya watu ambao wanamfahamu vizuri, wakianz kunong'ona kuwa yule jamaa sio RIZIKI

OH MY GOD !!!! : INAWEZEKANA PUA YA JANET JACKSON IKAHARIBIKA MUDA WOWOTE

1:48:00 AM Add Comment

Na Rich Sam    
KWA Mujibu wa Jicho la Mtaalamu wa Masuala ya Upasuaji wa kuboresha Muonekano, Pua ya Janeth Jackson inaweza kuharibika Muda wowote

Kauli hiyo imetoka kwa mtaalamu huyo anayeitwa Dr. MATTHEW SCHULMAN ambaye ana jina kubwa kwa shughuli yake hiyo hiyo katika Jiji la New York

Dr Schulman ingawa sio yeye ambaye kamfanyia Upasuaji wa Pua Janeth Jackson, lakini anaamini kuwa Msanii huyo mkongwe katika tasnia ya Muziki wa R&B na Pop anaweza kukumbana na hali hiyo na tayari dalili zimeshaanza kuonekana mapema hivyo anatakiwa kuwa makini sana

Kukazia Zaidi, Daktari huyo kasema kuwa, inawezekana kabisa kuwa Vipodozi anavyotumia Janeth Jackson, haviendani na havikubaliani na aina ya upasuaji aliyofanya Bibie huyo, nahilo aliliona katika Picha za Red Carpet ya OUT100 Gala’s Music Icon Awar, ambapo pua yake ilikuwa haijakaa sawa kabisa.

Tunamnukuu
 Inaonekana kuna kuharibika kwa Pua na kukaa vibaya kwa pua katika muonekano wa maumbile ya Pua. Hii inaweza kutokana na kufanyiwa upasuaji waPua mara kwa mara na huenda kuna maumivu ambayo alipata, na hii pia huchangiwa na aina ya Vipodozi ambavyo anatumia"

KUDADEKI !!! : SAFAREE SAMUELS ANAUHITAJI UTAMU WA NICKI MINAJ TENA

1:06:00 AM Add Comment

Na Baba Juti   
KAMA kweli ni kubaniana, basi inawezekana Safaree Samuels alibaniwa vitu vingi sana na aliyekuwa Mpenzi wake kipindi kileeee, Nicki Minaj, na ndio maana uvumilivu umemshinda kiukweli

Zaidi ya Masaa Matano yaliyopita, Safaree Samuels alioneshwa kushindwa kuvumilia baada ya kuona Utamu ambao Nicki Minaj anauonesha sasa hivi , na wala hakuwa kumuonesha kipindi kile wako pamoja katika Mahusiano yao

Safaree alipost picha ya Front Cover ya Jarida la PAPER ambalo Nicki Minaj alionekana kuwa Mbele zaidi kwa picha ambazo zinamfanya kila mtu atoe mimacho na mate ya kutosha

Picha hiyo inamuonesha Nicki Minaj akiwa katika Positions tatu tofauti ambazo zilionekana kumchanganya sana Ex wake huyo ambaye waliachana kwa vimbwanga vya hali ya juu

aliandika Hivi
"tunaweza kugundua Kitu hapa tafadhari?, hizi ndizo aina ya picha ambazo  kila mara nimekuwa nikitaka uzipige kwa ajili yangu ! Wow.... "

UPO HAPO !!!!?: RICK ROSS AUNGANA NA WAANDAMANAJI PHILLADEPHIA KUPINGA HUKUMU YA RAPPER MEEK MILL

12:46:00 AM Add Comment

Na Baba Juti   
Watu Wa Mungu, Sasa mambo yameanza kuwa na uzito idogo ikiwa ni baada ya kutolewa Hukumu ya Rapper Meek Mill.

Hali imekuwa sio shwari katika Mji wa Philladephia Nje ya mahakama ya Mji huo, ikiwa ni baada ya Wananchi na mashabiki wa Rapper Meek Mill kwa wingi kujitokeza na kuanzisha Maandamano ili kupinga Hukumu yake

Kuanzia November 13, Supporters hao waliingia Mtaani na kuanza kupinga hukumu ambayo imempata Meek Mill huku wakidai kuwa kumekuwa na ukandamizaji wa hali ya juu hasa katika Maamuzi ya mahakama huku Masuala Binafsi yakiwa ndani yake sanjari na ubaguziwa Rangi

Yote Tisa, Kumi ni baada ya Rapper Rick Ross naye kuamua kuingia mtaani kuungana na waandamanaji hao ili kuhakikisha kabisa kuwa haki kwa msanii ambaye yuko Chini ya Records label yake, anapata haki ya Msingi

Basi Nne kubwa zikiwa na ujumbe wa "SIMAMA KWA AJILI YA MEEK MILL" zilionekana zaidi ya Mbili katika Bara bara tofauti, zikiwa na shughuli moja tu, kupinga hukumu ya Rapper Huyo

UKIMWAGA MBONGA.......: BAADA YA JUSTIN BIEBER KURUDIANA NA SERENA GOMEZ, HATIMAYE THE WEEKEND AMCHUKUA EX MWINGINE WA JUSTIN BIEBER

1:40:00 AM Add Comment

Na Rich Sam   
Watu Wa Mungu Msanii The Weekend ameamua kuuthibitisha Ule Usemi wa "Ukimwaga Mboga, Namwaga Ugali", na hali halisi iko Hivyo tena hadharani sasa Hivi

Kama utakuwa una kumbu kumbu swadakta kabiosa, Baada ya Justin Bieber kuachana na Srerena Gomez kipindi cha Nyuma, The Weekend aliamua kuchukua nafasi hiyo na mahaba yakawa Mahaba Kweli kiasi kwamba wengi tukaamini mabo yataenda vizuri sana

lakini Mwezi uliokata, iliibuka taarifa kuwa Serena Gomez ameapigana Chini na The Weekend , kama haitoshi ni kama karudisha mahaba yake kwa aliyekuwa Mpenzi wake, JUSTIN BIEBER, na hivi sasa wako karibu sana

Sasa Bwana, Usiku wa Kuamkia Jana, The Weekend naye ameamua kujibu mapigo  kwa kuamua kujiweka kwa Ex- wa Justin Bieber anayeitwa YOVANNA VENTURA

Yovanna ambaye ni mwanamitindo kutoka Miami, alikuwa ndani ya Mahaba Mazito na Bieber kipindi ameachana na Serena Gomez , wakati huo Pia Serena alikuwa ameshaopolewa na The Weekend

Wawili hao walinaswwa pamoja usiku wa manane wakitokea kunako kiwanja kimoja kinachoitwa HYDE, ambapo Wawili hao walikuwa wamekaa Seat ya Nyuma ili wasionekane


Hata Hivyo inadaiwa kuwa, The Weekend na Ex- wa Bieber walikuwa pamoja pia katika Birthday party ya French Montanah huko Beverly Hills, NOVEMBER 9, na walikaa pamoja kwa kila u=ishara ya mahaba mpaka Usiku wa manane ambapo waliondoka pamoja pia na kuelekea kusikofahamika

KWISHA MANENOOOOO: KI-BEN-TEN CHA MARIAH CAREY NDICHO KI-MENEJA CHAKE KWA HIVI SASA !!!!

1:14:00 AM Add Comment

Na Baba Juti   
Oh My God !!!, Watu Wa Mungu sijui kama mtaitafsiri kama ni Good News ama Lah, lakini hali halisi iko Hivyo waungwana

Siku Kadhaa zilizopita, Msanii  Mkongwe wa Muziki wa R&B na POP, MARIAH CAREY, aliamua kupigana Chini na Meneja wake wa Muda Mrefu, STELLAH kutokana na namna ambavyo ukiukwaji wa makubaliano yao ilikuwa ukifanyika hasa katika Misinging ya Kazi.

Ingawa haikuwekwa wazi hasa katika Mandishi, pia haikufahamika zaidi ni nini hasa kilisababisha wawili hao kuacha kufanya kazi kwa pamoja, lakini vyanzo vya karibu vinadai kuwa, Boy Friend wake, yaani ki-Ben Ten chake Mariah Carey, Byan Tanaka ndiye chachu ya kuvunjika kwa Wawili hao

Kilichokuja kudhihirisha zaidi kuwa Ni Kweli Brian Tanaka ndiye chanzo cha kila Kitu, ni Mara Baada ya Mariah Kumtangaza Rasmi Boyfriend wake huyo kuwa ndiye Msimamizi wa kazi zake na Fani yake Kiujumla

Katika kukazia Zaidi, Ikatoka taarifa kuwa, katika makubaliano yao, Bryan Tanaka atakuwa analipwa USD 12,000 kwa Wiki sawa na Tshs. 27,420,000

Aidha mmoja kati ya Wahusika kunako Management ya Mariah Carey, aliweka wazi kuwa, Mwisho wa Mariah Carey na Brian Tanaka, ni kama Mwisho wa Kelvin Ferdeline na Britney Spears.

Tunamnukuu
"Mariah Carey ni Msanii na Brian Tanaka ni Back Up Dancer Wake. Hata kama taeandelea kumsimamia, Brian hajui lolote kuhusu Managerment ya Muziki na masuala ya Muziki na kumsimamia Msanii ambaye ana taswira kubwa kwa Dunia.... hata hivyo, Brian amekuja kuharibu kila kitu katika Muziki wa Mariah Carey na maisha yake kiujumla"

OH MY GOD !!!: FETTY WAP ANATARAJIA KUFIKISHA IDADI YA WATOTO 8

12:42:00 AM Add Comment

Na Baba Juti    
Watu Wa Mungu kuna kitu ambacho binafsi natamani kufahamu pia kutoka kwenu kwa sababu vitu hivi vinahitaji  uzoefu kidogo.

Rapper Fetty Wap inawezekana kabisa baada ya kuona kama soko la Muziki limeanza kuwa na changamoto kubwa sana kwake, sasa ni bora zaidik kuwekeza katika Watoto ama familia.

Kwa mujibu wa Taarifa ambazo tuko nazo mpaka Hivi sasa, Rapper Fetty Wap ambaye ana Umri wa Miaka 26 kwa Hivi sasa, anatarajia kupata watoto wengine wawili , wa kike na wa kiume, ambapo atakamilisha Idadi ya Watoto Nane ambapo Sita alionao hivi sasa ndio wanaotambulika

Awali Hitmaker huyo ambaye aliukunjua Ulimwengu kupitia Track yake ya TRAP QUEEN, aliingia katika Mgogoro mzito na Mzazi Mwenzake MASYKA baada ya kudaiwa kuukataa ujauzito miaka kadhaa iliyokata, lakini baadaye mambo yalienda Fresh

Ukiachilia mbali Masyka, Fetty Wap pia ana mtoto na wanawake wengine ambao ni Lezhae Zeona, Lez na Alexis, na mtoto wa kike anayesubiliwa, ni kutoka kwa mwanamitindo ALEXIS SKYY na yule wa kiume, haifahamiki ni kutoka kwa nani.

UPO HAPO!?: REMY MA KASEMA KUWA HUWA HAMFIKIRII MSANII YEYOTE AKIWA ANAANDIKA WIMBO, MAANA HAILETI MAANA YEYOTE KWAKE

12:59:00 AM Add Comment

Na Rich Sam  
WATU Wa Mungu kama mmepata Bahati ya kusikiliza Brand New Sh**t ya Remmy Ma Na Lil Kim, basi kuna namna ambavyo utakuwa uatafakari hasa kile ambacho umekisikia  ndani yake

Collable hiyo ambayo imepewa jina la WAKE ME UP ilikuwa ikisubiriwa kwa hali na mali, ukizingatia REMY MA na LIL KIM ni Wakongwe na wana historia zao katika Upande wa Hip Hop kwa Wanawake, maana hata Uzito wa Mashairi yao huwa ni balaa kupita maelezo

Lakini baada ya Kuachiwa, kuna baadhi ya waungwana walipongeza kile kilichofanyika lakini kama kawaida ya wengine, waligundua makosa mengi na hata kudai kuwa Mzigo huo sio mkali hata kidogo maana hakuna ukubwa wowote

Baadhi walianza kumponda Remy Ma wa sasa Hivi na Lil Kim wa sasa hivi wakidai kuwa Makali yao ya kipindi cha Nyuma yamepewa changamoto kubwa sana na kizazi kipya cha Female Emcees.

Sasa kubwa zaidi, watu walidai kuwa, Mkwaju huo moja kwa moja umemlenga Nicki Minaj ukizingatia wote wawili, yaani Remy Ma na Lil Kim waliwahi kuingia katika Msuguano mkali sana na hata hivi sasa bado kuna kila chembe chembe ya uhasama Juu yao

Katika kuliweka Sawa Jambo Hilo, Remy anadai kuwa ameshachoka kusikia kuwa kila baadhi ya Track atakazofanya zinamdiss Nicki Minaj. Hata kama ameshirikiana na Lil Kim, bado anavutiwa na namna ambavyo wawili hao wamefanya kazi. Hivyo kwa upande wake, akiwa anaandika wimbo na hata kuurekodi mpaka kuuachia, huwa hamfikirii msanii wa kike ama kumchana mtoto wa kike. yeye anachokifanya, ni kile ambacho wasanii wengi kama vile Jay Z, J Cole, Kendrick Lamar na wengine watamsifia na kusema kuwa , daah huyu Demu ni balaa. Hivyo huwa hafikirii kabisa Jinsia yoyote ile hasa ya Kike, sababu haileti Mantiki yoyote Kukichwa Chake

HUYU NDIYE MWAFRIKA SASA !!!: LUPITA ACHUKIZWA KUFANYIWA PHOTOSHOP

12:23:00 AM Add Comment

Na Baba Juti  
KAMA kuna baadhi ya Binadamu ambao wanavutiwa sana na Photoshop na hata kulazimika kufanya kila wawezalo ili wawe na muonekano tofauti na wa kwao, basi hii ni tofauti kwa Bini huyu ambaye ana asili ya Kenya

Mkali w Filamu kutoka Hollywood, LUPITA NYONG'O ameamua kung'aka vya kutosha baada ya Jarida GRAZIA UK kumfanyia Editing ambayo hakufurahiwa nayo katika Front Cover yao.

Kwa mujibu wa amalalamiko ya Lupita Nyong'o ambaye alivuma sana kunako Filamu ya 12 Years A Slave, Jarida hilo lilimuomba kwa ajili ya kuonekana katika ukurasa wa mbele kabisa , na yeye hakuona hiyana, ila wamemchefua zaidi baada ya kumfanyia Photoshop ambayo anaamini kabisa imeuficha uhalisia wake

Lupita aliongeza kuwa, Wahusika wa jraida hilo, waliweka Ngozi ya Kung'aa sana tofauti na Ngozi yake ambayo ni Nyeusi kiuasilia, lakini pia walimfanyia photoshop kwenye muonekano wa Nywele zake, kwa kuondoa zile alizokuwa nazo, na kubadilisha kabisa kwa kuweka za kwao ambazo walizitaka, kitu ambacho hajavutiwa nacho hata kidogo

Lupita ameongeza kuwa , ingawa hakupewa taarifa za kufanyiwa marekebisho hayo, bado hatokubali hata kidogo kwa baadhi ya watu wachache wanaojaribu kuficha urithi wa mtu hasa kiuasilia maana ni kama kupoteza ukweli na kujaza watu uwongo

NYOTA NDOGO. " KUSERMA KWELI, MIMI HUWA NINALALA NA NGUO...NINAOGOPA SANA"

2:20:00 AM Add Comment

Na INSTA COP.
WatuWaMungu Binafsi yangu siwezi kuruhus Eti Mke Wangu alale na mie kitanda kimoja , halafu awe amevaa nguo, hata kama ni nidhamu, aibu na heshima kiasi Gani. Lazima tu uzishushe

Lakini kwa Msanii kutoka Nchini Kenya, ni Tofauti, yeye kadai kuwa, Huvaa Nguo akilala na hata akiingia Toilet a.k.a Chooni, basi lazima achunguzi kwa Umakini zaidi, maana anweza kutana na ambalo halikutaniki

Aliandika Hivi
"Hebu niwaulize.maisha ya sasa unayaonaje hasa kwenye ndoa ama hata mpenzi wako na mitandao hii? Je upo huru na mume wako? Unaweza kutembea nyumba nzima bila nguo mukiwa nyie wawili? Nimeona mitandao yakijamii watu wakikosana unapata mume anatoa picha za mke wake kwa mitandao siri nje yani sikuizi mkikosana utu pia hakuna yote mliokua mukiyafanya pamoja yanakua nje.MUNGU ailinde ndoa yangu but sitawadanganya mimi ulala na nguo.nikienda chooni nachungulia kila sehemu kabla kukalia hio choo nimezidi ama? Je unakua muoga kama Mimi? Naogopa bure?"

MAMBO YA UTALII !!!: WASANII WA ARUSHA WAKUTANA NA MKUU WA MKOA (PICHA)

1:58:00 AM Add Comment

Na Baba Juti
WASANII Wa Muziki wa aina tofauti kutoka Jijini Arusha, wamekutana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha , Mheshimiwa Mrisho Gambo kuzungumza masuala yao ya Muziki na kuhamasisha Utalii.

Kupitia account ya Instagram ya Mkuu wa Mkoa Huyo, Mhe. Gambo alifafanua kuwa kwa alikutana na Wasanii hao akiwemo DOMO KAYA, JCB na wengine kuzungumzia namna ambavyo wanaweza kuhusisha Muziki wao wanaoufanya na Kutangaza Utalii wa Nchi ya Tanzania hasa Mbuga za Wanyama

Tukio hilo lilifanyika Jana katika Ofisi yake huku akidai kuwa, amewaambia waandae andiko Maalum na bora ambalo litaainisha namna ambavyo watautangaza utalii wa Ndani hasa ikiwemo Mbuga mbali mbali za Wanyama

Kwa Upande wake Msanii wa HIP HOP Nchini Tanzania, Domokaya, naye alisistiza kukutana kwao na Mkuu wa Mkoa huyu, huku akiwasihi wasanii pia kujikita katika Sekta ya Utalii ili kuangalia namna ambavyo unaweza kutangazika katika mataifa mengine hasa kupitia Muziki wao








BAADA YA KUKAMULIWA "NDIMU" KUHUSU KUCHEZA NA MWANAUME ALIYEBADILI JINSIA NA KUWA MWANAMKE, HATIMAYE RAPPER DESIIGNER ATOA UFAFANUZI (VIDEOS)

12:59:00 AM Add Comment

Na Rich Sam   
WAUNGWANA Bwana, waliamua kumuanzishia kwa Mara Nyingine Rapper Desiigner baada ya siku kadhaa kumtuhumu kuwa jamaa ni mkali wa Ngoma moja tu, na kwisha Habari yake.

Lakini Hivi majuzi tena, Desiigner aliingia katika Kashfa Nzito kwa kubainika kuwa alicheza na Dume lililojibadilisha Jinsia na kuwa mwanamke, linalojulikana kama SIDNEY STAR, walipokuwa kunako moja kati ya viwanja vya bata

Sasa, baada ya Video kufika mikononi mwa watia Ndimu, walianza kumshambulia Vilivyo bwana Desiigner huku wakidai kuwa safari yake inaelekea mwisho , wengine wakisema kuwa huenda alillitindua Usiku wake, huku wengine wakisema sasa wasanii wanaofulia wanaanza kufukuzia wanaume waliobadili jinsia na kuwa wanawake na mwisho wa siku wanaaibika kama ilivyokuwa kwa Bobby Valentino

Ili kuliweka sawa jambo hilo, Desiigner aliamua kujirecord kunako Video Clip na kudai kuwa, binafsi yeye hakuwa anafahamu kama Yule ni mwanaume aliyebadili Jinsia na kuwa mwanamke, bali alimfuata tu kama Shabiki na kucheza naye, ukizingatia yeye ni mtu maarufu, hivyo watu wa aina mbali mbali ambao humfuata, hawezi kuwachunguza histroia zao hasa wanapokuwa Club au kazini

IMEFICHULIWA !!!: SEAN KINGSTON ATHIBITISHA KUWA ALIWAHI KUWA NA MAHUSIANO YA KIMAPENZI NA SERENA WILLIAMS KIPINDI CHA NYUMA< NA NDIYE MTU MAARUFU KUTOKA NAYE

12:41:00 AM Add Comment

Na Baba Juti
SEAN KINGSTON kaamua kuanika kile ambacho watu wengi tulikuwa hatukifahamu katika Maisha yake ya Umaarufu na kadharika.

Hitmaker huyu wa "Beautiful Girls" , amedai kuwa katika maisha yake ya kutinduana , ameshawahi kupita na Bibie SERENA WILLIAMS ambaye ni Mcheza Tenis hatari sana kwa upande wa wanawake hapa ulimwenguni.

Akizungumza kwa Ujasiri kabisa, Sean Kingston ambaye Hivi sasa yupo katika Mahusiano ya kimahaba na Mwanamitindo Angela, alidai kuwa, alipata angalau nafasi ya kufurahia naye, japo Serena alikuwa ni Mtu wa gharama sana na alikuwa akinunua vitu vya kampuni yenye gharama

Kingston anaongeza kuwa, hakuona tatizo kutumia Mijihela mingi sana zaidi ya USD Milioni 300 kwa Serena hasa kunako Maduka ya NIKE na kadhalika, maana alikuwa bado ni Mdogo kipindi hicho na alikuwa akispend tu bila mpangilio.

Tunamnukuu
"Alikuwa akipendelea Kuvaa vitu vya gharama, na alikuwa akivaa Mavzi ya Kampuni ya NIKE. na unajua ni nini,nilipokuwa nikienda naye sehemu yoyote, halafu nikatoa kadi yangu ya benki, alikuwa akinipiga mkono na kuniambia niirudishe Mfukoni kadi hiyo, ila nilikuwa nikimuambia, Ooh, Miss Serena Williams, endelea na kile unachotaka kufanya....."

Lakini ukiachilia mbali suala Hilo, Sean Kingston bado kamsifia Serena hasa kipindi ambacho alikuwa akimjali sana wakati yupo katika matatizo, ikiwemo kulazwa Hospitali na Serena alikuwa akija kwa Takriban siku saba mfululizo kumjulia hali.

Pia akaongeza kuwa, Namkubali sana kwa yale ambayo alimfanyia, na bado ni rafiki yake na anajivunia kuwa Serena anafurahia hivi sasa maisha ya Ndoa na familia Nzima kiujumla

YAMEFIKIA HAPA !!!!: KANYE WEST KUANZISHA MTANDAO WAKE WA KU-STREAM ILI KUCHUANA NA TIDAL YA JAY Z

12:13:00 AM Add Comment

Na Baba Juti   
#WatuWaMungu Hatimaye inaanza kudhihirika Rasmi kuwa ukaribu ama mahusiano ya Wawili ambao walifanya vziuri kabisa kunako soko la Muziki wa Hip Hop, yanaelekea kupotea rasmi na kuingia katika uhasimu wa hali ya Juu.

Hapa namzungumzia Rapper Jay Z pamoja na Kanye West, ambao waliingia katika uhasama wa hali ya juu huku kila mtu akimtuhumu mwenzake kwa kuanzisha noma hilo

Sasa, Taarifa ambayo tuko nayo ni kwamba, Kanye West ameamua kufungua Mtandao wake wa huduma za Kustream Muziki mbali mbali kwa dhumuni la kupambana na TIDAL: ya JAY Z

Licha ya kuwepo kwa taarifa rasmi kuwa, Jay Z na Kanye West watahusika katika mazungumzo ya moja kwa moja yaani face to face ili kuondoa tofauti zao ambazo zingeathiri mtandao wa TIDAL ambapo Jay Z alimjumuisha Kanye West pamoja na Nyimbo zake kwa ajili ya huduma za kustream, lakini Mambo yamekuwa tofauti baada ya Kanye West kutangaza ujio wa Huduma yake mpya mabyo inaashiria kuchuana vikali na Jay Z

Katika hatua ambayo haikutarajiwa, Kanye West alitangaza Rasmi kuanzisha huduma hiyo ambayo itaitwa YEEZY SOUND

YEEZY SOUND itajihusisha na masuala ya Recording, Kupromote Muziki, Videos na Audio, lakini pia huduma ya Kustream, na mengineyo

WEDNESDAY 08TH NOVEMBER : X-RAY DAY

12:50:00 AM Add Comment

DAYS OF THE YEAR  
If the hand be held between the discharge-tube and the screen, the darker shadow of the bones is seen within the slightly dark shadow-image of the hand itself… For brevity’s sake I shall use the expression ‘rays’; and to distinguish them from others of this name I shall call them ‘X-rays’.
РWilhelm R̦ntgen

In 1895 there was an incredible discovery made, one that would utterly change the way we looked at the human body, both literally and figuratively. On the back of this discovery, a million new technologies would be developed in the areas of medicine, security, and much more. The man who discovered all this? Wilhelm Röntgen, and as a result, he may just be one of the most important men in medical history. X-Ray Day celebrates his discovery and everything that’s come from it.

    History of X-Ray Day   
The X-Ray was discovered by accident, as part of an experiment where Wilhelm was attempting to ascertain whether or cathode rays could pass through glass. Nearby there was a chemically coated screen, and from it was emanating an odd glow, and dubbed the rays causing that glow X-Rays. Why you ask? Because he didn’t know what they were, so the ubiquitous ‘X for unknown’ was utilized. They’ve been called X-Rays ever since.

So what are x-rays really? They’re energy waves of electromagnetism that act in much the same way light rays do, but with an incredibly short wavelength. 1,000 times shorter than those of light to be precise. Once he discovered them, he began experimenting extensively with them, determining what they could and couldn’t pass through, and how they could be photographed. It was through this that he discovered that lead absorbed it almost completely, and human bone would stop it, creating a new and innovative way to see what was going on inside the human body.

X-Rays were used extensively during the Balkan War to locate shrapnel, bullets, and broken bones in soldiers in the field. X-Rays were used extensively in things like shoe-fittings until it became apparent that it wasn’t all fun and games. Now they’re used for things like security at airports, material analysis, and more, but with much more attention to safety.

  How to celebrate X-Ray Day   
The best way to celebrate X-Ray Day is to research X-Rays and what they’ve done for us. Then you can sit down and try to think of all the different ways that x-rays are used in modern living.

MNADA BANNER