REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

INSTACOP:ETI DULLY SYKES ANAPENDA KUHONGWA

3:57:00 AM Add Comment

JANA Katika Mtandao wa Instagram, kulizuka Mopja ya info ambayo Kitengo Chimbua Chimbua kiliweza kuinyaka na kuibeba kabla haijafutwa..iko Hivi..

Kupitia account ya Instagram inayoitwa USIPOJIPANGA NITAKUPANGA, kulipostiwa Madai ya Bibie Mmoja anayefahamika kwa Jina la Brina, na kudai kuwa, alikuwa na mahusiano naye ya Kimapenzi kuanzia Mwaka 2010, ila Mwaka jana wakapigana Chini na Mkali huyo wa kabinti SPECIAL.

Aidha bibie huyo aliendelea  kulalamika kuwa, baada ya kupigana Chini na Dully, basi Dully akaanzisha mahusiano na dada Mwingine anayefahamika kwa jina la BWEDAH ambaye eti inasemekana ni Mke wa Mzungu mmoja, na ndiye aliyelengwa zaidi kwenye Track ya KABINTI SPECIAL

Kitu ambacho kilikuja kushtua TTM, ni ile kauli kutoka katika Post hiyo, kuwa DULLY anapenda Kuhongwa, ndio maana alipigana Chini na Mlalamikaji (BRINA), kuamua kuanzisha mahusiano na BWEDAH ambaye huenda akawa vizuri kimkwanja maana yuko na Mdhungu.


BAADA ya Comments Kibao, Hatimaye Dully alijitokeza kunako account yake ya Instagram, na Kupost Picha Bibie Huyo BWEDAH, na kuandika  yafuatayo

#ROHO #YANGU #MZEE #KASAMPAIDER # KABINTI #SPECIAL @ BWEDAH_MALANGA

CREDIT (ISTAGRAM @ usipojipangantakupanga/@princedullysykes)

T.I KUFUNGULIWA MASHTAKA KWA KUDHURUMU VIFAA VYA JUKWAANI.

3:51:00 AM Add Comment

MDUDU wa Kesi unazidi kuwatafuna baadhi ya wasanii wenye majina makubwa Duniani…

BAADA ya Kitengo Chimbua Chimbua Kushusha Ishu ya R.Kelly kushtakiwa, Once Again mzigo unahamia kwa Rapper T.I, ambaye na yeye anakabiliwa na Kesi ya Dhuruma Dhidi ya Vifaa vya Jukwaani, alivyokodi kwa ajili ya Tour

Aidha Mitonyo inazidi kushuka kuwa, kuna kampuni Moja ilimpatia Vifaa kwa ajili ya Tour ya AMERICA’S MOST WANTED ambayo ilihusisha Vichwa Vikali pia akiwemo YMCMB Boy LIL WAYNE, pamoja na wengineo Kibao

Kampuni hiyo, iliongeza Kuwa, T.I aliweza kulipia Gharama za kukodi Vifaa Hivyo, ambayo ni USD 50,000 sawa na Takrimbani Tsh Milioni 80, lakini wakati wa kurudisha, hakuweza kurejesha SCREEN inayofahamika kwa jina la ROLL DROP inayosadikiwa kuwa na  Gharama kubwa, na ilitumika kuonesha Picha Kwa Jukwaa.


Tofauti na Hilo, kampuni hiyo, imedai kuwa inafungua Mashtaka ya Dhuruma ama Wizi dhidi ya T.I, na anatakiwa Kulipa Kiasi cha USD 100,000 ambapo USD 50,000 ni gharama za Kukodi, na USD 50,000 ni muda ambao T.I amekaa nayo na ni Fidia ya kupoteza kipato ambacho kingeingia

R.KELLY KUFIKISHWA MAHKAMANI ENDAPO HATOLIPA DENI

3:26:00 AM Add Comment

R.KELLY aliyewahi kuusumbua Ulimwengu wa R&B kipindi kileeee..na hivi sasa amekuwa ni Zilipendwa, yuko katika Kuti kavu la Kushtakiwa na aliyekuwa Meneja wake kipindi anapiga Mzigo

TTM tumeshushiwa Ripoti na Kitengo Chimbua Chimbua, Mwaka jana, Robert Kelly aliyevunja hasa na Kwaju la STORM IS OVER, alipigana Chini na manager wake, DERREL McDAVID, ambaye amedumu naye Miaka na Miaka

Sasa Ripoti hiyo inazidi kujieleza kuwa, Meneja huyo mstaafu, ameamua kufungua mashtaka Dhidi ya Mkali huyo wa kitambo. Kwa madai kuwa anamdai takribani USD MILION 1 na Uchafu.

Kwa mujibu wa kumbukumbu za Mkataba, inasemekana kuwa, R. Kelly aliahidi kumlipa McDavid USD Milion 1.3 ambazo ni sawa na zaidi ya Bilioni 2 za Kitanzania, lakini badala yake alimlipa USD 300,000 na mpaka hivi sasa wanazungushana kuhusu Kiasi kilichobaki.


Kutokana na hayo, Ex Manager huyo ameamua kufungua Mashtaka ya madai dhidi ya Kiwango kilichosalia.

MNADA BANNER