REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

CHECK HOW MODEL NAOMI CAMPBELL SUFFERED ALOT TO MAKE HERSELF FIT IN THIS FASHION

7:37:00 AM Add Comment

During a relatively quiet night for fashion fails and major style slip-ups at this year's Glamour Women of The Year Awards, it was supermodel Naomi Campbell who was left blushing after suffering an awkward wardrobe malfunction.

Wearing a daring red and black feathered Alexander McQueen creation, the model, who scooped the TV Personality award on the night, found the dress coming undone at the back at one point during the night.

Which isn't totally surprising considering it looked like it might have been put together in a Year 10 Textiles class. JOKES.
But fortunately nice guy Grimmy was on hand to help the glam 44-year-old fix it, despite people overhearing her asking her team to piece it back together with sellotape.


And later that evening she was pictured posing up a storm with the Radio 1 DJ and fashion designer Henry Holland as she clung onto her glass award, so style crisis averted.

See MorePhotos




MIKOANI: SAKATA LA KUTUPA WATOTO BADO LINAITAFUNA MBEYA. HILI NALO NI LINGINE...

7:06:00 AM Add Comment
(C) Mbeya Yetu

MBEYA, Tanzania
WIMBI la wanawake mkoani Mbeya kujifungua watoto na kisha kuwatupa na wengine kutoa mimba limezidi kushika kasi na kukithiri baada ya vitendo hivyo kuripotiwa na vichanga kuokotwa kwenye mashimo na mitoni.

Kukithiri kwa vitendo ni baada ya leo Wananchi wa Mtaa wa Mwambenja kata ya Iganzo jijini Mbeya kugundua kutupwa kwa mtoto anayesemekana kuwa na umri usiozidi siku moja jinsia ya kike katika shimo la choo kisichotumika.

Kwa mujibu wa mwenyekiti wa Mtaa huo, aliyefahamika kwa jina la Lukasi Mwakalonge, alisema alipewa taarifa na wananchi wake mchana na kuambiwa kuna katoto kametupwa shimoni na bado ni kazima hali iliyomlazimu kutoa taarifa katika Jeshi la Polisi.

Alisema baada ya kufika eneo la tukio na kugundua kuwa mtoto bado yuko hai wakaamua kumtoa ndani ya shimo huku wakisubiri jeshi la polisi kwa ajili ya hatua zaidi lakini akawa amepoteza maisha muda mfupi baada ya kutolewa ndani ya shimo.


Hata hivyo jeshi la Polisi lilifika eneo la tukio na kuuchukua mwili wa marehemu, vitendo hivyo vya wanawake kutupa watoto kabla na baada ya kujifungia bado vinazidi kutokea hapa nchini ingawa hakuna takwimu sahihi za wanawake waliopatikana na hatia kwa makosa kama hayo.

NA MBEYA YETU

UNAWEZA KUMSAHAU KIM KARDASHIAN KATIKA PICHA HIZI....

6:40:00 AM Add Comment

 KWA mara ya Kwanza kabisa, TTM tunapata nafasi ya kumuona Kim Kardashian akiwa amevalia gauni refu ambalo linafunika hadi miguu yake…

Tizama Picha Hizi





TANGAZO LA PERFUME YA RIHANA...STOOOOOOOOOOOOOOP !!!!!

2:49:00 AM Add Comment

Bibie Mwenye Sifa ya aina yake katika tasnia ya Muziki pamoja na Vituko Vyake kila kukicha, Rihanna, amjikuta katika wakati Mgumu baada ya Perfume yake kuingizwa katika matangazo tayari kwa Kuanza Kuuzwa.

Rihanna ambaye hivi sasa anaumri wa Miaka 26, ametengeneza tangazo la Perfume yake Mpya aina ya ROGUE (ROUGI), ambapo katika matangazo ya Kubandika anaonekana akiwa nusu Mtupu, Huku Miguu yake ikiwa imenyanyuliwa Juu, na kukanyaga Chupa hiyo.

Aidha jambo lililotokea Ni kwamba. Mamalaka inayoshughulikia Matangazo Nchini Marekani  (ASA), amepiga marufuku tangazo Hilo kubandikwa katika Eneo Lolote lile ambalo watoto Wadogo wanaweza Kufika kiurahisi.


ASA wameongeza kuwa, Wamefikia uamuzi huo kufuatia Tangazo hilo kuwa na Uchokozi wa mambo Fulani hivi hasa Kihisia, jambo ambalo si vema kuwekwa wazi kwa watoto wadogo. Naye Mzalishaji wa Perfume Hiyo PARLUX FRAGRANCES (PARUS FRAGRANSEZ), amesema kuwa hawajapokea Lalamiko lolote kuhusu Perfume hiyo zaidi ya Hilo la ASA

WATOTO ZAIDI YA MILLIONI 7.5 WANATUMIA FACEBOOK ULIMWENGUNI

2:44:00 AM Add Comment

Utafiti Unaonesha Dhahiri Kwamba kwamba, Watoto zaidi ya MILIONI 7.5, wenye  Umri wa Miaka 13, Hutumia Njia za Udanganyifu kufungua account zao katika Mtandao wa Facebook

Aidha taarifa zaidi zinafafanua kuwa, Awali mnamo mwaka 2012, FACEBOOK ilitakiwa kuwa na mchakato wa watoto walio na umri wa Miaka 13 kufungua account zao facebook, lakini Endapo wataruhusiwa na kusimamiwa na wazazi wao.

Naye Mkurugenzi wa Masuala ya Msaada wa watoto katika matumizi ya Mitandao, JAMES STEYER (STEYA), amesema kuwa ni kweli kuna Suala hilo, lakini hivi sasa hawana Utafiti madhubuti wa Kisayansi, kuweza kutathmin Faida hasi na Chanya ambazo Mitandao ya kijamii inaweza kuitoa kwa Vijana wenye umri mdogo.


Hata hivyo inasemekana kuwa, Hivi sasa Mtandao wa facebook bado inashughulikia Jukumu la Kuanzisha kanuni hasa katika Kujisajili, ambapo watoto walioko katika Umri wa Miaka 13, watahitaji kujaza majina ya wazazi wao, Mahusiano yao na wazazi wao, pamoja na Idhini ya wazazi wao, ili kutambua umri wa Mtoto huyo, ama mtumiaji wa Account hiyo ya facebook.

LINGINE KUHUSU DHAHABU YA LOLIONDO

2:40:00 AM Add Comment

Wataalamu wa Wizara ya Nishati na Madini, Kanda ya Kaskazini wamethibitisha uwepo wa hazina ya madini ya dhahabu katika Mlima RANKIROGA na Mto KARABALINE katika Kijiji cha Mgongo, Kata ya Samunge, Wilaya ya Ngorongoro Mkoa wa Arusha.

Kamishna wa Madini Kanda ya Kaskazini, Alex Magayane amesema kuwa Ofisi yake imefanya utafiti wa awali katika Kijiji cha MGONGO na kubaini uwepo wa dhahabu hiyo.


Habari kutoka Samunge zinasema wachimbaji wanazidi kumiminika kusaka madini hayo yaliyogundulika kuwapo kwenye mashamba ya watu na maeneo ya kingo za mto huko Mgongo, kijiji kilichopo jirani na kwa Mchungaji Mwasapile, maarufu kama Babu wa Loliondo.

JUMATANO MSETO: TAKUKURU NA WAFANYAKAZI WA TANESCO WALIORUKA UKUTA

2:36:00 AM Add Comment


Tasisi kuzuia na kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Kilimanjaro, imewatia mbaroni wafakazi  watatu na kuwachunguza wawili wa Shirika la Umeme nchini (Tanesco),  kwa kosa kuomba na kupokea rushwa ya Sh. 400,000.

Wafanyakazi hao wanadaiwa kwenda nyumbani kwa Baltaza Zafa Ally, mkazi wa Shant Town Manispaa ya Moshi, kwa malengo la kukata umeme wa nyumba hiyo kwa madai kuwa alikuwa akidaiwa na shirika hilo.

Baada ya akufika nyumbani kwa mteja huyo, Wafanyakazi hao  walikuta geti limefungwa ndipo walipoingia kwa kuruka ukuta wa geti na kuanza kukagua mita ya umeme na kudai kuwa mita hiyo imechezewa na kumtaka mteja huyo awalipwe Sh. million moja ili wasikate umeme.


Kwa Upande wake Baltaza amefafanua kuwa, watuhumiwa hao walifika nyumbani kwake kwa kuruka ukuta na kuingia ndani na kuanza kusoma mita, baada ya kumaliza kusoma miti hiyo ndipo walipomwambia kuwa mita hiyo imeonekana kuchezewa na kisha kumwambia awape fedha ili wasikate umeme.

MNADA BANNER