REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

INSTA COP: HATA BABA YAKO ANANIJUA...AU NIKUPE NAMBA YANGU? : CHIDDI BENZ

2:32:00 AM Add Comment

Na Baba Juti
#WatuWaMungu kuna Jamaa mmoja alijitia kumkandia Chiddi Benz "Chuma kwa Madai kuwa ameisha na hana lolote kwa sababu ya Kubwia Miunga (Dawa za Kulevya)

Sasa, Jibu alilolitoa Chiddi kupitia Instagram, Insta Cop tuliliona tukasema sio mbaya kama na wewe Tukikuhusisha Kabisaaaaa



MONEY ! MONEY ! MONEY ! : ETI KEYSHIA COLE AMEKUWA "CHIZI" NA MAYWEATHER TENA?

2:27:00 AM Add Comment

Na Samuel Richard "Sam Rich"
#WatuWaMungu Hivi kweli kuna kitu ambacho huwa kinaweza kufunika Pesa linapokuja suala zima la Furaha ya Moyo au Roho?

WAUNGWANA wanadai kuwa, Baada ya Floyd Mayweather Jr kumtandika McGregor na kuchukua Mkwanja ule Wote, basi yule Ex wake wa Mwaka Jana, Keyshia Cole, ameanza kujisogeza Taratiiiibu

Kwa Mujibu wa Waungwana Pia ambao huwa hawapendi U-Makuzi, walidai kuwa, Siku ya Mtanange, Keyshia Cole ambaye pia ni Ex-wa Rapper Birdman, alikuwepo uwanjani. Na Baada ya Floyd kumchapa McGregor, alifanya kila awezalo, kujipenyeza huku na kule, mpaka akafanikiwa kumfikia Floyd Mayweather Jr na hata kutandika naye Picha

Kinachokuja kuduwaza Zaidi ni kwamba, tangu waachane, Keyshia hakuwa ni mtu wa kumsifia ama kujiweka Karibu sana na Floyd, lakini baada ya Kushinda kibunda kile cha Fwedha, ikawa ndo Njia.

BAADA YA KUDAI KUWA KAFANYA TRACK NA TUPAC !!!! : MSIAMINI KILE MDOMO UNACHOONGEA-CHIDI BEENZ

2:03:00 AM Add Comment

Na Baba Juti & Instacop        
#WatuWaMungu kama mtakuwa ni wafuatiliaji wazuri sana katika Muziki hapa Nchini Tanzania, kuanzia Jana nadhani, Chiddi Benzi alinukuliwa akisema kuwa "Tupac Yuko Hai, na amefanya naye Track kwa Mensen Selkekta, and Very Soon ataiachia"

Katika Kauli Nyingine, Chiddi Benzi aliopngeza kuwa Tupac (Ambaye Ni Marehemu ) yuko Hai na Yuko Cuba, hivyo alienda kule, wakakutana na kutengeneza Track Hiyo, lakini Mzigo bado anao Tupac, so soon atamuachia.

Lakini katika Hali isiyotarajiwa, Dakika chache zilizokata (Wakati Tunapata Update Hii) kupitia Instagram account yake, Chiddi Benz ametoa Tamko Rasmi kuwa, kuna wakati huwa anazungumza  "Masihala" ili kupima akili za watu ziko Vipi

Katika Kukazia Zaidi, Chiddi a.k.a KING KONG "Chuma" alisema kuwa, usisikilize kile unachoambiwa kwa Mdomo

Tunamnukuu

UBAGUZI UTAKWISHA KWELI? : CHANCE THE RAPPER ASHAMBULIWA KWA KUWA NA MAHUSIANO NA MWANAMKE MWENYE ASILI YA KIZUNGU

1:32:00 AM Add Comment

Na Baba Juti   
#WatuWaMungu tunafahamu Vizuri kabisa Rapper Kutoka Nchini Marekani, CHANCE THE RAPPER, ni moja kati ya Rappers ambao wamefanikiwa katika masuala kadha wa kadha kiburudani, na kijamii Zaidi

Kama mtakuwa Mnafahamu Vizuri, Chance The Rapper aliweza kujiachia na kufanya Kweli katika Track aliyoshirikishwa na Dj Khaled "IM THE ONE"

Lakini katika hali ambayo sio ya Kawaida, Chance The Rapper amejikuta katika "Kichambo" kizito baada ya kubainika kuwa ana mahusiano ya kimapenzi na mwanmke mwenye asili ya Kizungu, yaani Mwanamke Mweupe kama ambavyo wanasemaga wenyewe

Hii imekuja siku chache baada ya Rapper huyu ambaye ana Ngozi ya Kiafrika, kuonekana akifurahia kuwa Out na Mpenzi wake huyu, kitu ambacho kilishambuliwa sana na wengi

Aidha, Chance The Rapper amekuwa ni miongoni mwa wasanii ambao wanapinga sana Ubaguzi wa Rangi, na mara Zote amekuwa katika Kutetea Wamarekani Weusi, hivyo wanashangaa kwa nini anajihusisha na watu ambao wamarekani weusi wanawachukia kwa sababu huwabagua sana na huwatenga sana, ikiwemo kuwadhalilisha


NEW SONG !! : NAY WA MITEGO- MAKUzi

1:06:00 AM Add Comment

Na Baba Juti  
#WatuWaMungu Nimeisikiliza hii Track ambayo Rapper NAY TRUE BOY kaiachia Ghafla Bin Vuu !!, nimecheka Sana aisee

Track Inaitwa MAKUzi, na Producer ni AWESOME kutoka Free Nation. Unaweza kuiskiliza na wewe

MNADA BANNER