REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

MUNGU TUOKOE: Muimbaji Huyu wa Gospel Ameimba Wimbo Unaoitwa "NIPE NYONYO"

1:08:00 AM Add Comment

Na Baba Juti
SASA, Sijui ndio muelekeo wa Gospel, sijui Yuko Sawa..au Lah
Msanii Chipukizi wa Muziki wa Injili Kutoka Nchini Kenya, anayefahamika kwa Jina la SBJ, ameachia Track ya Gospel inayoitwa Nyonyo.

Kama hujakutana na audio au Video hiyo, Msanii huyo ambaye ameonekana kukosolewa Vikali kwa Wimbo huo ambao unaonekana ni kama kuanza kuudhalilisha na kuunyima Muziki wa Injili Heshima, anamuomba Mungu ampe Nyonyo, huku akisisitiza pia kuwa anamuomba Yesu ampatie Nyonyo nay eye ashibe

Pia katika Track Hiyo Msanii huyo analalamika kuwa, kuna wengine wamepewa Nyoyonyo wakanyonya kasha Wakavimbewa. Na Kuna wengine walipewa Nyonyo, kasha wakalala
Mstari mmoja wapo ni kama ifuatavyo:

“Eeh Baba nipe nyonyo oh Yesu niko tayari eeh..nijue jinsi ya kamua, nielewe mi kunyonya.


Comments zinasema hivi
  • Bienaime Alusa Baraza: Pewa nyonyo mbili hapo kwa bill yangu
  • Sheelah Kenis : what the fuck is this????
  • Njeri PaulineThe lyrics oh my word, is he for real..this is sooo wrong in every way
  • james kiarie : This video should be removed from You Tube. What the hell !!
  • peter nganga "Holy crap" this guy shld come read the comments and try another field
  • sherry kamondo : i cant believe my ears, gooosh. inauthi
  • Joshua Kembero: I wasted two precious minutes of my life
  • Douglas Kigotho : the name first of all is a disgrace ati s......BJ.what tha hell is wrong with this guys
  • njoroge gatitu: I blame the producer for producing this kind of a song, try something else other than singing
  • Mary njengahThis is crazy....Jeez what kind of a gospel is this....Lord have mercy on us
  • Shizney winko I know we're not supposed to judge but this is madness, is it a must for everyone to sing gospel in Kenya? shame shame. Mungu atusaidie

WATANZANI: KWAKWELI MUNGU ANAWAONA. SIO KWA MATUSI NA KUPUYANGA HUKU KATIKA AKAUNTI YA KUMPIGIA KURA MISS WORLD 2016

12:59:00 AM Add Comment


 Na Baba Juti
KWAKWELI , kama ikija Tuzo ya Matusi , Madongo, Kutokuelewa, na kukurupuka katika Mitandao ya kijamii, hasa Instagram, Bongo Tunaweza kuchukua nafasi ya Kwanza

Kama ulikuwa hujui, tofauti na kufanyiana Mafyongo katika account zetu sisi Wenyewe, na hata kutukana wasanii wetu ama watu Maarufu, safari hii Bongo tumeamua kuwavamia Washiriki wa Miss World kunako Account zao za Instagram, sambamba na account ya MISS WORLD ambayo huwa tunaitumia kupiga Kura kumpata Mshiriki.

Sasa Ili kudhihirisha kuwa sie ni Vichwa Ngumu, Takwimu za Madudu yetu katika Instagram account ya Miss World, inayotumika kupiga Kura
MISS NORTHEN IRELAND
  • MATUSI-29
  • MABIFU YA UTIMU-14
  • KUPUYANGA- 67
MISS RUSIA
  • MATUSI-18
  • MABIFU YA UTIMU-45
  • KUPUYANGA- 78
MISS SINGAPORE
  • MATUSI-2
  • MABIFU YA UTIMU-0
  • KUPUYANGA – 45


MISS US VIRGIN ISLAND
  • MATUSI-01
  • MABIFU YA UTIMU- 0
  • KUPUYANGA- 24
MISS UKRAINE-
  • KUPUYANGA 17
MISS GUINEA BISSAU
  • MATUSI-07
  • MABIFU 02
  • KUPUYANGA- 45

AT: NILIMTAFUTIA RIHANNA BAIBUI, LAKINI MEDIA HAIJALITAMBUA HILO

12:47:00 AM Add Comment
Na Baba Juti
AT Jana alitia timu katika Ofisi za 93.7 Jembe Fm-Mwanza, na kupiga Story Nyingi sana, lakini kuna hili moja ambalo sijui tuliamini ama tulipe Uzito Gani.

Mkali huyu wa “Vifuu Tundu” ambaye huwa hapendi kuitwa Mzanzibar, amedai kuwa, Media Nyingi Nchini Tanzania zimekuwa zikijikita zaidi kuzungumzia na Kupost Kuhusu masuala ya Skendo Skendo tu, lakini wanasahau kuwa kuna mambo Mengine ya Msingi kuzungumzia.

Katika Kuliweka Hilo Jambo sawa, AT amedai kuwa, amewahi kufanya Mambo makubwa Matatu lakini Mpaka hii Leo, Media haijawahi kuzungumzia Masuala hayo

Katika  Kufafanua zaidi, AT anadai kuwa, Wimbo wake mmoja uliwahi kuchukuliwa na kutumika Kimataifa katika Ngazi za Juu. Lakini Pia, kushauri katika Vazi la Baibui ambalo alivaa Rihanna

Msikilize

VICTORIA KIMANI: SINTOFANYA TENA KOLABO NA MSANII WA KENYA

12:20:00 AM Add Comment

Na Baba Juti
MSIMTAFSIRI kama amevimba kichwa, no, ni Msimamo wake jamani, na mwingine anaweza kuamua hivyo hivyo.

Victoria Kimani kutoka Nchini Kenya, amedai kuwa hana mpango wa kufanya “Kolabo” na msanii mwingine yeyote Kutoka Nchini Kenya Bali ana matarajio makubwa zaidi

Akifafanua Vizuri kuhusu Hilo, Kimani ambaye hivi sasa yuko Chini ya Chocolate City ya Nchini Nigeria, amedai kuwa, awali alitamani kufanya kazi na baadhi ya Wasanii Nchini Kenya na Tayari, hivi sasa hana plan Hiyo

Nukuu:
“Nilitaka kufanya Kazi na Wyre, nilifanikiwa, nikatamani kufanya kazi na King Kaka, nikafanikiwa. Muda huu, siwezi kumfikiria mtu yeyote tena, ambaye natamani kufanya naye kazi. Kwa upande wa Wasanii wa Kenya, nadhani nimeshamaliza, na hao ambao nimefanya nao Kazi.”

Pia Katika hali Nyingine, Victoria Kimani amedai kuwa anahitaji kufanya Kazi na Kanye West kutoka Nchini Marekani.
Pia amefichua kuwa, yuko tayari kuolewa sasa hivi, na anatamani kuwa Rafiki wa Beyonce.

SHOGA NCHINI KENYA: NINAMTAKA NAHREEL WA NAVY KENZO

12:12:00 AM Add Comment
Na Baba Juti
KAMA Mtakuwa mnakumbuka Vizuri kuna kipindi Nahreel na Mpenzi wake Aika ambao wanaunda Kundi la Navy Kenzo, walitia Maguu Nchini Kenya kwa Ajili ya Shughuli moja Tu, Kazi Kunako tuzo za Video za Pulse- PULSE MUSIC VIDEO AWARDS 2016

Lakini kwa Mujibu wa Info ambazo mpka hivi sasa Team Hit Zone tunazo, ni Kwamba kna jamaa mmoja ambaye anasifika Nchini Kenya kwa Kushiriki Mapenzi ya Jinsia Moja, yaani "Shoga" alilazimisha kuingia kunako upande wa VIP kwa nia Moja tu, anamtaka Navy Kenzo

Pia Taarifa zinazidi kueleza kuwa, Jamaa huyo, alilazimisha kupiga Picha na Nahreel Peke yake, lakini hali haikuwa hivyo, badala yake Nahreel alimkamatilia Vizuri Aika na wakapiga Picha na Shoga Hilo.

Lakini Kama Haitoshi, Jamaa huyo alisisitiza zaidi kuwa anataka kumpatia Kitu Spesho Nahreel, akiwa Peke yake Bila Aika, kitu ambacho kiliwalazimu mabaunsa wamtoe upande wa VIP kwa Nguvu kubwa, lakini bado jamaa aliwajibu Baunsaz kuwa, bado tu atampata Nahreel hata wambanie vipi

SOULJA BOY: MIKONONI MWA POLISI

11:49:00 PM Add Comment


 Na Baba Juti
SASA, Mbwembwe zooooote za kututishia Bunduki, mara kutukana wasanii wenzake, mara kutulingishia kuwaa yeye anapendwa na Mtoto wa Rais Barack Obama, mara yeye ndiye ameanzisha Internet, hatimaye kimya !!!!

Rapper Mwenye Jeuri, Dharau na Kiburi kutoka Nchini Marekani, SOULJA BOY, hatimaye amerushwa Nyuma ya Nondo kwa kosa la kukiuka masharti ya Chini ya Uangalizi

Kwa Mujibu wa Mahaklama Nchini Marekani, Soulja Boy alikiuka Masharti hayo baada ya Kutishia Wasanii Wenzake kwa Kutumia Silaha aina ya Bunduki,.

Na  Baada ya Jeshi la Polisi kuingia Nyumbani kwake kwa Kushtukiza na kufanya Upekuzi, walifanikiwa kukamata Silaha hiyo, na kumfikisha Mahakamani.

HATIMAYE: KERI HILSON AMEZUNGUMZA SABABU YA KUACHIKA.

1:09:00 AM Add Comment

BLACK TOUCHEZ
MDUDU wa Usaliti katika Mahusiano ya Watu Maarufu hasa wasanii wa Muziki wa Kizazi Kipya, ambapo safari hii, Keri Hilson naye ameamua kuvunja Kimya.

Hit Maker huyo wa Loose Control aliomshirikisha Rapper Nelly, amesema kuwa, sababu kubwa ya yeye kupigana Chini na Mchumba wake SERGE IBAKA ambaye ni Mtupia Kikapu wa NBA, ni baada ya kubaini kuwa amempata mtu tofauti na alivyotarajia.

Akifyatuka kwa Hisia kuhusu hilo, Kerry Hilson anadai kuwa akiwa kama mtu mwenye msimamo kama ambavyo anafahamika katika Muziki wa RnB, basi alidhani pia amepata Mtu mwenye msimamo dhahir, lakini ikawa topfauti, kitu ambacho kilimuangusha

Pia Keri Hilson aliongeza Hivi :
"Katika maisha yangu ya Mahusiano, sheria yangu ilikuwa ni kutokuwa na mwanaume ambaye ni mwanamichezo, Rapper, au Muigizaji, lakini ghafla nikavunja sheria yangu baada ya kukutana na Huyu mtu. Ila ameniangusha kabisa kwa kuwa tofauti na Matarajio yangu. "

Pia Katika kauli Nyingine, Keri Hilson amesema hivi
"Sina Tofauti na Wanawake wengine linapokuja suala zima la Mvuto na Ubora kwa Mwanaume. Level yangu iko mbele sana. Ninamtaka Mwanaume ambaye anampenda Mungu vizuri sana, na kumuheshimu mwanamke, na Mstaarabu. Yale yale ambayo kila mwanamke bora anayapenda"

KEISHA: AHSANTE MUME WANGU !!!!

12:22:00 AM Add Comment

NA BABA JUTI
HATIMAYE Msanii ambaye amekuwa Kimya kwa Muda Mrefu sana katika Muziki Industry, ameweza kuibua jambo lingine ambalo ni la kufurahia na hata kujivunia, huku shukrani kubwa zikienda kwa Mwenyezi Mungu na Watu wawili ambao ni Muhimu kwake.

KEISHA, ambaye hivi karibuni amehitimu elimu ya Chuo Kikuu, sanjari na kupata mtoto mwingine wa Tatu, amemshukuru sana Mume wake JAM JAYS kwa kuwa naye kwa Takriban muda wote na hata kuvumilia mengi ambayo wameyapitia na hata kufanikiwa watoto watatu...

Nukuu !!
"Nimebarikiwa, ninafuraha na niajivunia. Shukrani sana Mume wangu Mpendwa kwa kuwa Sehemu ya Maisha Yangu siku zote. Ni bahati kubwa sana kuwa na wewe Maishani Mwangu. Shukrani tena kwa kuwa Baba Bora wa Watoto wangu watatu kwa mapenzi yako yote, na kuendelea kusupport na kutimiza ndoto zangu. Ni 100% kweli kabis, katika Mafanikio ya Mwanamke, basi kuna mwanamume nyuima ya mafanikio hayo. Nakupenda sana Mume wangu JAMYJYS"


Tofauti na hilo, Kesha pia amemshukuru Mama yake, na kusema kabisa kuwa yeye ni Mungu wa Pili kwake

Pia Keisha amedai kuwa, mama yake alikomaa na kila kitu ili ampatie maisha ikiwemo kuuza biashara ndogo ndogo

Nukuu
"Ana nafasi ya kipekee sana mama yangu kama nilivyonayo mimi kwake nakiri kusema bila yeye mimi si kitu huyu ni mungu wangu wa pili hakuna anebisha furaha yangu ni yake maumivu yangu ni yake shida zangu ni zake mimi ni wapekee kwake hana mwingine kwenye maisha yake mapenzi yake kwangu siwezi yaelezea hakuna ambacho hajafanya kwaajili yangu anauza kila aina ya biashara ndogondogo zote mimi nifurahie maisha hata ingetokea nizaliwe upya ningeomba nizaliwe na huyu mwajuma binti salum mama khadija mwenyewe. Nakupenda sana mama yangu mungu pekee ndo anajua nani kama mama jamani???"

Neno Moja kwa Keisha Tafadhari !!

LIL WAYNE: AMESAINI NA JAY Z?

11:52:00 PM Add Comment


BLACK TOUCHEZ
BANANGE, Matumaini ya Birdman kumrudiusha Lil Wayne katika Record Label yake ya Cash Money, huenda ikawa ndo imepotea, baada ya Weezy kufanya jambo ambalo kila mtu hakulitarajia.
Akiwa kwa Stage, Weezy alifanya Vitu  viwili ambavyo kila mtu ilikuwa ni lazima akubaliane na kutafakari kwa namna yake na namna ambavyo anaweza.


Jambo la Kwaza, Lil Wayne akiwa kwa Stage, alitamka yeye kama yeye kwa Kinywa chake kuwa, amesaini Deal na Rapper Mkongwe mwenzake , JAY Z katika kufanya shughuli zake mbali mbali kimuziki, hali ambayo iliashiria kabisa kuwa huenda jamaa uyu sasa akawa chini ya ROCA FELA RECORD LABEL ambayo iko chini ya Jay Z

Lakini katika Hali Nyingine, Weezy alifanya Editingi katika moja ya Wimbo wake ambao awali Rapper huyo alisikika akisema kuwa "I am a Cash Money Bilionaire", lakini akiwa stage, alisema hivi, "I am a Roca Fella Bilionaire" kitu ambacho kinaashiria kuwa, hivi sasa amesaini mkataba na Rapper Jayz

JIBU LA KAKA MENEJA:
Kwa Mujibu wa Taarifa kutoka kwa Meneja wa Lil wayne - CORTEZ BRYANT, amekanusha taarifa hizo na kudai kuwa Mitandao ya kijamii na Blogs imetafsiri suala hilo tofauti, maana halina ukweli wowote. Aliochokimaanisha Weezy ni kwamba ameungana na Jay Z kwa ajili ya kusambaza mikwaju yake kupitia Mtandao wa TIDAL, na sio kusaini mkataba.
hata hivyo jibu hilo halijawapa chochote mashabiki.

STOPA RHYMES : STYLE TATU ILIWAFANYA WASANII WABADILIKE NA KUANZA KUIFUATA TONGUE TWISTA NA KUPATA UJASIRI WA KUTUMIA LUGHA ZA KIGENI KATIKA NYIMBO ZAO

6:44:00 AM Add Comment

Na Baba Juti
RAPPER kutoka Arusha na Hitmaker wa STYLE TATU, Stopa Rhymes Okoyi, kupitia Hit Zone, ameweka wazi kabisa kuwa katika Game kwa asilimia kubwa, kuna baadhi ya Wasanii ambao huangalia kuna kitu kimefanyika halafu na wao wafuate

Akiweka Wazi kuhusu Hilo, Mkali huyo ambaye aliua pia na Zigo la Boom Bye Bye, amesema kuwa, Kipindi ambacho yeye anaachia Style 3, Wasanii Wengi walianza kupata Ujasiri wa kufuata Mfumo na kutumia Tongue Twista na hata kutumia Lugha za kigeni kama Vile Kiingereza
Tofauti na Hilo, Stoppa anaamini kuwa, Support ya Mashabiki katika Kipindi hiki Imekuwa Ngumu, maana wanasupport kwa kucomment tu, kulike, na mengineyo, lakini katika kununua bidhaa zao, imekuwa Ngumu

MAADHIMISHO YA SIKU YA MABOGA: IZZO BUSINES ANADAI KUWA UBACHELOR ANAOISHI DAR, UMEMFANYA ASHINDWE KULA MABOGA MPAKA ATAKAPORUDI KWA MAMA YAKE (AUDIO)

6:39:00 AM Add Comment

Na Baba Juti & Cathberth Mazigo
KAMA wewe unapenda kula kula kama wengine ambao tulishajaliwa kula vyakula vya aina tofauti tofauti sana, basi utakubaliana na mie kabisa kuwa, Kuna Chakula ambacho ni Jamii ya Tunda kinachoitwa BOGA

Boga haizalishi Tunda tu, bali hata majani yake huwa ni Mboga Nzuri, na unaweza kuiita Msusa, au kuyapika Kama Mrenda kwa jamii mbali mbali kama vile wasukuma, Wanyamwezi na wengineo
Lakini Kama Haitoshi , unaweza kufurahia Juice ya Maboga, na Hata Ile Mbegu yake, hutumika kama kitoweo pia, na hunoga sana ikiwa na Viazi Vitamu

LEO, OCTOBER 26, Ni Siku Maalum ya Maboga, na huazimishwa Sehemu Mbali mbali Hapa Duniani, lakini Pia Huazimishwa kwa Njia Tofauti.

Baadhi ya Mataifa Husherekea na kutumia Maboga kama kihisishi cha Siku ya HALLOWEEN, Lakini kuna Badhi ya Mataifa hupinga Vikali matumizi hayo ya Maboga katika Siku Hiyo

Mataifa hayo huamini kabisa kuwa, Heshima ya Boga Ni Chakula Maalum na siku ya Maboga ni Siku ya kufaidi kitu Kizuri na Rahisi zaidi kupika ama kuandaa.

Tofauti na hayo, Boga kwa Kiingereza huitwa PUMPKIN , jina liliotokana na Lugha ya Kigiriki ambao huliita PEPON wakimaanisha TIKITI MAJI KUBWA

Ukiachana na Hilo, Ufaransa huliita Boga kama POMPON, Kisha Uingereza wakaliita PUMPION, lakini Wamarekani Wakaliita PUMPKIN na ndivyo linafahamika hivyo Tayari.

Izzo Business , Msanii wa Kizazi Kipya Hapa Nchini Tanzania, anasema kabisa kuwa Ni Kitu ambacho Huwa anakipenda, ila kutokana na Maisha ya Kibachelor ambayo anaishi Dar, hajala Boga Muda Mrefu wala Mboga ya Msusa, lakini akienda Mbeya kwa Mama yake, lazima alikule
Lakini Pia, anakiri kuwa anapenda sana hicho kitu na anajivunia kulipenda


NISHER: ANAAMINI KUWASIKILIZA WATU, NI NJIA YA KUPIGA HATUA

6:31:00 AM Add Comment

Na Baba Juti
DIRECTOR Nisher Kutoka Hapa Hapa Nchini Tanzania, amepotea kidogo katika Industry ya Production, but Guys, mujamaa yuko na mashine Very Classic na Expensive Bya Hatari !!!

Kitu ambacho Director huyu aliyewahi kusumbua kabla hata ya akina Hascana kutake Over, ni kwamba kuwaheshim na kuwasikiliza Watu sometimes, inakusaidia kuzingatia na kufanya kazi yako kwa Ufanisi...


Akizungumza hayo kupitia Channel yake ya Youtube, Nisher ambaye hivi sasa ameachia Series yake ya ALEX, amesema kuwa, kwa asilimia kubwa huwa anapitia Comments za Wadau wake na kuchambua vizuri, ili kuweza kupata japo kitu cha msingi katika Kazi yake
Tofauti na Hayo, Nisher amesema hajaacha kufanya Video za Muziki kama ilivyokuwa awali, bali hivi sasa anafanya kwa Malengo, tofauti na zamani alvyokuwa akifanya kwa sababu ya kutafta jina, na alikuwa akifanya hata kama ni Kulipua
Kwa Upande Mwingine, Nisher amesema kuwa, anapenda kuwasuprise zaidi, hivyo hatoshea vitu vingine, ila ni bora mkamfuatilia katika mitandao yake ya kijamii ili kujua what is Next.

KEKO: HATIMAYE AMERUDI KATIKA FLOW..KUPIGA SHOW NCHINI KENYA

6:26:00 AM Add Comment

Na Baba Juti
ANGALAU sasa wale ambao tulikuwa tuna hamu na Flows na Matamshi Matamu kutoka kwa Ugandan Female Rapper - KEKO, tunaweza anaza kupata matumaini ya Ujio Wake

Baada ya Kuhusishwa na matumizi ya dawa Za Kulevya, ikiwemo pia kufulia kimuziki, na hata kuminywa sana na management yake na hata kutamka kuwa sasa anabwaga manyanga katika Music Industry, hatimaye Keko hivi sasa ana matumaini ya kurudisha heshima yake katika Stage.

Hit Maker huyo wa  HOW WE DO IT, anatarajia kupiga Show  katika Jukwaa litakalofungwa katika Makao Makuu ya KENYA, Nairobi, katika Show ya QUEENS OF THE MIC itakayokunjwa  November Mwaka huu

Keko ambaye kwa asilimia kubwa ana hamu ya kurejesha heshima yake katika Muziki wa Africa Mashariki , aliwahi kupitia majanga kadha wa kadha ya kukatishwa tamaa, baada ya kufutwa katika Mfululizo wa COKE STUDIO kwa Mwaka Jana, na hata kutimuliwa katika Moja ya Hotel Kubwa Nchini Kenya, kwa madai kuwa alilewa sana na kusababisha fujo.

ALL THE BEST KEKO.

ANGELINA JOLIE: AMESITISHA MASUALA YA MOVIE KULE HOLLYWOOD ILI KUWA KARIBU NA WATOTO WAKE,

6:23:00 AM Add Comment

Na Baba Juti
MUIGIZAJI Angelina Jolie ameamua kuweka Kando suala zima la Kuporoduce Filamu aliyokuwa na hamu nayo sana, ili kuwa Karibu na Watoto wake

Uamuzi huo unatokana na Vuguvugu la Talaka na Mumewe wa Muda Mrefu, BRAD PITT, ikiwa ni baada ya kuwepo kwa Madai kuwa, Mumewe huyo amekuwa akiwanyanyasa watoto wao kutokana na matumizi ya Pombe pamoja na Madawa ya Kulevya.

Kwa Mujibu wa Taarifa kutoka Hollywood ni kwamba Bibie huyo hivi sasa hajihusishi tena katika Kumalizia Filamu yake ya FIRST THEY KILLED MY FATHER ili kuhakikisha kuwa suala la malezi linaenda sawa kwa watoto wake


Tofauti na hilo, inasemekana kuwa, Watayarishaji wa Filamu hiyo wamekuwa wakijitahidi kumuhusisha Angelina Jolie kwa Njia ya SKYPE, lakini amekuwa hajibu Chochote.
Pia inawezekana kabisa Angelina Jolie akahamia LONDON.

Lakini Kwa Upande Mwingine, Mume Wake Brad Pitt anatarajia kutokea katika RED CARPERT ya Uzindz wa Filamu ya ALLIED itakayoachiwa Rasmi na kuingizwa Sokoni NOVEMBER hii.


TONI BRAXTON: NI MBISHI BALAA, AMEAMUA KUPIGA SHOW AKIWA NA KIFAA CHA HEART CONTROL

6:20:00 AM Add Comment

Na Baba Juti
SIKU Kadhaa zilizokata, kama utakuwa unakumbuka Vizuri, tulikupa Info Kuwa, Mwanamama Toni Braxton, alikumba na tatizo baya la Kiafya hali ambayo ilimlazimu apelekwe Hospital Mara mbili kabla ya Show yake na hata kuahirishwa Mara Kadhaa.

Lakini Ili Kuonesha kuwa ni Mbishi Kupita Maelezo, Hit maker huyo wa Breath, aliamua kupanda jukwaani na kifaa maalum cha Kupima muelekeo wa Moyo Wake yaani HEART CONTROL.


Tatizo kubwa la LUPUS ambalo madhara yake huvamia kila sehemu ya mwili hasa Ngozi na sehemu ya Moyo, ndilo lilikuwa likimsumbua sana Bibie Huyu, lakini Hiyo bado haikumzuia yeye kufumua Show yake huko maeneo ya Savanna, lakini alionekana akiwa na kifaa hicho.

Kwa Mujibu wa Maagizo ya Madaktari wa Toni Braxton, bibie huyo anatakiwa  kuvaa kifaa hicho masaa 24 kwa Wiki, ili kubaini Maumivu ya Kifua, pamoja na Shambulio la Moyo au Stroke kama ikibidi.

JUSTIN TIMBERLAKE HUENDA AKAINGIA MATATANI BAADA YA KUPOST PICHA AKIPIGA KURA.

6:16:00 AM Add Comment
Na Baba Juti
SIJAFAHAMU kwa Nchi ya Tanzania kama ni Kinyume cha Sheria kupost Picha ukiwa unapiga Kura hasa ya kumchagua kiongozi wa Nchi au lah, lakini asilimia kubwa huonekana wakiwa Tayari wana wino katika Vidole vyao.

JUSTIN TIMBERLAKE huenda akautana na kifungo cha Siku 30 Jela pamoja na Fain ya Mkwanja, baada ya kupost Picha akiwa anapiga Kura, katika Maeneo ya TENNESSEE huko Nchini Marekani


Kwa Mujibu Mawanasheria wa Jimbo la SHEBY huko huko Tenessee, inasemekana kuwa Hitmaker huyo wa Cant Stop The Feeling hivi sasa yupo katika mahojiano na ukaguzi mkubwa hasa kubaini kwanini alikiuka Sheria za Nchi Hiyo, kupiga Picha ukiwa unapiga Kura, na kupost katika Mitandao ya Kijamii

katika Sheria ambayo iliboreshwa na kuhimizwa kufutawa zaidi kuanzia mwaka Jana, Ni Marufuku kwa Mtu yeyote kupiga picha au kurekodi mazungumzo ya aina yoyote yanayotokea katika Eneo la Kupiga Kura. na Endapo itabainika kuwa, umevunja Sheria hiyo, basi unakula Nyundo ya Siku 30 Jela, pamoja na Faini ya USD 50


ANNE KANSIIME : KUWANIA TUZO ZA UK AWARDS - BAWR

5:31:00 AM Add Comment


Na Baba Juti
HAKIKA kila mtu hivi sasa anamfahamu vizuri Binti mchekeshaji kutoka Nchini Uganda, ANNE KANSIIME !!!

YEs, The Good News ni kwamba Bibie huyu ambaye amejichukulia umaarufu mkubwa Afrika Mashariki, amechaguliwa kuwania Tuzo za Kimataifa za UK BLACK AFRICAN WOMAN ROCK (BAWR) ambazo zinatarajia kufanyika Uingereza , DECEMBER 03 2016

Tuzo hizo ambazo zilianzishwa na LINDANI MOYO mwaka 2013, ziko maalum kwa ajili ya kuwapa Moyo wanawake wa Kiafrica, kuelimisha, na hata kuhamasisha wanawake ambao wana mizizi ya Kiafrika katika harakati zao

Kansime amekuwa ni Msanii wa Vituko wa Kike Pekee kutoka Afrika mashariki, asiyeogopa kuthubutu na hata kupambana mpaka kupata Deals Nyingi sana

TUMEMMIS KANYE WEST WA ZAMANI?

5:25:00 AM Add Comment
Na Baba Juti

WANGAPI wanakubali kuwa Rapper Kanye West Wa Zamani alikuwa ni Bora kuliko Kanye West Wa Hivi Sasa?... Lakini Pia, ni wangapi wanakubali kuwa Kanye West wa sasa ni Bora kuliko yule wa Zamani?

Swali hilo pia imebidi team tujiulize kama yanayosemwa na Business patner wa Jay Z yana ukweli wowote, ikiwa ni baada ya kuwepo na Mgogoro wa majibizano baina ya Jay Z na Kanye West


KAREEM BIGG BURKE ambaye ni Patner wa Jay Z katika Studio ya ROCA FELLA RECORDS amedai kuwa, mara ya kwanza wakati anamsikia Kanye West akimzungumza vibaya Jay Z na kudai kuwa hata watoto wao hawajawahi kucheza pamoja, iliweza kumshtua kila Mtu.


BURKER ANASEMA...
"Nilishtuka sana kasikia kile ambacho Kanye aliksema kwenye Jukwaa. hakukuwahi kuwa na tatizo baina yao.. kwa hiyo ukisikia kitu kama hicho tena hadharani , lazima ushtuke kidogo. Mara ya Mwisho namuona Kanye , alizungumza vizuri na Jay Z. Sina uhakika sana kama mahusiano yao yamefikia hatua hii. Na nilipozungumza na Jay Z kuhusu Ishu aliyoisema Kanye West, kila mtu alibaki akisema TUMEMMISS KANYE WEST WA ZAMANI. Kwa kile ambacho ninafahamu kutoka kwa Kanye, ni kwamba huwa ni mkweli sana. hivyo inaonekana kabisa kuwa kuna kitu ambacho kinaendelea baina yao kwa hivi sasa. Anaweza kuzungumza kitu kama hicho, lakini baada ya Wiki kama tatu, utamsikia tena akisema "Jay Z ni Kaka Yangu kabisa. "

Tofauti na Hilo, Nicki Minaj pia aliwahi kutamka kauli ambayo kila mtu ilimshtua kuhusu Kanye West, ambapo alidai kuwa Kanye West wa Zamani sio wa hivi sasa, maana kupitia kwa mkwaju wa GOLD DIGGER, alikuwa akiwapondea wanawake tegemezi sana na wanaotafuta pesa kwa njia za kijanjanja kijanjanja, huku akihamasisha Wanaume Weusi, kutwaacha wanawake Weusi kisa wanawake weupe. Lakini hivi sasa, imekuwa tofauti, na Kanye West ana Mke Mweupe na Gold Digger ambaye ni Kim Kardashian.

MNADA BANNER