REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

KISA WAMEFUTA POSTER YAKE INSTAGRAM !!! : HIKI NDICHO ALICHOKISEMA KING KAKA KUHUSU SAUTI SOL...TUNAKOENDA AISEE !!!

3:19:00 AM Add Comment

Na Baba Juti   
#WatuWaMungu Instagram !! Instagra !! Instagram !! Instagram imekuwa Instagram safari hii, naomba tu tufahamishane Hili

King Kaka kutoka Nchini Kenya, ameonekana kuchukizwa na Kundi la Muziki Nchini Kenya SAUTI SOL kwa kitendo cha Kufuta Poster yake katika Instagram account yao

Chanzo cha hayo yote inaonekana kuwa ni namna ambavyo aliwadiss katika Interview yake na moja ya mtandao wa kidaku Nchini Kenya, huku akitoa kauli kuwa kila mtu anatakiwa ajisaidie ili baadaye pia aweze kusaidiwa.

Lakini kama haitoshi, akadai kuwa, SAUTI SOL hawasaidi Music Industry ya Kenya, ingawa wenzao wanawapigia kura, na yeye ni shabiki yao Mkubwa

Sasa inavyoonekana , baada ya Saut Sol kukutana na kauli hiyo ya Rabbit a.k.a KAKA SUNGURA ama King Kaka, waliamua kuifuta Poster yake kuhus Mkwaju wake Mpya, kitu ambacho kimemuuma Rapper huyo na kusema haya kupitia Instagram account yake

TIZAMA

JAMANI !! NA HUYU TENA? : DRAKE ANA MAHUSIANO YA KIMAPENZI NA EX WA TYGA?

2:26:00 AM Add Comment

Na Rich Sam   
#WAUNGWANA mnaanza kutushinda Tabia, maana sio kwa Uchionganishi huu ambao mnaanza kuuweka, ingawa ni kweli sawa lazima tufanye Uungwana

Taarifa ambazo tuko nazo mpaka Hivi sasa, Ni kwamba  Rapper Drake ambaye anapewa daraja la kwanza kwa Hivi sasa kwa kukunjuka na wasichana wengi bila kuangalia wametoka na nani ama wana sifa gani, hivi sasa yupo katika Mahusiano na Ex- wa Tyga

Kama utakuwa unamfahamu DEMI ROSE, Miezi kama Mitano iliyokata, alikuwa katika Mahusiano na Rapper Tyga, huku akipewa sifa pia ya kufanana na Kylie Jenners, lakini baadaye zikavuma kuwa Mrembo na mwanamitindo huyo hayuko naye Tena

Sasa, Waungwana walipata nafasi ya kuvizia katika Kiwanja ambacho kinapatikana katika Jiji la London, ambapo Drake na Ex Huyo wa Tyga walikuwa wakila Bata.

lakini ajabu na Kweli ni kwamba, Baada ya Muda kadhaa, Drake na Mrembo huyo walichomoka kunako Club Hiyo na kuelekea Hotel Moja ambako inasemekana kuwa ndiko walifikia na kufanya kile ambacho wanastahili kukifanya

   KAMA ULIKUWA HUMJUI     
DEMI ROSE ni Mwanamitindo ambaye ana Umri wa Miaka 22 kwa hivi sasa, na Ni Raia kutoka Jiji La London Uingereza.

Binti huyo ana Urefu wa 5'2, na alipata umaarufu mkubwa baada ya kuanza kupost Picha zake peke yake, na hii ilikuwa ni baada ya kujitoa katika Kundi la Wanamitindo "Tata" ambao walikuwa wakitumia instagram na walijiita TAZ'S MODELS


HALELLUYA :: HAKIMU ASITISHA ADHABU YA KIFUNGO CHA CHINI YA UANGALIZI KWA GUCCI MANE

1:42:00 AM Add Comment

Na Baba Juti   
#WatuWaMungu Sio kwamba ni kwa sababu ya Ndoa yake ambayo inatarajiwa kufungwa hivi karibuni, hapana, bali kuna jambo ambalo limeonwa.

Hatimaye Hakimu kutoka mahakama ya Georgia ameamua kusitisha Probation ama adhabu ya kuwa chini ya Uangalizi , aliyokuwa akiitumikia Rapper Gucci Mane.

Gucci Mane ambaye jina lake halisi ni RADRIC DAVIS, alikutana na Rungu hilo ikiwa ni baada ya kukutwa akiwa na Silaha kinyume cha Sheria za Nchi ya Marekani, lakini hivi sasa amtajwa kuwa ni moja kati ya Wafungwa waliotumikia adhabu yao Vizuri, ikiwemo kuhudhulia katika Sobber House , Kupunguza Uzito, kukaa eneo alilotakiwa kukaa, na hata kupoteza pesa Nyingi katika Matamasha aliyokuwa afanye, lakini ilikuwa ni kwa sababu ya kutii Sheria

Kutokana na hayo na mengi aliyofanya, Mahakama imeamua kusitisha Adhabu yake, na hivi sasa yuko Huru kufanya mambo mengine ya Msingi

    IKUMBUKWE   
Baada ya kutoka Jela, Gucci alionekana akiwa amepungua Uzito kwa kasi ya ajabu, na hata kuachia Wimbo ndani ya Saa 24, pamoja na kuachia Album Mwaka ulioppita, hali ambayo iliashiria kuwa Gucci alikuwa ni mtu wa Kujituma hasa katika kuandaa mikwaju yake

MNADA BANNER