REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

MNAZAA WA NINI?: MARIO WINAS ALIYESUMBUA NA "I DONT WANNA KNOW" ASWEKWA RUMANDE KWA KUSHINDWA KUMHUDUMIA MTOTO WAKE WA MIAKA 12

2:56:00 AM Add Comment

Na Baba Juti   
#WatuWaMungu sijui kama mtakuwa mnakumbuka huyu jamaa aliyeukimbiza ulimwengu katika Hisia za Burudani kupitia Track yake inayoitwa I DONT WANNA KNOW akiwa amemshirikisha Rapper P.DIDDY.

Jina lake anaitwa MARIO WINAS, na alikuwa ni moja kati ya wasanii ambao walikuwa wanapatikana katika Record Label ya BAD BOYS ambayo iko chini ya SEAN COMBS maarufu kama DIDDY, mpaka hivi sasa

Sasa Taarifa ambazo tuko nazo mpaka hivi sasa, ni kwamba mkali huyu ambaye hivi sasa ni kama imekuwa ngumu kwake "kufurukuta" katika Game la Muziki, amekutana na RUNGU LA SHERIA baada ya kushindwa kumuhudumia mtoto wake wa Kiume mwenye miaka 12.

Maafisa wa Polisi kutoka Jimbo la BERGEN huko huko Nchini Marekani, walimvaa bwana Mario Siku ya JUMATANO huko Nyumbani kwake FORT LEE na kumkamata kwa kosa la kushindwa kumhudumia mtoto huyo toka kipindi cha nyuma na mpaka kufikia kudaiwa kiasi cha USD 171,000 kitu ambacho ni kinyume na makubaliano ya hapo awali

Ukiachilia mbali suala hilo, Mario Winas aliwahi kukutana na Rungu la kukwepa Kulipa Kodi kuanzia mwaka 2008 mpaka 2012.

Hata hivyo, Mkali huyo wa R&B  mwenye miaka 43, huenda akachezea miaka 6 Jela kama hatosuluhisha mapema jambo hilo

SAY WHAT? : LIL WAYNE ANATARAJIA KUPATA MTOTO WA SITA?

2:16:00 AM Add Comment

Na Rich Sam   
WAUNGWANA kuna habari ambayo binafsi imenibidi niwaze na kukubaliana na akili yangu kuwa sasa ni muda wa kuishusha Kwenu Kabisa, na hii ni kuhusiana na Lil Wayne

Jicho la "Waungwana" hatimaye limebaini kabisa kuwa Rapper Lil Wayne anatarajia kupata Mtoto wa Sita Sasa, kama mwenyezi mungu atajalia kila Kitu.

"Chai" hiyo kuhusu ujauzito mwingine kutoka Kwa Mpenzi wa Hivi sasa wa Lil Wayne, anayeitwa DHEA, ilimwagika katika Birthday Partyu ya Lil wayne ambayo ilikuwa ni Ndogo tu na iliwahusisha washkaji kadhaa akiwemo mpenzi wake huyo wa Hivi sasa

Katika Pekenyua ptkenyua, Dhea alionekana akishoot Video kwa Njia ya Simu, akiwa amevalia Kigauni Cheupe ambacho kilionesha kabisa kuwa Dhea ni mjamzito

Iwapo atapatikana mtoto huyu, Basi atakuwa ni Mtoto wa 6 kutoka kwa Wanawake 6 Tofauti.

FRIDAY BAM !!! : DIAMOND PLATNUMZ FT MORGAN HERITAGE- HALLELUJA

1:54:00 AM Add Comment

Na Baba Juti   
WATU wa Mungu Diamond Platnumz kaachia Video Mpya ambayo hatuna Budi kushare na Wewe. Track Inaitwa HALELLUYA na ameshirikiana na Morgan Heritage Kutoka Jamaica

Itizame kupitia FRIDAY BAM!! ya Baba Juti Blog

ESMA PLATNUMZ: "MWISHO MTAKUJA KUSEMA NA DYLAN NI WA PETIT"

2:52:00 AM Add Comment

Na Insta Cop  
WAUNGWANA wa Kitanzania wasiopitwa na Jambo wameongea meeengi sana kuhusiana na Mupenzi ya Esma Platnumz kukunjuka kimahaba na Hamisa Mobeto, mara sijui ikawaje yaani vitu Moooob sana !!!

Lakini kama haitoshi, wakaanza kupost Picha zao, wakaandika Mengi, wakafunguka Mengi, wakafungua account Nyingi, wakaoanisha Picha kibao, lakini Jibu ndo basi limeshatolewa

Instagram account ya Esma ambaye ni Ndugu yake na Diamond Platnumz, ilikuwa ikitembelewa mara kwa mara kujua ni "Ndimu" gani atazikamua mama huyo lakini hiki ndicho alichoamua kukiamsha

MAHABA NIUE !! NIGARAGAZE !!! : FUTURE ATOA ZAWADI YA SAA YA ROLEX KWA MPENZI WAKE MPYA, JOIE CHAVIS AMBAYE PIA NI EX-WA BOW WOW

2:41:00 AM Add Comment
  
Na Baba Juti  
WAUNGWANA bwanaaaa...sasa naona Mahaba yameanza kunoga maana Future huwa hakawizi, na sifa yake kubwa ndiyo hiyo, na wala huwa hakuna ujanja ukishanasa katika Mtego wake.

Siku ya Jana, JOIE CHAVIS ambaye ni mama wa Mtoto wa BOW WOW na hivi sasa ni Mupenzi ya Rapper Future, alikuwa anasherekea Siku yake ya Kuzaliwa, nyie mnaitaga Birthday.

Kila kitu kilienda sawa, na mambo yakaenda Vizuri, keki ikakatwa, watu wakaimba, na ka-picha kake waka-kapost kama ambavyo ilivyo siku zote.

Lakini mambo ya keki hayatuhusu hata kidogo, bali linalotuhusu ni hili Hapa.... FUTURE, alikuwepo !!!!!.

Ingawa hakutaka kuonekana katika Videos ambazo zilikuwa zikirekodiwa pale ama picha ambazo zilikuwa zikipigwa pale, lakini alikuwepo kwa ajili ya kuhakikisha kuwa Mpenzi wake anakula bata la Kutosha na kila kitu kinaenda Fresh kabisa



Kitu ambacho kiliipamba Partyu hiyo, ilikuwa ni zawadi ya Saa ya Gharama aina ya ROLEX, ambayo Future ndiye aliitoa kwa Mrembo huyo ambaye mpaka hivi sasa bado anamchanganya akili Bow Wo

UMA SIO YA KEKI PEKE YAKE!!!!!: BINTI AMBAYE ALICHOMWA KWA "UMA" NA NICKI MINAJ, AJITOKEZA NA KUTOA SABABU AMBAYO ILIFANYA TUKIO HILO LITOKEE

2:30:00 AM Add Comment

Na Baba Juti   
#WatuWaMungu Siku ya Jana, yaani September 27, kulikuwa kuna jambo ambalo sijui kama mlikutana nalo ama inakuwa vipi...ni Kuhusu Nicki Minaj.

Infact, Nicki Minaj mwenyewe alikiri kupitia Instagram account yake kuwa aliwahi kumchoma na UMA alipokuwa na umri wa Miaka 11, kwa madai kuwa alimuingilia katika harakati zake na ilikuwa ni maeneo ambayo hakuna aliyetarajia kama lingetokea hilo

Nicki Minaj hakuyasema hayo tu, bali alimtaja mpaka jina binti huyo kuwa anaitwa DAMEKA WILLIAMS, huku akionekana kufurahia ama kuchekelea Tukio Hilo.

DAMEKA AJITOKEZA   
Baada ya kuona kuwa Nicki Minaj kamtaja na kuzungumzia namna alivyomdhuru huku akionekana kufurahia tukio hilo, Dameka mwenyewe alijitokeza kupitia Twitter account yake na kuporomosha maneno makali huku akionekana kukwazwa na namna ambavyo Minaj kalizungumiza suala hilo.

Dameka aliandika Hivi :
Kahaba Wewe unajivunia kufanya upuuzi huo?. Ulivuruga Party kwa kila mtu na bado ukaniacha na Kovu mguuni mwangu tangu uliponichoma na Uma"

SABABU IMETOLEWA   
Kama haitoshi, moja kati ya Followers wa Dameka, alimuandama Binti huyo ambaye kwa kusema kuwa yeye ndiye aliyeanza kumzingua Nicki.

Lakini katika kulifafanua hilo, Dameka alidai kuwa, yeye alimchana Live kwa kumwambia kuwa hawezi kuimba, labda ajikite katika Rap, na hapo ndipo kiliponuka zaidi.

Aliandika hivi :
"nilimuambia kuwa hawezi kuimba, hivyo ajikite zaidi katika Kurap, na ghafla akaanza kunirushia Ngumi"

ANACHEZEA SHARUBU ZA SIMBA!!!!: HUYU NDIYE MWANAMKE AL:IYEAMUA KUMDHALILISHA MTOTO WA LIL KIM...JE ...KITANUKA?

1:59:00 AM Add Comment

Na Baba Juti   
WATU wa Mungu kuna jambo ambalo sina hakika kama Dada yetu kutoka kwenye ulimwengu wa Hip Hop, LIL KIM, atalifurahia ENDAPO ATAPATA NAFASI YA KULIONA

Mwanamke mmoja ambaye jina lake halijafahamika, ameanza kuisumbua mitandao ya kijamii kwa kupost Picha za mtoto wa Rapper Lil Kim na kuanza kumfanyia masihala ambayo ni wengi sana wameonekana kutoyafurahia hata kidogo

Mwanamke huyo ambaye anayumia Instagram handle ya LOW CUT SAVAGE kunako instagram account yake, kiwizi wizi alionekana akimpiga picha na kushare kupitia Instagram Story, huku akionekana kabisa kumdhalilisha Binti huyo wa Rapper Lil Kim

Katika Picha tofauti tofauti ambazo Mwanamama huyo alizipost, ilikuwa ni pamoja na picha ambayo inamuonesha mtoto huyo akiwa na nywele ambazo zimechoka choka na kutaka kuonesha kuwa inaonekana Lil Kim hamjali Bint yake

TIZAMA PICHA HIZO





LADIES VIBE: KUTANA NA BAADHI YA BIDHAA ZA RIHANNA KWA AKINA DADA WANAOHITAJI UREMBO ZAIDI

5:32:00 AM Add Comment

Na Baba Juti  
WATU Wa Mungu hasa wale wenye Jinsia ya Kike, tunafahamu vizuri kabisa kuwa Hitmaker wa "DIAMONDS", Rihanna, ameamua kujitosa moja kwa moja katika Biashara

Na Biashara ambazo tunazifahamu anazofanya Rihanna ukiachilia mbali Muziki, ni pamoja na Slippers, Mavazi na safari hii kaamua kuwagusa akina Dada Vizuri kabisa kupitia Vipodozi

Sasa, Tumepita katika Account yake ya Kibiashara, tukakutana na huu mzigo ambao akina dada inabidi mjipange kuuchangamkia, kama mlivyochangamkia Slippers zake







MASIKINI POLE !!!: MJENGO WA JASON DERULO WAVAMIWA NA WEZI NA KUIBA USD 300,000

5:24:00 AM Add Comment

Na Baba Juti  
WATU Wa Mungu kuna waungwana Wengine huwa wanakuwa na "Huruma-less" hata kama umejipinda vipi ili kurekebisha maisha yako na mipango yako. Hawa wanaitwaga WEZI.

Jumba la Hitmaker wa "SWALLA" , Jason De Rulo limevunjwa na Wezi "Wasiofahamika" na kumkomba kiasi cha USD 300,000 na vito vya thamani kama vile Cheni, saa, Pete, nk.

Tukio hilo lilifanyika SEPTEMBER 22 huko maeneo ya TARZAN, LOS ANGELS, Marekani ambapo hakuna Mtu aliyejeruhiwa na Wakati huo Jason De Rulo hakiwepo eneo la Tukio, yaani alikuwa Nje ya Mji kwa ajili ya Kazi maalum

Polisi kutoka Los Angel (LAPD) wametoa Taarifa kuwa, Wezi hao walivunja na kuingia kupitia Dirishani na mlangoni, na kisha kwenda moja kwa moja mpaka Chumbani kwa Jason De Rulo na kukomba vitu hivyo.

Hata Hivyo mfanyakazi wa Ndani wa Mkali huyo, anasakwa ili kutoa maelezo maana inasemekana huenda akawa anahusika kwa namna moja ama nyingine

WOLOLO YAYEEEEE !!!: KUTANA NA MWANAMKE ALIYETENGENEZA HISTORIA YA KUWA NA KALIO "FEKI" AMBALO NI KUBWA KULIKO YOTE DUNIANI (PICHA)

5:12:00 AM Add Comment

Na Baba Juti  
WAUNGWANA tunaombeni mtupatie Ruhusa, kama ni sahihi kumpongeza ama inabidi tumkaushie maana nyie ndo mnaweza sema lolote juu ya hiki ambacho kinaonekana

NATASAH CROWN, raia wa SWEEDEN mwenye Miaka 24 kwa hivi sasa, ameingia katika Historia ya Kitabu cha GUINESS WORLD RECORDS kwa kuwa ni mwanamke mwqenye Kalio Kubwa la Kupandikiza, kuliko yeyote hapa Duniani.

Akizungumz\ia suala hilo kwa undani zaidi, Natsha ambaye Kalio hilo Feki lina ukubwa wa "Inchi Mzunguko" 72, amesema kuwa alifanya upandikizi wa kwanza akiwa na Miaka 20 tu

"Nilikuwa na Miaka 20 wakati nafanyiwa Upandikizi wa Mara ya Kwanza. Kitu ambacho huwa nakifanya kila nikiamka asubuhi ni kuliangalia Kalio langu kupitia Kioo"

Katika hali nyingine, Natasha amedai kuwa, kuwa na Kalio kubwa kiasi hicho, halimfanyi kujihisi Mzito, bali anajihisi ni mwepesi kabisa na anafikiria kuongeza ukubwa Zaidi"

   TIZAMA PICHA ZAKE    








MAMBO YA MKWANJA !!!!!! : QUAVO KUTOKA KUNDI LA THE MIGOS, NDIYE RAPPER WA KWANZA KUNUNUA SIMU MPYA YA I PHONE 8 PLUS?

3:16:00 AM Add Comment

Na Baba Juti   
#WatuWaMungu Hatari ya I PHONE 8 PLUS kila mtu anaifahamu sasa hivi, maana watu wameanza kutengeneza historia zao sasa hivi

Katika Historia ya Muziki wa Rap, ama Hip Hop, kuna vingi sana huwa vinatengenezwa na hata kufikia kuandikwa kama sehemu ya Historia. Lakini kama ulikuwa hujui, kuna hii ambayo Quavo kutoka The Migos kaitengeneza aisee

Rapper Quavo, amekuwa ni Rapper wa Kwanza kununua Simu hiyo kali na ya gharama kuliko maelezo, ya I PHONE 8 PLUS

TUMEZINYAKA AISEE !!!! : U-BONGE NDIO UNAOMFANYA MARIAH CAREY ASHINDWE KUIMBA

1:14:00 AM Add Comment

Na Rich Sam    
WAUNGWANA Buana, huwa hawapitwi na jambo hata kidogo. We ficha unavyoweza kuficha lakini mwisho wa siku kila kitu kitakuwa hadharani Tu.

Hatimaye sababu nyingine kubwa inayomfanya Mariah Carey apoteze ubora na kiwango chake cha kuimba na hata kutoa ile sauti Nzuri, imewekwa hadharani safari hii

Kwa mujibu wa Taarifa Halisi bila chenga wala hofu hofu kutoka kwa mmoja kati ya Kitengo cha management cha Mariah Carey, inasemekana kuwa, Mariah amekuwa ni Mtu ambaye anajiachia vya kutosha, kitu ambacho kimekuwa kikimfanya ashindwekufanya majukumu yake hasa ya kimuziki.

Hilo pia limekuja kuthibitishwa na Picha za hivi karibuni ambazo zilimuonesha Mariah Carey akiwa Bonge , wakati akitoka kwenye Birthday ya Miaka 44 ya Jermain Dupri, moja kati ya Producers ambao wamemuweka Mariah Carey katika Ramani nzuri ya Muziki

HAKI YA MBONGOOO !!! : MKE WA T.I ADAI MUMEWE HAVAI VIATU VYA KUMFANYA AWE MREFU

3:20:00 AM Add Comment

Na Baba Juti. 
KAMA huwezi kumtetea Mumeo ama Boyfriend wako, basi usidhani wengine wanaweza kumkandia ama kuacha kumtetea. wako serious in love

Mke wa T.I, Tameka Harris maarufu kama Tinny, ameamua kuwatolea uvivu wale wote ambao wanamzunguimiza kuwa ni Kifupi Nyundo, na ndio maan hupenda kutengeneza urefu wake kwa kuweka baadhi ya vitu maalumu vya kumfanya aonekane mrefu hasa kupitia Viatu vyake

Sakata hilo lilianzaishwa na Wendy Williams maarufu kwa kuwakosoa watu maarufu Nchini humo, ikiwa ni baada ya yeye kuambiwa kuwa amepigwa Pasi.

Katika kulifafanua sasa suala Hilo, Mke wa T.I ameweka wazi kuwa, amekuwa akiishi na T.I kwa Miaka 16, lakini hajawahi kuona hivyo vifaa vya kurefusha kupitia Viatu, maarufu kama Shoes Lift, labda kama alikuwa anamficha.

Katika kukazia Zaidi, Tinny amedai kuwa T. I anajiamini akiwa yeye kama yeye na ukizingatia yeye ni mwanaume. Hivyo jalishi kama urefu wake ni kwenda juu au kwenda chini.

Na katika kuzungumzia Bifu la Mumewe na huyo Bi Mkubwa Wendy, alidai kuwa anatamani kabisa watu wasimuhusishe mumewe na Mabifu ya Kijinga ambayo hayana Faida kama Hayo

UBAGUZI NDIO BASI TENA!!!!?: ARIANA GRANDE AMTIMUA DANCER KIONGOZI WAKE KWA KUTUMIA NENO NI*****

2:38:00 AM Add Comment

Na Baba Juti   
#WatuWa Mungu wenyewe mtatuambia kama hii adhabu iliyotolewa ilikuwa ni sawa ama ilikuwa ni ya kiuonevu

ARIANA GRANDE, ameamua kumfukuza kazi Dancer-Kiongozi wake kwa kitendo cha Kutumia N-WORD (NIGGA) kunako katika account yake ya mtandao wa Kijamii

Kwa mujibu wa Taarifa za kichini chini zinafafanua kuwa, uamuzi huo ulichukuliwa na Ariana kutokana na yeye kutokuruhusu suala lolote la kibaguzi katika Maisha yake na hata katika Kazi yake ya aina yoyote ile.

LADY CULTURAL ambaye inasemekana ni moja kati ya viungo muhimu sana katika Timu ya Ariana Grande hasa katika Upande wa Kucheza, aliandika neno hilo kama Caption katika Instagram Story yake, na hapo ndipo dude lilipoamshiwa

Kwa Upande wake Lady Cultural, aliamua kuweka wazi kile ambacho amekisikia, sasa kupitia instagram account hiyo hiyo, aliamua kujitetea kama ifuatavyo

"Kusema ninampenda huyu N***, haimaanishi kukufanya wewe uwe mbaguzi. Unatakiwa kuelewa kinachosemwa. Kama ningesema Ninawachukia Watu Weusi, hiyo ni Ubaguzi wa moja kwa moja. Ni Vitu viwili tofauti. Na kusema jina hilo ama neno hilo, haikufanyi kuwa mbaguzi. Binafsi sikubali maana mie sio mbaguzi. Hata Hivyo, Marafiki zangu weusi hawajaonesha kumaindi chochote. Wote wanapenda na kufurahia nikilitamka hilo neno"

HAKI YA MUNGU MMEKWISHA !!!: KUTANA NA KAHABA AMBAYE HUVUNA MKWANJA MWINGI NA NI KINARA WA KUFANYA UKAHABA KUPITIA GARI ZA USAFIRI AINA YA UBER

3:02:00 AM Add Comment

Na Baba Juti  
KIBONGO BONGO najua Madreva "Boda Boda " ndo huwa wanakutana sana na timbwili la "Makahaba" amba huwafanya hata kusahau kabisa kuwatoza mkwanja.

Hata wale ambao ni Madreva Tax pia hapa Bongo, huwa wanakumbana na mizigo ya aina hii, ambapo wanambeba binti halafu mwisho wa siku , akimfikisha semeu, anamwambia hana hela, labda ampe "Dudu", na kwa wale wenye ukata, basi hujikuta wakisafisha haja yao kwa "kuwatindua"

Sasa Nchini Marekani bwana, kuna huyu bibie ambaye kajichukulia umaarufu na hata nafasi namba moja kwa kuwa "Kahaba" ambaye huwatumia Madreva UBER kupiga safari zake bure, na kisha wanatoa mkwanja bila wao kutarajia.

Wamempachika jina la KAHABA WA UBER, maana jina lake halijafahamika Mpaka Hivi sasa, lakini mkwanja ambao anauvuna huwezi kuamini aisee

Binti huyu hutumia mbinu kadha wa kadha kabla hujatoa Hela lakini ni tayari anakuwa ameshaingia ndani ya Gari la Uber

   NJIA ANAZOTUMIA   
  • Anakuimbisha Kule anakoenda kwa sauti laini, na kila aina ya Mitego
  • Mkishaingia kwenye Gari, Style ya Kukaa tu, mwenye utashusha mikono, inaitwa BFFU (But First For You)
  • Baada ya hapo, huruhusu mapaja yake yakuchangany akili, hasa wakati unaongea naye na hata kuwasha Gari
  • Kisha atakuambia uweke wimbo anaoutaka, na unakuwa ni wimbo ambao umetawaliwa na maneno ya ngono, na kisha huanza kuimba huku akicheza
  • Huanza kucheza Style kadha wa kadha huku akitikisa "Kalio", style ambayo huitwa TWERK
  • Baada ya Hapo, huchukua Selfie ya kila kinachotke huku akikushawishi ujaribu japo kumshika unapopataka wewe Dreva
  • Baada ya hapo, huanza kukuambia Bei, na huanzia chini kabisa ambapo lazima utakuwa unakubali, na ukifikia Bei yake, imekula kwako.
  • Utakachokuwa umekosea, ni pale utakapomruhusu aondoke  na video clips, maana anatishia kuzivujisha..au uwe unamchapa kila siku

VIDEO: INASIKITISHA SANA... HIVI NDIVYO RAFIKI WA KARIBU WA DRAKE ALIVYOUAWA KINYAMA

2:33:00 AM Add Comment

Na Rich Sam & Insta Cop  
#WatuWaMungu tunaamini kabisa litakuwa ni pigo moja kubwa sana kwa Rapper Drake na Familia nzima ya OVO ikiwa ni baada ya kupatwa na Msiba wa mwanafamilia wao anayeitwa Anthony Soares – aka “FIF”

Tukio hilo liliwekwa Wazi siku kama sita hivi zilizopita na Rapper Drake ambaye alionekana kuumizwa sana na Kifo hicho cha moja kati ya Marafiki zake wa Karibu ambaye pia muda mwingi alikuwa Torronto.

SIKU ya jana, Video ya namna FIF alivyouawa hatimaye imewekwa Hadharani , ambapo alionekana katika Chumba Fulani hivi (haifahamiki kama ni ATM au lah, akifanya shughuli fulani huku mkononi kashika Glas ya Juice.

Baada ya Sekunde kadhaa walionekana vijana wawili, mmoja akiwa amevalia sweta la Blue na Mwingine sweta la Rangi ya Damu ya Mzee, na kuanza kumfyatulia Risasi, kitendo ambacho hakikuchukua hata Dakika moja, na kisha wawili hao kukimbia.

Video Mbili ambazo zimachiwa na TORRONTO POLICE SERVICES ziliweza kuwaonesha wawili hao wakihakikisha wamemshambulia FIF mpaka umauti kumkuta na kisha kuondoka na Gari Jeupe aina ya Ford

Mpaka Hivi sasa haijawekwa wazi chanzo cha Mauaji hayo

IKUMBUKWE
SIKU ya Jana, Drake alionesha Tattoo amabyo aliichora maalum kabisa kwa kumuenzi Rafiki yake huyo

MNADA BANNER