REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

HATARI ZAIDI YA DANGER: WANAWAKE KUJIFUNGUA PEKE YAO BILA DAKTARI, KATIKA MAZINGIRA YA PORINI, KISA ..REALITY TV SHOW...(Kumradhi kwa Picha Zitakazoonekana)

8:32:00 AM Add Comment

HII SASA IMEKUWA NI ZAIDI YA TUNACHITA “Utafutaji Wa Pesa”..Iko hivi…

Katika Reality Show Moja Nchini Marekani, inatarajia kuwaonesha akina Mama wakijifungua Bila Msaada Wowote wa daktari, katika Meneo yanayozungukwa na Asili ya Mwitu ama Pori


Kwa mujibu wa Info ambazo zimetufikia TTM, Producers ambao wanaandaa kipindi hicho, wamedai kuwa kitendo hicho Usalama lazima Utakuwepo katika mazingira hao, huku Timu Nzima ya Uandaaji wa Reality Show hiyo ikiwepo eneo la Tukio, huku MADAKTARI wakikosekana na hawatoruhusiwa kuwepo.


Aidha Wameongeza kuwa, Dhamira ya Kipindi ama Mfululizo wa matukio hayo, ni kwamba “Mwanamke anaweza kujifungua Mtoto wake Mwenyewe, huku akiwa amezungukwa na mazingira ya Asili Tupu, na Sio Hospitali”



Licha ya kuonekana Kupendwa sana na baadhi ya watu katika Mtandao wa YOUTUBE, baadhi ya wataalamu wamedai kuwa, Kitendo hicho ni hatari sana hasa ukizingatia Madhara ambayo yanaweza kutokea endapo Mzazi atashindwa Kujifungua, pamoja na Mtoto Mwenyewe

KANYE WEST HAMUELEWI KABISA KIM KARDASHIAN JUU YA NORTH WEST…

2:09:00 AM Add Comment

NEW YORK , Marekani.
KAMA Utakuwa huchezi mbali na TTM, basi utakuwa unafahamu vizuri kabisa kuwa rapper Kanye west hapatani hata Kidogo na Mapaparazi, sasa Kuna hili Toka Chimbua Chimbua.


Kubali Ukatae Kanye West ameshaanza kuwa na mashaka mazito juu ya Usalama na Mtoto wake NORTH WEST baada ya kuonekana sana hadharani katika Kipindi cha Mchakato wa kufunga Ndoa, ambao ulihitimishwa Mwezi Uliopita.

Kwa mujibu wa chanzo kilichopo karibu na Wanandoa hao, Kimedai kuwa, Kanye West na Mkewe Kim kardashian wamekuwa wakibishana sana na hata kukwaruzana kuhusu Ishu ya Mtoto wao kuonekana hadharani na kupigwa picha Ovyo na Mapaparazi, jambo ambalo Kanye hapendi na walishakubaliana Awali kuwa tukio hilo lisifanyike hata kidogo.

Aidha Kanye alimchana Kim Kardashian kuwa, Hivi sasa Mchakato wa Ndoa umeisha, Hivyo haturuhusu Mtoto wake aonekane hadharani hata kidogo, na hata Picha zake hazitakiwi kuzagaa Mitandaoni Bila Idhini yake ama sababu maalum.


Tofauti na Hilo, Pia Yeezy amepiga marufuku North West kuonekana katika Kipindi cha KEEPING UP WITH THE KARDASHIANS, kinachoongozwa na Kim Mwenyewe.

TWITTER SASA KUPATIKANA KATIKA TV YAKO…

2:05:00 AM Add Comment

Kampuni ya Microsoft imezidi kujitengezea Mazingira yake bora zaidi ya kibiashara, baada ya Kuanza Mchakato wa kuingiza Sokoni Mfumo wa Kupatikana kwa Twitter katika Luninga yako.


Microsoft kupitia XBOX, safari hii itaonesha Tweets kadhaa kwa Upannde wa Chini wa Luninga ama TV yako.



Aidha taarifa Zinaelezakuwa, Tweets Hizo ambazo zitakuwa Zikionekana katika Luninga yako, Ni zile ambazo zitakuwa zinahusiana na Chanel lama Show ambayo unaitizama wakati huo, Mfano ukiwa Unatizama Kipindi cha JAM SESSION, Basi, Tweets zinazohusu kipindi hicho, zitakuwa Zikionekana mara kadhaa..

FASHI-TOUCHEZ: BAADA YA KUVAA KILE KIGAUNI CHENYE UTATA...NOW, HUYU HAPA RIHANNA..TENAAAAAA !!!!

2:01:00 AM Add Comment

Na Purhiya Mahmood
Rihanna alionekana Tofauti sana ndani ya vazi hili, ikiwa ni baada ya Kukandiwa kuvaa Kigauni Fulani hivi kilichomuonesha Kila Hazina aliyokuwa nayo kasoro tu..ile Muhimu sana

Sasa, wakati jana anaenda Ku-present Perfume yake ya ROGUE katika Jengo la SEPHORA, Riri aliwashtua wengi kuonekana amevaa vazi hili ambalo lilimfunika Sehemu Kubwa ya Mwili wake

Check alivyopendeza…













HII NI MOJA YA ACTION ITAKAYOPATIKANA KATIKA FAST & FURIOUS 7

1:51:00 AM Add Comment









USHER RAYMOND NA TYGA WALIVYOZAMA KWA CHRIS BROWN

1:45:00 AM Add Comment

CALIFONIA, Marekani.
KutokaGerezani  Kwa Chris Brown kumekuwa Ni kitu cha Kufuatiliwa Sana, ili kufahamu ni Mchakato gani ambao unaendelea kwa hivi sasa, ila Kitengo kisicholala cha Chimbua Chimbua,, kimeshusha Ripoti yake ya Kwanza kama ambavyo TTM tunaishusha kwako Pia.

Breezy alipata Ugeni wa Kwanza wa kimya Kimya kutoka Kwa marafiki zake, Usher Raymond na rapper Tyga akiwakilisha Kundi la YMCMB, Jumanne ya Wiki Hii, katika maskani yake ya ENCINO, CALIFONIA.

Aidha baada ya kufika Nyumbani kwa Breezy, inasemekana kuwa watatu hao walitumia Muda mwingi kupiga Stori za hapa na pale, huku wakienjoy Mchezo wa basket ball ama Mpira wa Kikapu hapo hapo maskani kwa Chris Brown.

Kama Ulikuwa hufahamu vizuri, Tyga na Chris Brown wameshirikiana katika Mikwaju kadhaa ikiwemo DEUCES, HOLLA AT ME, na Loyal ambayo inafanya Vizuri sana katika Soko la Muziki nna Media Mbali mbali hapa Ulimwenguni.

Tofauti na Tyga, Usher Raymond alitangaza awali kuwa, anashirikiana na Chris Breezy katika Albam yake Mpya ambayo itaingia Sokoni Pindi itakapokuwa Tayari


Chris Breezy ametumikia Siku 108 Jela kati ya Siku 131 tangia March 24 Mwaka Huu,  ambazo alihukumiwa kwa Makosa kadhaa ikiwemo kukiuka Adhabu alizokuwa amepewa na mahakama Dhidi ya makosa mbali mbali likiwemo lile la kuswapua makofi Ex-baby wake Rihanna

MNADA BANNER