REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

KUTANA NA TALLIA STORM, BINTI ALIYEPIGA KIBUTI NA MTOTO WA DAVID BEKHAM.

7:19:00 AM Add Comment

KWELI kabisa, Wahenga hawakuwahi kukosea hata Kidogo, maana Penzi likiwa linachanua kama Maua, basi huwa Tamu Balaa, lakini Likinyauka na kukauka kabisa, nbasi Maumivu lazima uyaone

TALLIA STORM Ni Binti Mwenye Umri wa Miaka 18, na Ni Msanii wa Pop Huko Uingereza, ila alijikuta akiingia katika Headlines zaidi baada ya kuanza Mahusiano ya Kimapenzi na Mtoto wa David Bekham, BROOKLYN BEKHAM

Lakini Baada ya Muda kadhaa, Mtoto wa Bekham alimpiga Chini Tallia na Kumuachia Kovu kubwa ndani ya Moyo wake, huku Brooklyn akiendelea na Mahusiano mengine na Binti Mwingine

Sasa, Baada ya kubaini kuwa Ex Wake Tayari yupo na mahusiano Mengine, Tallia aliamua kuaamsha naye katika Njia Nyingine kwa Kumrushia Madongo ya Nje nje japo sio kwa sauti kubwa, bali ni kwa Ujumbe tu

Katika Picha ya Hivi karibuni, Tallia alipost Picha ya Dongo kwa Mtoto huyo wa Bekham iliyokuwa imeandikwa “I DATE MEN NOT BOYS”. Sasa ukichukua Ujumbe huo, unabaini kabisa kuwa ni Dongo la moja kwa Moja kwa Brooklyn Bekham, maana yeye bado ana Umri wa “Boys”

“Baada ya Kuachana, nilimuona Brooklyn (Mtoto wa Bekham) Backstage ya Tuzo za BRITISH AWARDS. Ulikuwa ni Usiku mkubwa sana kwangu. Alijaribu kunisemesha ila Sikuwa na Muda, maana ni Mpenda Drama Sana. Ninahisi watu wengi waliona Mahusiano yetu. Lakini hivi sasa Sitaki mahusiano na Watoto, bali Wanaume” Alisema Tallia

Ila akizungumzia Kipindi cha mahaba yao, Tallia anadai kuwa, ingawa Walikuwa na Mahaba ya Kitoto zaidi, ila walijitahidi sana kuyafanya yawe ya siri zaidi. Na watu wangewaona Pamoja tu labda wakiwa wametoka Out



#DakaHiiFasta: MWANASHERIA WA YOUNG THUG AMUOKOA KATIKA KESI YA TANGU MWAKA 2015

6:44:00 AM Add Comment

KUNA kila Sababu kwa Rapper Young Thug Kumshukuru Vilivyo Mwanasheria wake ambaye amemsaidia vizuri kisheria mpaka kuepukana na Kesi ambayo Ilikuwa inamkabili

July Mwaka 2015, Mjengo wa Young Thug ulifanyiwa Msako Heavy na Polisi na taarifa kutolewa kuwa, Dawa za Kulevya aina ya COCAIN pamoja na Bastola, kitu ambacho ni Kinyume cha Sheria.

Kutokana na Tukio Hilo, Young Thug alifunguliwa mashtaka baada ya kubainika kuwa ni Kweli alikutwa na Vitu kama Hivyo Nyumbani kwake

Lakini kama “zari” vile, Mwanasheria wake alimtetea kwa kutoa Taarifa kuwa, Polisi walivamia Nyumba ya Mteja wake na kufanya Upekuzi bila Utaratibu maalum, yaani walitumia mammlaka ambayo haitambuliki Kisheria

Bada ya Swali hilo kurushwa mpaka kwa Mammlaka maalum, ilibainika kabisa kuwa ni Kweli, Nyumba ya Young Thug ilifanyiwa Ukaguzi kinyume na Utaratibu, hivyo Young Thug akawa ameponea hapo

BONUS………….

YOUNG THUG ni Jina la Kutaftia Ugali, lakini Jina Lake Kamili likiwa ni JEFFERY LAMAR WILLIAMS. Alizaliwa AUGUST 16, 1991 Huko Atlanta Georgia, USA

MNADA BANNER